SteveMollel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 8,797
- 25,177
Daniel alifanikiwa kuuona mwaka mpya lakini hakumaliza hata robo ya siku katika mwaka huo.
Ikiwa ni alfajiri ya saa kumi na moja, siku ya Ijumaa ya tarehe 1 January 2021, Dan alikuwa njiani kuelekea nyumbani kwake akitokea Club Tent ambapo alikuwa anasheherekea 'kuuona mwaka mpya'.
Ndani ya gari alilokuwa anatembea nalo siku hiyo, volkswagen nyeupe (golf mk8), alikuwa na chupa ya pombe ya smirnoff pamoja na kiasi kadhaa cha pesa. Cash. Pesa ambayo ilibaki baada ya kufanya matanuzi ya hapa na pale kwenye sehemu ya starehe.
Japo alikunywa pombe na mpaka zingine kuishia kuzibeba, Dan alifanikiwa kuendesha salama mpaka mbele ya geti la nyumba yake iliyopo mji mdogo wa Mweiga, mkoa wa Nyeri.
Alipofika hapo, alishuka ili afungue geti lakini kabla hajafika popote, kufumba na kufumbua, alivamiwa na wanaume wawili walotokea kichakani wakiwa wamebebelea silaha baridi.
Mmoja ana nondo na mwingine kisu.
Alipigwa na nondo ya kichwa kisha baada ya hapo mwili wake ukagombaniwa kwa nondo na visu, zamu kwa zamu, mpaka alipolala chini akiwa taabani hajiwezi.
Damu zikimtiririka kama bomba la maji.
Akiwa hapo chini, anagugumia huku akiogelea kwenye bwawa la damu yake mwenyewe, wauaji walitoweka kwenye eneo la tukio.
Haikupita muda mrefu, Daniel akafa kandokando ya geti lake.
Baada ya nusu saa tangu tukio hili litokee, ikiwa ni saa kumi na mbili ya asubuhi, bwana James Mahinda aliyekuwa nyumbani kwake, anapokea simu ya bwana mmoja anayeitwa Eddy Kariuki.
Simu hiyo haikuwa na salamu wala mambo mengi, Eddy anasema tayari tumeufuta mlima, yaani tayari washaua, na James anauliza mko wapi.
Maongezi haya mafupi yalifanyika kwenye simu ya bi. Charity Muchiri, mke wa bwana James Mahinda.
Kisha James akatoka ndani na kukwea gari, Toyota prado lenye usajili wa: KBA 583B, akaenda kukutana na wanaume wawili; Eddy Kariuki pamoja na bwana Rafael Wachira.
Wanaume walohusika na mauaji ya Dan.
Wakaenda kutupia silaha ya mauaji kwenye mto Honi (pichani), mto mkubwa unaokatiza mkoa wa Nyeri, kisha James akawapeleka wanaume hawa Kamatongu Hill, mwendo wa kilomita 4.5 toka mji wa Mweiga walipofanya mauaji, hapo akawaacha sehemu salama wakati akishughulikia kumalizia malipo ya kazi.
Baadae, siku hiyohiyo ya Ijumaa, James alipokea Ksh 160,000 ambayo ni sawa na milioni tatu na sitini na kitu za kitanzania, akawapa Eddy na Rafael jumla ya ksh 92,000 sawa na tsh milioni moja na laki tisa, nyingine akabaki nazo yeye mwenyewe.
Yani wauaji wakawa wamepokonya roho ya mtu kwa milioni moja na chenji tu.
Kwani hasara nini mbele ya jobless asiye na mbele wala nyuma?
Waliachana kila mtu akarejea kwenye mambo yake ya awali.
Eddy na Rafael walirudi walipotokea, mji wa Embu, mwendo wa masaa mawili kasoro tokea mji wa Mweiga, huko Eddy akatumia pesa yake haramu kupambana na nyumba yake ya vyumba viwili (pichani) huku Rafael akifuata ile sera isemayo, 'kama pesa haitoshei kujenga basi hiyo ni ya kula'.
