Taja madeni yako: Je, unadaiwa kiasi/ kitu gani?

Taja madeni yako: Je, unadaiwa kiasi/ kitu gani?

Wanasema kwamba hata uwe tajiri vipi huwezi kukosa deni. Lazima kutakuwa na mtu, kampuni/ benki inayokudai.

Wengine wanafika mbali zaidi na kusema kama mtu unaogopa kukopa na kudaiwa, basi huwezi kuwa na mafanikio.

Je, wewe hapo kwa sasa unadaiwa nini? Kama ni pesa, ni kiasi gani?

Binafsi hapa nilipo nipo na madeni haya:

-Tala=45,000
-Tigo =36,000
-Airtel =37,000
-Branch=6,000
-Nadaiwa bili ya maji 9,200, hii leo nitailipa.
-Nadaiwa na jamaa 35,000.
-Nadaiwa hela ya posa milioni 1 na laki 3, kati ya milioni 1 na laki 5, nilitoa laki 2 tu.


Hayo ndiyo madeni yangu hayo ya juu ukitoa matatu ya mwisho, yameshakuwa sugu sasa.


Cc Zero iq
20191118_191645.png
20191118_191645.png
 
Watu mbalimbali: 57.4M, TRA: 18M (ambazo sitowalipa), na1200$ ambazo zinaninyima usingizi namna ya kuzilipa. Eh Mwenyezi Mungu nisaidie nilipe madeni yote. Amen
ulikopa wapi namimi nikakope mkuu?
 
Voda Mpawa 125K yaani sina raha kila siku kupokea simu na sms za vitisho kutoka kwao najua nimepitiliza muda ila nitailipa.


Mpendwa mteja, MPAWA, Kila jambo lina mwisho. Mkopo tuliokupa sio kiwango cha mwisho, Ila marejesho yake tulikuekea mwisho wa kufanya. Umekaidi,Umedharau,Umepuuzia, Tafsiri yako kwetu ni mteja anaetaka kutapeli kampuni. Mwisho wa ubaya ni Aibu, HATUTAKI KUKUAIBISHA AU KUKUDHALILISHA KWA MKOPO MDOGO. Bonyeza *150*00#KULIPA LEO HII.
Pole mkuu
tapatalk_1574095069412.jpeg
 
Back
Top Bottom