Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua

hapo unabidi uwe na miradi miwili wa nyoka na panya. ila urafiki kati ya mtu na nyoka ni kitu kisicho wezekana hio ni natural
 
Fuga tu maana wewe ni mwanaume, mwanamke ndiye haruhusiwi.
Watu wote nimaadui wa nyoka. Hakuna cha mchina wala nani yoyote akikutana na nyoka lazima awe makini ndo maana wale wakisha wakamata wana watoa sumu kwanza ndo wawafuge. Hakunaga uswahiba wa nyoka na binadam
 
Huwezi kuwafuga kiholela kama vile kuku wa kienyeji ndio maana ukaambiwa snake farm sehemu special ,sasa vipi hao watoto ,mke wataingia bila ya kuruhusiwa.

Ukiwa na vifaa ,mafunzo huwezi kudhuriwa uhakika kabisa na unakuwa na sindano yako ya anti venom inacase ikitokea la kutokea
bei yake ni 250,000
 
mkuu nimekua nikipata mafunzo mbali mbali juu yA hii mifugo at the end of this year nitakua mekamilisha taratibu zote na mifugo itakua mabandani
Kama ni kweli hongera mkuu
Nakutakia kila la kheri

Siku zote risk takers ndio wanaofanikiwa

Ufugaji wa nyoka upo poa sana haswa ukiwajua
 
Unavuna vipi hiyo sumu?
Tupe shule I like innovative young one like you




Hatua ya kwanza unamkamata nyoka kwa kutumia vifaa special ,kuna fimbo aina 2 inabidi uwe ayo moja inakibanio ambayo inakusaidia kumbana shingoni karibu na kichwa ,ukishamdhibiti shingoni Basi unamkatama kiurahisi nyuma ya kichwa.









Ukishamkamata huyo nyoka unachukua chombo chako ambacho umekitayarisha kwaajili ya kuweka sumu hiyo ,kuna namna mbali mbali ya kutoa sumu

1.chombo chako kwa juu unafunga plastic inayotoboka kiurahisi ,kisha unamuinamisha nyoka ili fangs zake zigonge plastic hiyo na hatimaye sumu huingia ndani ya chombo

2.chombo cha wazi pia unamuinamisha nyoka agonge kuta za chombo na kuachia sumu

Namna zipo nyingi
 
Nilichogundua wabongo wengi hatuzunguki kujifunza mambo..
kwa mtu wa arusha ii kilimo ya nyoka hawez kushangaa maana snake farm zipo za kutosha na watu wanafika kujifunza. ila naona kuna raia umu wanaona ii ni kama fursa ya kisenge na watu wameamua kuifanya kwa sababu magufuli kabana, umepotoka kama unafikiri ivo. watu wana piga pesa za venom toka kpnd cha mkapa. na pia bado wanapokea pesa za watalii wanaotembelea
 
Tatizo wanachukulia poa

Laiti wangefahamu gram ya venom ilivyokuwa na thamani wasingeongea ukiachilia utalii


Gram ya boomslang ni $4800
Gram ya cobra $800
Gram ya koboko $550
Nk nk nk


Tatizo wabongo tuna mzaha sana kila kitu wanadhani ni nadharia tu,

Watu wanadhani kufuga nyoka ni risk sana na nyoka hawafugiki lakini hawashangai zoo zilizopo.

Ukipatiwa elimu na mafunzo kila kitu kipo easy na Arusha snakefarms kweli zipo nyingi kama ile ya meserani snake park
 
[emoji37] [emoji37]
 
baadae wakiona mtu anamiliki ndege wanasema freemason, so stupid.
 
Kwani ni kilimo cha nyoka au ufugaji wa nyoka mbna naona kama vitu viwili tofauti
 
aisee hii fursa inipite tu jamani!! naogopa nyoka sana.Bora nifuge sungura
 
Mimi nipo tayari kulima nyoka lakini hahitaji kufika shambani kwako kujifunza. Nataka kujua namna ya kuwapata, mtaji, ulishaji, matumizi mbali ya kupata dawa ya sumu yao na mengineyo.
 
kwa aina hii ya maisha hadi 2025 tutakuwa tumeletewa kila aina ya Kilmo humu mmetoka kuhamasisha kufuga nge na siafu sasa mmekuja kwa nyoka
 
Hata bajeti ya mboga itapungua, ukijisikia kula nyama unaingia bandani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…