HOJA Takriban mwaka moja tangu treni ya SGR ipate ajali Ruvu, ila hakuna taarifa rasmi ya chanzo, harasa wala hatua zilizochukuliwa

HOJA Takriban mwaka moja tangu treni ya SGR ipate ajali Ruvu, ila hakuna taarifa rasmi ya chanzo, harasa wala hatua zilizochukuliwa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Oktoba 23, 2025, treni ya SGR ya mchongoko (EMU) iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ilipata ajali katika eneo la Ruvu. Jambo la kufurahisha ni kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha, ingawa ajali hiyo ilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu, ikiwemo reli na njia za umeme. Pia, kituo cha Ruvu kimeendelea kutopandisha wala kushusha abiria tangu wakati huo.

Muda mfupi baada ya ajali hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa, akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani wakati huo, Abubakari Kunenge, alieleza mbele ya vyombo vya habari kuwa ajali hiyo ilisababishwa na hitilafu za kiuendeshaji. Kauli hiyo ilitolewa pia kupitia taarifa kwa umma.

Hata hivyo, hadi sasa, TRC haijaweka wazi chanzo halisi cha ajali hiyo, nani alihusika na hitilafu hizo za kiuendeshaji, wala hatua zilizochukuliwa baada ya tukio hilo.

Kwa kuwa ajali hiyo ilisababisha uharibifu wa miundombinu na treni yenyewe, ni wazi kuwa Serikali imepata hasara inayohitaji uwajibikaji na maelezo ya kina.

Kwa kuwa mradi wa SGR ni mali ya umma, wananchi wana haki ya kupata taarifa kuhusu chanzo cha ajali hiyo, hatua zilizochukuliwa na juhudi zilizofanyika kurejesha huduma katika kituo cha Ruvu.

Kwa nini TRC haijatoa ufafanuzi wa kina kuhusu suala hili hadi sasa, na ni lini wananchi watapata majibu?
 
Takribani mwaka mmoja sasa toka treni ya mchongoko ipate ajali eneo la Ruvu, mpaka leo wananchi hatujawahi kusikia TRC wakitolea taarifa rasmi juu ya chanzo cha ajali hiyo, ni hasara gani Serikali imepata kufuatia ajali ile. Uwekezaji wa SGR ni kodi za wananchi, TRC watuambie nini kilisababisha na hatua zilizochukuliwa
 

Attachments

  • 20260926_112552.jpg
    20260926_112552.jpg
    958.2 KB · Views: 6
Back
Top Bottom