Alinunua pombe na subwoofer ili akiwa anakunywa basi asikilize 'raggae' kuupa mwili pole na kuurejeshea fadhila kwa kazi kubwa ilofanyika.
Kazi hii haikuchukua muda, kama vile nzi wa soko anavyouwahi mchuzi wa embe unaotiririka mkononi mwa mlaji, ndivyo habari ya mauaji ya Dan ilivyosambaa katika mji mdogo wa Mweiga.
Kwani kuna mtu asiyemjua Dan kwenye mji huu? Mfanyabiashara kijana ambaye ametoka kwenye familia yenye pesa kichele, uzao wa bilionea wa Nyeri, bwana Stephen Wangondu?
Hakuna!
Kila mtu alizungumza na kila aliyepita karibu na makazi yake alinyooshea kidole geti la nyumba ya Dan, pale polisi walipookota mwili wa bwana huyo ukiwa umelala mfu.
Zilipopita siku tano, tarehe 6 January, Daniel akazikwa huko kijiji cha Wendiga, kaunti ya Nyeri.
Kwenye msiba huo, bwana James Mahinda na mkewe, Charity Muchiri, walihudhuria wakiketi pembeni ya familia, wakilia na kuomboleza pamoja nao.
Baada ya hapa ndiyo bilionea Stephen Wangondu anasikika mbele ya hadhara akisema yuko radhi kutumia gharama yoyote ile kuitafuta haki ya mwanae.
Na nani atambishia? Mtu anayemiliki biashara ya kusafirisha mazao nje ya nchi, ana vituo vya mafuta, mabwawa ya samaki, mashamba ya chai na ndizi, apartments na migodi? Unaanzia wapi?
Kweli, siku ya Jumamosi ya tarehe 20 February, polisi wakamtia nguvuni bwana James Mahinda akiwa huko Githurai, kaunti ya Kiambu alipokuwa amekimbilia kujificha baada ya vuguvugu la upelelezi wa polisi kupamba moto.
Lakini katika namna ya ajabu, baada ya siku nne tu za James kuwa mahabusu, naye bwana Stephen Wangondu, baba wa marehemu, akatiwa nguvuni na polisi akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Daniel!
Hapa kila mtu akashtuka. Baba amuue mtoto wa damu yake mwenyewe?
Maswali yakatiririka watu wakitaka kujua,
Ni nani hasa kahusika wa mauaji ya Dan? Sababu ya mauaji yake ni nini? Alikamatwaje? Na upi ni ukweli wa mambo katika sakata hili?
Mtandaoni ikaibuka hashtag #justicefordan watu wakishinikiza haki itendeke kwa kijana huyo ambaye ndoto zake zilikatizwa ghafla na wadhalimu wasio na huruma.
Lakini sasa ukweli wa mambo ni upi?
Tafarani hii ilianzia miaka michache hapo nyuma.
Daniel akiwa miongoni mwa watoto wengi walozaliwa na wake watatu wa bwana Wangondu, alifanikiwa kupata elimu na malezi mazuri katika nyumba kubwa ya baba yao.
Bwana Wangondu, kama ilivyo kwenye mali zake zingine, alikuwa na kawaida ya kuwakatia bima ya maisha watoto wake. Na kwa wale wa kiume ambao kwa jumla walikuwa wanne, basi alipenda kuwavesha suti wafanane na yeye.
Lakini tofauti na watoto wengine, Dan alipenda sana biashara kama baba yake na swala hili lilimpendeza sana bwana Wangondu kwani aliona amepata msimamizi na mrithi wa biashara zake nyingi.
Kwenye shughuli hiyo ya usimamizi, Dan ndo' alipata kufahamiana vema na bwana James Mahinda (pichani), bwana anayefanya kazi na baba yake kama dereva na pia kama msimamizi wa shughuli za tajiri.
