Supu ya kokoto
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 4,194
- 7,602
Huo ukanda wa ntimaru,nyamagongwi,kwiribha na kuelekea vilima vya maeta jirani na MTO tebesi kuna upuuzi mwingi sana.Yes. Mambo ni bambam.
Ukisikia yowe inapigwa ukiwa juu ya paa ya nyumba unaezeka, usishuke na wala usiende huko kwenye yowe. Ukienda linaweza kukukuta balaa hutasahau.
Siku moja ilipigwa yowe watu wakiwa wanafuatilia wezi wa ng'ombe. Jamaa mmoja aliyekuwa juu ya paa anaezeka, akashuka na kwenda kusaidia kufuata nyayo za wezi. Alipofika kule watu wakamfananisha na mwizi wakaanza kumpiga.
Kaka yake asingekuwepo aingilie kati, huenda wafuata nyayo wangemuua. Hii ni kutoka Ntimaru (Kenya) mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Umejuaje mkuu mimi mchagga ila ukiniona huwezi kujua.we mchaga
Asante kwa nyongeza mkuu. Bila shaka wewe ni mtu kutoka "Kanda Maalumu" Hiyo namba 3 hata kwetu ipo (unaacha kamba hadi mfugo ukipatikana kamba hiyo itatumika kuufunga). Hiyo ya kutooa binti asiyekeketwa au binti huyo kuzaa, ni kutoka kanda maalumu kabisa.
Halafu hiyo ya mtoto kutompiga baba yake kama ikitokea inakuwa ni laana inayoendelea kizazi hadi kizazi hadi lifanyike tambiko maalumu kuitengua.
Ni hivi ukimpig baba yako, nawe pia utapigwa na watoto wako nao watakaokupiga nao wao pia watapigwa tu....yaani unakuwa ni mwendelezo wa milele.
Hii nimeishuhudia pale kijijini kwetu. Kuna mzee mmoja alikuwa akimpiga baba yake. Naye watoto wake walimpiga na wale watoto wake waliompiga nao pia walipigwa na wao pia wanapigwa. Ni laana isiyofutika hadi tambiko lifanyike kutengua laana hiyo.
Hii dhambi nimeishuhudia pale kijijini kwetu hiki ni kizazi cha 3 sasa bado hali hii inaendelea kujirudia. Wazazi wanapigwa hatari!Hiyo ya kumpiga mzazi huwa ni vizazi vinne viishe ndipo nayo hukoma!
Ni mwiko mgeni kula firigisi ugenini kwa mkurya
Sahihi, nyingi ni mila za kijima tuSidhani kama ni miiko kweli kwamba utapata mabalaa hapana.
Bali ni taratibu au malezi ya kumjengea mtu tabia nzuri tu naamini tukizifuata hizo basi ni wazi tutakuwa na jamii Bora sana.
Kuhusu Jogoo kuwika nje ya muda tuliouzoea ni dhahania tu, kwakuwa viumbe nao huwa wanaota ndoto kama ilivyo kwa binadamu.
Bundi ni Moja ya ndege wasiopendwa na jamii nyingi kwakuwa yeye mawindo yake huyafanya usiku kama ilivyo kwa baadhi ya viumbe,pia wanahusishwa zaidi na ushirikina, lakini ni ndege wa kawaida hata akilia karibu yako sidhani kama Kuna ishu yeyote.
Asante kwa nyongeza mkuu. Pia:1. Mwiko wa Ugali ukivunjika wakati Ugali unasongwa. Mwanaume haruhusiwi kula huo Ugali (labda asongewe mwingine).
2. Ni marufuku kumuachia sahani Mkubwa wako mkiwa mnakula pamoja hata kama umeshiba kabla yake.
3. Hutakiwi kutaja neno Chumvi wakati wa usiku (Badala yake sema Dawa ya Mboga) [emoji23]
4. Mkiwa meza moja ni marufuku kuanza kula kabla ya wakubwa zako. Wataanza wao kushika kijiko na kula ndio utafuata wewe.
5. Kiganja cha mkono wa Kushoto kikikuwasha, ni dalili za kupokea hela hiyo siku. Cha mkono wa Kulia kikikuwasha, ni dalili za kutoa/kupoteza hela.
