Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wote nimaadui wa nyoka. Hakuna cha mchina wala nani yoyote akikutana na nyoka lazima awe makini ndo maana wale wakisha wakamata wana watoa sumu kwanza ndo wawafuge. Hakunaga uswahiba wa nyoka na binadamFuga tu maana wewe ni mwanaume, mwanamke ndiye haruhusiwi.
Huwezi kuwafuga kiholela kama vile kuku wa kienyeji ndio maana ukaambiwa snake farm sehemu special ,sasa vipi hao watoto ,mke wataingia bila ya kuruhusiwa.Mkuu mbona hujatutajia pia HASARA ya kufuga nyoka? Hasara kubwa ya kufuga nyoka ni kwamba nyoka mwenye sumu anaweza kukugonga wewe mmiliki, shamba boy wa shamba lako nyoka au mtu yeyote atakayekutana naye (mtoto wako, mama yako, mke/mume wako, nk) na kupoteza maisha ndani ya dakika 5 tu hata kabla hujapatiwa huduma ya kwanza au kufikishwa hospitalini. Kwa hiyo, nyoka ni kiumbe hatari sana...ukimuona popote muue na kumtupia mbali kabisa.
Kama ni kweli hongera mkuumkuu nimekua nikipata mafunzo mbali mbali juu yA hii mifugo at the end of this year nitakua mekamilisha taratibu zote na mifugo itakua mabandani
Unavuna vipi hiyo sumu?
Tupe shule I like innovative young one like you
Tatizo wanachukulia poaNilichogundua wabongo wengi hatuzunguki kujifunza mambo..
kwa mtu wa arusha ii kilimo ya nyoka hawez kushangaa maana snake farm zipo za kutosha na watu wanafika kujifunza. ila naona kuna raia umu wanaona ii ni kama fursa ya kisenge na watu wameamua kuifanya kwa sababu magufuli kabana, umepotoka kama unafikiri ivo. watu wana piga pesa za venom toka kpnd cha mkapa. na pia bado wanapokea pesa za watalii wanaotembelea
View attachment 502154
Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo yenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya "snake venom" ipo juu sana.Sumu ya nyoka inatumika kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi hivyo thamani ya "snake venom " ipo juu sana kutokana na uhitaji wake.
View attachment 502152
Gram moja ya "snake venom " kwa soko la kimataifa inauzwa $1880 ,na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25,000
*Kama unafikiria kuanzisha shamba lako la nyoka ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata faida ya kutosha kutokana na venom wanayozalisha Nyoka
1.zingatia hali ya joto na hewa .
View attachment 502150
Nyoka wanahitaji joto ya kiwango cha 24-29 degrees Celsius nyakati ya siku na 21-24 nyakati za usiku,
2.mabanda na nyumba za nyoka zinahitaji kusafishwa mara kwa Mara
Hali hiyo itasaidia kukuza uzalishaji wa nyoka kwa wingi.Nyoka wanahitaji kuwekwa mahali salama kuzuia matatizo yeyote ile ya kiafya kuwapata.
3.Nyoka kwa kawaida hula panya 3-4 na hulishwa kwa wiki 3-4 .Nyoka hula panya walio hai lakini wanaweza kula waliokufa pia ,Nyoka hupenda kucheza na panya mwanzo kabla ya kuwala hivyo ni vema kuwapatia walio hai.
Faida 3 za ufugaji wa nyoka
1.uzalishaji wa venom ambayo ukiuza unapata kiasi kikubwa cha pesa.
2.hupunguza na kutokomeza wadudu waharibifu kama panya nk.Nyoka chakula chao kikuu ni panya hivyo husaidia kutusafishia shamba au nyumba kwa kuwamaliza wadudu hawa.
Dawa ya kuua sumu ya nyoka itengenezwayo kutoka kwa sumu ya nyoka, yaani anti-venom, ndiyo tiba bora pekee ya kuumwa na nyoka.
View attachment 502151
**Mwisho nawashauri ndugu zangu sio kila tukiwaona nyoka tunawaua ,nyoka ni rafiki zetu na sio maadui.Tuwatumie ipasavyo watatusaidia sana.
baadae wakiona mtu anamiliki ndege wanasema freemason, so stupid.Tatizo wanachukulia poa
Laiti wangefahamu gram ya venom ilivyokuwa na thamani wasingeongea ukiachilia utalii
Gram ya boomslang ni $4800
Gram ya cobra $800
Gram ya koboko $550
Nk nk nk
Tatizo wabongo tuna mzaha sana kila kitu wanadhani ni nadharia tu,
Watu wanadhani kufuga nyoka ni risk sana na nyoka hawafugiki lakini hawashangai zoo zilizopo.
Ukipatiwa elimu na mafunzo kila kitu kipo easy na Arusha snakefarms kweli zipo nyingi kama ile ya meserani snake park
Hivi nyoka sio nyara za serikali???