Bwana huyu alikuwa ni mtu wa karibu sana na Wangondu, na kitendo cha Dan kusogezwa karibu na biashara ya baba yake kulipelekea waingie kwenye migogoro ya hapa na pale ila migogoro hii haikuwa na madhara yoyote kati yao.
Mambo yalikuwa hivi mpaka pale Dan alipokuja kumpata mwanamke aliyempenda, akamtambulisha kwao na wakafunga ndoa. Mwanamke huyu aliitwa Frida Njeri. Mwanamke mrembo haswa.
Baada ya muda mfupi, ndoa ilijibu wakapata mabinti wawili. Mzee Wangondu alifurahi sana kuwa babu, akatoa ekari ishirini za ardhi kama zawadi kwa mwanae.
Dan alijenga nyumba eneo hilo, akaishi na familia. Lakini wasidumu sana kwenye ndoa, matatizo yakaanza rasmi.
Kila siku ilikuwa ni ugomvi ndani. Frida amebadilika. Ikafikia pahala, Dan na Frida wakatengana, kila mtu akiishi kivyake.
Kama ujuavyo hapa duniani, utanyimwa chakula ila si maneno, Dan akaja kupata taarifa kuwa Frida sasa anaishi na baba yake kama mke ndani ya nyumba moja na huku biashara ashafunguliwa.
Swala hili likampelekea Dan kujiingiza kwenye ulevi ulokithiri, akinywa walau ajipoze nafsi kwa msongo wa mawazo.
Lakini kuna siku uvumilivu ukamshinda. Akaona hapana, inabidi afanye kitu.
Siku ya tarehe 1 December 2020, alionana na baba yake katika moja ya kituo cha mafuta anachokimiliki hapa Nyeri.
Alipofika hapo, pasipo kujali kuna watu, alimvamia baba yake kwa maneno makali akimshutumu kutembea na mkewe, bi. Frida.
Japo baba alijaribu kumtuliza ili waongee kistaarabu, tena faragha, Dan hakutaka kuelewa kitu. Alimtandika baba yake kofi zito lililompeleka chini pasi na huruma kisha akaondoka zake eneo hili.
Hapa ndo' mzee Wangondu akachukua simu yake na kumpigia moja kwa moja bwana James Mahinda.
Alichosema ni,
"I have 160,000 ksh. Find a team, I want that boy dead!"
Alitaka kumwadabisha Dan, na hakuwa na masikhara kwenye hilo. Alimuahidi James kiwanja kikubwa sana kama akifanikisha hii kazi.
Alimtumia ksh 20,000 kwaajili ya kutengenezea mazingira ya oparesheni kisha akamwambia amjulishe kila kitakachoendelea.
Sasa bwana James akajikuta amepata fursa adhimu ya kumwondoa Dan katika shughuli zake kwani alikuwa ni kikwazo kikubwa mbele yake na biashara za Wangondu.
Jumanne ya tarehe 29 December 2020, James Mahinda alikutana na Geoffrey Warutumo, muuza duka la miraa, huko mji wa Embu, akamwambia amtafutie wanaume wawili ambao watamfanyia kazi.
Akapatikana Eddy Kariuki kisha baadae Rafael Wachira.
Mabwana hawa, wakiongozana na James Mahinda, walikwea basi mpaka mji wa Mweiga. Hapo walifikia sehemu fulani walipoketi na kupata nyama choma huku wakipanga mpango wao wa mauaji.
Walipopata wasaa, walikwea bodaboda wakiongozwa na James mpaka maeneo ya karibu na nyumbani kwa Dan ili wapate picha ya eneo la tukio.
Baada ya hapo, James aliwapitisha hardware store, wakanunua gloves na nondo kwaajili ya kazi.