6. Ikitokea umejikwaa mlangoni wakati wa kutoka nje halafu kuna safari ulikua umepanga hiyo siku, unatakiwa uhairishe kwenda mara moja. Haitakua salama kwako.
7. Ndege akikunyea ni ishara ya Bahati nzuri.
8. Ukipaliwa ghafla wakati wa kula basi jua kuna mtu anakusema vibaya muda huo huo unaokula.
9. Jicho la kushoto likikucheza ni machale. Kwahiyo kama kuna magendo unafanya mahali/ au upo mahali ambapo hutakiwi kuwepo basi ondoka haraka sana utakamatwa!
10. Mtu mzima akianguka bafuni ni ishara mbaya sana. (Wanasema hana muda mrefu wa kuishi).
11. Ni marufuku kumpiga mtoto mdogo wa Kiume kwa nguo. Atakosa Mke [emoji23]
Na Mimi huwa nakerwa sana na hiyo tabia. Tena, wakati mwingine, unakuta anayefanya hivyo ni mtu anayehesabiwa kama mmoja wa "waheshimiwa".- kujichokonowa pua mbele za watu. Ni tabia ambayo kwetu haijwahi kukubalika kuanzia kwa watoto wadogo mpaka watu wazima. Kwetu Pwani.
Imefikia mpaka mimi siikubali kabisa na nashindwa kujizuwia mtu akijichokonowa mbele yangu, nampa wazi, nendachooni jichokonowe mpaka uchoke kisha nawa mikono yako kwa sabuni, usije kuwapa watu mkonoau kutushikia vitu na mauchafu yako.
Kinyaa.
Sikupingi ila nakuliza tu....hivi umesha wahi patwa na mafua makali kitambaa kimoja kikawa hakitoshi ..... tena uwe maeneo ya arusha au njombe kwnye baridiNa Mimi huwa nakerwa sana na hiyo tabia. Tena, wakati mwingine, unakuta anayefanya hivyo ni mtu anayehesabiwa kama mmoja wa "waheshimiwa".
Hiyo ni sambamba na tabia ya kupenga kamasi kwa kubinya pua bila kuwa na leso. Nilikuwa nafikiri ni watu wasiosoma tu ndiyo wenye hiyo tabia. Nimeshangaa hivi majuzi kumshuhudia Engineer mmoja naye akipenga kamasi kwa staili hiyo.
Huwa nakereka sana.
[emoji23][emoji23][emoji23]hiiii mpyaaaaaaaaSisi wapare haturuhusiwi kufanya mapenzi kabla ya ndoa
Arusha ndiko nilikozaliwa na kukukulia. Na kuna nyakati ambazo ni kama misimu ya mafua huko, hasa nyakati za baridi. Lakini tokea nilipoanza kutumia leso, nafikiri ilikuwa darasa la kwanza au la pili, sikumbuki kama nilishawahi kukosa leso ya kupengea kamasi. Nilipokuwa sina hela ya kununulia ya dukani, nilikuwa nikijitengenezea kwa kutumia nguo zilizochakaa. Na wakati nilipokuwa na mafua, kikishachafuka, nilikuwa nikiifua na kuilazimisha kukauka haraka. Ilikuwa nikiishaifua, naikamua na kisha kuifungia kisogoni ili ikaushwe na joto la mwili. Kwa hiyo muda mfupi tu baada ya kufuliwa inakuwa tayari kwa matumizi.Sikupingi ila nakuliza tu....hivi umesha wahi patwa na mafua makali kitambaa kimoja kikawa hakitoshi ..... tena uwe maeneo ya arusha au njombe kwnye baridi
Hii nafikiri ni ndani ya Morogoro kama nitakuwa sahihi...1. Ni mwiko kuingia shamba la mtu la miwa au mahindi na kuvunja Kisha kuondoka nayo, inaruhusiwa kama ni miwa basi ikate kdhaa, kaa humohumo shambani kula Kisha uondoke au kama ni mahindi unaruhusiwa kuwasha moto kwenye hilo shamba Kisha kata mahindi yanayokutosheleza kula na kushiba Kisha choma kula maliza, zima moto na uondoke.
