TAKUKURU, Bila Kuchunguza hii Rushwa ya Bunge, bora ivunjwe

TAKUKURU, Bila Kuchunguza hii Rushwa ya Bunge, bora ivunjwe

Kumekuwa na tuhuma nyingi kuwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa ni Toothless bull dog na kwamba taifa linapoteza fedha nyingi kuiendesha wakati haina tija yeyote. Na haya yamesemwa mpaka na wabunge wenyewe.

Kuna tuhuma ambazo zimekuja kama swali bungeni leo kuhusu wabunge wa CCM kupewa rushwa ya milioni 10 katika kikao alichohudhuria PM na Kinana ili mswada wa habari na mpango wa maendeleo upite.

Ni tuhuma mbaya na chafu sana kupata kutokea tokea Uhuru kwa serikali kwa ujumla wake kutoa hongo kwa kundi moja la wabunge walio wengi.
Haijalishi kama ni milioni 10 au 5, zote ni rushwa na ninauhakika wapo wabunge wamepokea lakini nafsini mwao hawajapendezwa na jambo hilo na hapo ndio pakuanzia.

Kufuta aibu hii ya kitaifa TAKUKURU watangaze kufuatilia jambo hili na kuchukua hatua hata kama itabidi serikali yote iathirike.
Nchi zingine hata rais au mfalme kwenye rushwa anachunguzwa iweje hapa waogopwe?

Na kama Rais atazuia uchunguzi huo basi ni kuwa rushwa hiyo ina baraka zake, na jee kumbe naye pamoja na kauli zake zote ni mtoa rushwa?
TAKUKURU ikishindwa ivunjwe haina maana kuwepo
Takukuru wachunguze tuhuma za mbowe?
Labda kama hawana kazi ya kufanya! Yaani mbunge ahongwe m zote ili mswada upite ili serikali ipate faida nini?
Huyu Mbowe kawaroga au? Hata akili ndogo ya kufikiri na ukatambua huu uongo hakuna?
Chadema mmekuwaje? Mlikuwa vizuri sana, lkn sasa hivi mnaumwa ugonjwa usiokulikana!
 
  • Thanks
Reactions: nao
Hivi zile tuhuma za Mbowe kupokea Bilioni 10 kutoka kwa Lowasa ili aruhusiwe kugombea Urais uchunguzi ulishafanyika?
Leo tunajadili naibu spika kumkingia kifua waziri mkuu kuhusu kugawa mlungura bungeni!
anzisha uzi wako kuhusu hizo tuhuma
 
Mkurugenzi wa TAKUKUR anateuliwa na kuwajibika kwa nani?

Nachoka kabisa na sheria zinazounda Taasisi nyeti kama hizi katika nchi yetu.
Wote Watakaochangia Hii Thread Wazingatia Hili Jambo Lililisemwa Na Mdau.

Ikumbukwe Michango Yote Imemezwa Na Hayo Maneno Machache
 
Takukuru wachunguze tuhuma za mbowe?
Labda kama hawana kazi ya kufanya! Yaani mbunge ahongwe m zote ili mswada upite ili serikali ipate faida nini?
Huyu Mbowe kawaroga au? Hata akili ndogo ya kufikiri na ukatambua huu uongo hakuna?
Chadema mmekuwaje? Mlikuwa vizuri sana, lkn sasa hivi mnaumwa ugonjwa usiokulikana!
Ulitaka wachunguze tuhuma za Olesendeka kwa zitto?
tulia dawa iingie vizuri
 
Nashauri uchunguzi huu uende sambamba na uchunguzi wa tuhuma za Mwenyekiti mmoja kupokea bn 12 pamoja na wajumbe wengine kupokea si chini ya mil 200 kila mmoja sometime around July-August 2015
tuliza mdomo povu likuishe
 
Achana propaganda na siasa za kibunge hizo
Wewe kweli kwa akili ya kawaida tu
Kweli unaweza amini kuwa serikali
Inaweza kuhonga mil 10 kila mbunge
Kwa kupitisha muswada wa habari?
Kweli tanzania tunavichaaa..nenda kapime
 
Mkuu Chakaza hii ni taasisi ya kukuza na kusambaza rushwa nchini haiwezi kufanya chochote, yenyewe inanuka rushwa.
Mkuu umeona wanavyochangia hapa? Kwao ni jambo lisilo na maana na ndio sababu hata Naibu spika badala ya kushika mdomo na kushangaa anazuia swali lisijibiwe.
Yeye kama kiongozi wa mhimili wa bunge alipaswa kuacha PM ajibu kuwa ni kweli au sio kweli na majibu hayo yaingie kwenye rekodi za bunge.
Walichofanya sasa hivi ni kuwa wamemnyima mamlaka Rais kuzungumzia rushwa tena hadharani kwani tuhuma kuwa serikali inahonga wabunge inamhusisha naye kama mtoa rushwa kinara.
Mbowe kakitaja kikao hicho, saa ya kukutana na waliokuwepo. Sasa kazi kwao kujisafisha au kuacha tuelewe kuwa serikali inatoa rushwa na wabunge wa Ccm ni wala rushwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yaani tayari mmesahau mengine yooote mmerukia suala la "rushwa". Ha ha ha. Ndio maana Mkapa alisema nyie ni malofa na....
 
  • Thanks
Reactions: nao
Yaani tuhuma za mbowe ndo zifanye hili lisichunguzwe hivi nyie CCM mna funza vichwani au

Kama mbowe alizingua achunguzwe na awajibishwe vivyo hvyo kwa sakata hili hatuwezi kuwa na nchi inayoegemea upande mmoja tu

Tatzo kubwa ni mfumo hapa mtatuelewa yaan mkurugenzi wa TAKUKURU ni mteule wa rais na anawajibika ataweza kumchikulia hatua kweli

Nchii bhana dah
 
Hivi zile tuhuma za Mbowe kupokea Bilioni 10 kutoka kwa Lowasa ili aruhusiwe kugombea Urais uchunguzi ulishafanyika?
Ski mlisema aliuza? Na kuwa Chadema ni Mali yake, sasa Takukuru wanachunguza je rushwa hapo?
Hii ya sasa ni aibu ya wazi, serikali ina honga chama tawala kinahongwa.
 
Si lazima Bashe naye apewe lakini yawezekana kabisa walio wengi wamepewa
Exactly, lengo lao ni kupata kura za kutosha ikibidi.
Hata hizo milioni 10 alizosema Mbowe yaweza zisiwe hizo ikawa 7 au 5 au 3.
Lakini bado ni rushwa, na Naibu spika lazima analijua hilo ndio maana kapanic alikuwa anajua PM akijibu basi kitawaka
 
Hivi kufikia mbunge anahongwa milioni kumi TAKUKURU kazi yao nini hasa?

Hivi siku hizi hakina usalama wa taifa bungeni kama ilivyo kuwa kwa Nyerere?

Hivi mpaka sasa TAKUKURU na police hawajajua kwamba wabunge wamehongwa kwa maagizo ili wasipitishe muswada mbovu wa habari.?

Hii ingelikuwa kwa wenzetu tayari watu wangekuwa wameshajiuzulu kabisa.

Tunaambiwa nchi haina pesa na wanabana matumizi lakini za kuhonga Wabunge na Lipumba zinapatikana .

Mimi nitakuwa wa mwisho kuamini hii serikali ni ya wanyonge..
 
Back
Top Bottom