Siku hiyo, James aliwaachia 500 ksh kila mmoja wao kwaajili ya matumizi ya usiku mpaka pale watakapoonana kesho yake.
James alimhabarisha mzee Wangondu kila alichokifanya, mzee akampa 'go ahead'. Endelea na mpango.
Usiku wa tarehe 31 December, Eddy na Rafael, baada ya kumfuatilia Dan akiwa anastareheka klabu hii na ile, walikwea bodaboda mpaka eneo la nyumbani kwake wakajificha kwenye kichaka kumngojea arudi.
Dan, pasipo kufahamu, akiwa amelewa na amechoka kwa kuparty, akazama kwenye mtego wa wauaji waliofanya kazi yao vema.
Baada ya mauaji, mzee Wangondu alimkabidhi James pesa yote walokubaliana, 160,000 ksh, James akawapa wauaji 92,000 ksh yeye akabaki na 68,000 ksh.
Kama ilivyo kawaida, baada ya Dan kuuawa, kesi ilifunguliwa na uchunguzi ukaanza mara moja.
Kila kitu kilikuwa sawa na hakukuwa na namna yoyote ya kumnyooshea kidole mzee Wangondu wala James Mahinda kwenye mauaji haya.
Lakini kosa moja lilikuja hapa, pua za polisi zikaanza kumnusa tajiri huyu na macho yakaanza kumtazama kwa ukaribu zaidi.
Ikiwa zimepita siku chache tangu Dan afukiwe chini, mzee Wangondu alianza kutembelea ofisi ya Regional Commander na ofisi ya bima kuanza kuulizia pesa za bima ya maisha ya Dan.
Mzee huyu akiwa anaendeshwa na James Mahinda ndani ya prado yake, alitembelea ofisi hizo mara kwa mara akiwashinikiza wafanye upesi upesi kutoa ripoti ili apate pesa yake.
Haraka hii iliwafanya polisi wazame kwenye mafaili ya mzee Wangondu kupekua pekua, huko wakakutana na kesi ya mwaka 1995.
Mtoto Emmanuel Wangondu, umri wa miaka 18, alikufa kifo cha kutatanisha katika shamba la baba yake mzee Stephen Wangondu kwa kinachosemekana aliangukia kwenye bwawa la samaki akashindwa kujiokoa.
Kama kawaida, mzee huyo alienda kudai pesa yake ya bima haraka iwezekanavyo akisema kifo kile kilikuwa ni ajali. Bima wakamlipa pesa kubwa, maisha yakaendelea.
Kosa la pili, wakati uchunguzi wa kifo cha Dan ukiwa unaendelea kufanyika, James Mahinda alitoroka kaunti ya Nyeri akakimbilia kaunti ya Kiambu, mji wa Githurai.
James alitoroka baada ya kushukiwa kufanana kwa mawasiliano yake ya simu na safari yake ya gari, Toyota prado, sawa sawa na muda wa tukio la mauaji.
Kutoroka huku, kuliwasha taa nyekundu kwa polisi. Walimfuatilia na kumtia nguvuni.
Baada ya kubanwa mazaga, aliwaelekeza polisi mji wa Embu walipoenda kushikwa wenzake watatu; Geoffrey Warutumo (mtoa connection) na wauaji wawili; Eddy na Rafael.
Baada ya kushikiliwa kwa siku nne na kufanyiwa mahojiano, polisi walifika nyumbani kwa mzee Wangondu wakamshikilia kwa tuhuma za kupanga na kudhamini mauaji ya mtoto wake, Daniel.
Washukiwa walifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yao. Kesi ikarindima kwa miezi miwili kabla ya Stephen Wangondu kuja kuachiwa kwa dhamana tarehe 7 May 2021 baada ya kulipia milioni moja ya Kenya.
Kesho yake tu, mzee Wangondu aliaga dunia katika hospitali ya Outspan kwa matatizo ya upumuaji. Na huo ndo' ukawa mwisho wake.