2. Mwiko kuhadithia hadithi mchana, utaota mkia.
3. Kwenye ukoo wetu kula utumbo wa mnyama yeyote mwenye miguu minne ni mwiko.
4. Ni mwiko Kupuliza moto kwa pamoja na ikitokea mmepuliza pamoja mmoja anatakiwa kutema mate juu na mwingine chini. Inaaminika msipofanya hivyo basi mtakuja kufa kwa siku moja.
5. Kuna mchezo mmoja tunauita 'buriburi' mnaketi chini kwa mzunguko kunakuwa na kimkaa au kijiwe unakificha kwa mikono nyuma na unaitoa mbele anayekufuatia anaonesha umekificha mkono gani, akipata unampa anaendelea yeye na anayemfuata hivyohivyo. Akikosa basi unakuwa ni ushindi na unaendelea kucheza. Sasa mkitaka kuanza kucheza ni lazima aanzishe mtu ambaye baba yake au mama yake alishatangulia mbele ya haki. Kama wote Wana wazazi basi mtoto wa mwisho kuzaliwa aliyepo hapo ndio huanzisha huo mchezo. Kwahiyo ni mwiko kwa mtu yeyote tu kuanzisha huo mchezo.
6. Kusonta kaburi na kidole ni mwiko.
7. Mwiko kulima usiku yaani jua likizama huruhusiwi kulima.
8. Kupanda mbegu shambani kwa kifaa chenye masizi ni mwiko, huashiria mbegu kutokuota maana ni kama unapanda mbegu zilizokaangwa.
9. Ni mwiko kumruka mtu, ikitokea inabidi urudi kwa kumruka kuelekea ulikotoka (kurudisha mruko [emoji4])
Ipo miiko mingi sana sana. Naweza Andika Kitabu.
Hatakusumbua, atakusalimia na kukupa pole.Asante kwa nyongeza mkuu. Ila hizo namba 1, 4 na 5 zimenitisha. Na ikitokea mmiliki wa miwa au mahindi akakukuta kwenye shamba lake inakuaje? Anakupongeza au anakuchukulia hatua? Je, akikuchukulia hatua yeye atapata madhira gani?
Na hilo la kumvuka mtu naona lipo kariba kwenye makabila yote aisee!
Asante mkuu, umenikumbusha kitu:Hii nafikiri ni ndani ya Morogoro kama nitakuwa sahihi...
Sambamba na yote hapo, pia...
1. Ni mwiko kuingia shamba lenye mahindi baada ya kunyolewa, mpaka siku ya pili.
2. Ni mwiko kuburuza kuni au kamba na kuingia nayo ndani.
3. Ni mwiko kusimama wakati wakubwa wamekaa, au kukaa wakati wakubwa wamesimama.
4. Ni mwiko kukalia kaburi.
5. Ni mwiko kuacha mchi kwenye kinu usiku.
6. Ni mwiko kuua chura, mbayuwayu na vunjachungu.
7. Ni mwiko kukaa au kusimama mlangoni.
8. Ni mwiko kutokea dirishani.
9. Ni mwiko kupima kimo cha MTU kwa kiganja, tumia kiwiko.
10. Tuna majina ya Mizimu ambayo ni mwiko kutamka kwa kujifurahisha au kujiapiza huku unajua unadanganya, YATAKUFIKA TU UTAJUTIA.
11. Ukiwa na njaa njiani, ingia shambani kwa MTU, kata muwa au chimba muhogo ule ila usitoke nao, hata kipande kimoja. Ikiwezekana panda pegu.
12. Usiache nguo usiku nje, ulizofua.
13. Usilipite kaburi la babu au chifu bila kukata jani lolote na kuliweka juu ya kaburi. Hasa kama ni wa ukoo wako.
14. Ni mwiko kutupa chakula, hakikisha unakimaliza au unatafuta MTU.
15. Usimruke mtoto.
16. Usiimbe wala kuongea chooni, au kupiga mluzi.
17. Ni mwiko kumpiga mtoto kwa fagio.
18. Ni mwiko kuchezea chakula, hata kama hutakitupa. Mfano kulirusharusha tonge kisha ule.
19. Ni mwiko kurusha chochote nje kutokea ndani.
20. Ni mwiko kutoka au kuingia ndani ya nyumba kwa kukimbia.
21.....