TAKUKURU, Bila Kuchunguza hii Rushwa ya Bunge, bora ivunjwe

TAKUKURU, Bila Kuchunguza hii Rushwa ya Bunge, bora ivunjwe

Kama hili limefanyi
Kumekuwa na tuhuma nyingi kuwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa ni Toothless bull dog na kwamba taifa linapoteza fedha nyingi kuiendesha wakati haina tija yeyote. Na haya yamesemwa mpaka na wabunge wenyewe.

Kuna tuhuma ambazo zimekuja kama swali bungeni leo kuhusu wabunge wa CCM kupewa rushwa ya milioni 10 katika kikao alichohudhuria PM na Kinana ili mswada wa habari na mpango wa maendeleo upite.

Ni tuhuma mbaya na chafu sana kupata kutokea tokea Uhuru kwa serikali kwa ujumla wake kutoa hongo kwa kundi moja la wabunge walio wengi.
Haijalishi kama ni milioni 10 au 5, zote ni rushwa na ninauhakika wapo wabunge wamepokea lakini nafsini mwao hawajapendezwa na jambo hilo na hapo ndio pakuanzia.

Kufuta aibu hii ya kitaifa TAKUKURU watangaze kufuatilia jambo hili na kuchukua hatua hata kama itabidi serikali yote iathirike.
Nchi zingine hata rais au mfalme kwenye rushwa anachunguzwa iweje hapa waogopwe?

Na kama Rais atazuia uchunguzi huo basi ni kuwa rushwa hiyo ina baraka zake, na jee kumbe naye pamoja na kauli zake zote ni mtoa rushwa?
TAKUKURU ikishindwa ivunjwe haina maana kuwepo

Kama hili limefanyika basi ndiyo mambo tunayojifunza kutoka kwa baadhi ya majirani zetu wenye uzoefu wa kunyamazisha wabunge!
 
Utendaji kazi wa vyombo primitive ndio unaohitaji ushahidi kwa anayetoa tuhuma. Ushahidi unatafutwa na vyombo competent vya kukusanya ushahidi kwa wenzetu. Wao wenzetu unapeleka tuhuma wao wanafanyia kazi tuhuma kwa utaalam advanced.
Sio kweli tuhuma bila ushahidi zinaitwa umbeya.hakuna taasisi yoyote ya upelelezi duniani yaweza fanyia kazi umbeya .Hata vyombo vya habari makini huwa haviandiki wala kutangaza umbeya popote duniani
 
Mbowe anatafuta "kiki" tu, hana lolote kaishiwa kisiasa huyo.
 
We ndio nani wa kuamuru bunge livunjwe kwa story za vijiweni za Mbowe! Ebo!
Hivi huwa mnatumia akili au matope? Kusoma kitu uelewe husomi unakimbilia kujibu kama mwendo wa gari bovu.
Nani kasema Bunge livunjwe?
 
Rushwa ndio imeota mizizi na inastawi sana

Naam rushwa imetamalaki nchi hii. Wengi wa wanaotoa mapovu katika jukwaa hili ni mamaluki wanaoishi kwa umamluki unaolelewa na rushwa ya kitaasisi.
 
[QUOTE="Lizaboni, post: 18331522, member: 138049"ivi zile tuhuma za Mbowe kupokea Bilioni 10 kutoka kwa Lowasa ili aruhusiwe kugombea Urais uchunguzi ulishafanyika?[/QUOTE]

Kazi ya kufanya au kuwafanyia uchunguzi
mbowe na lowasa ni ya nani????
Mbowe kuchukua rushwa ya lowasa does it justify wabunge Wa ccm nao wakubali kuhongwa?
 
Hivi zile tuhuma za Mbowe kupokea Bilioni 10 kutoka kwa Lowasa ili aruhusiwe kugombea Urais uchunguzi ulishafanyika?
Unamuuliza nani sasa ?
Unataka JF ndio ifanye uchunguzi ?
 
Kwa Tanzania tunayofahamu, ambayo wananchi hawajuai hata ni namna gani wanaweza kuishinikiza serikali, ambayo wabunge ni washangiliaji tu bungeni, tunatona mengi, na niwahakikishieni.....HILI NALO LITAPITA
 
Kumekuwa na tuhuma nyingi kuwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa ni Toothless bull dog na kwamba taifa linapoteza fedha nyingi kuiendesha wakati haina tija yeyote. Na haya yamesemwa mpaka na wabunge wenyewe.

Kuna tuhuma ambazo zimekuja kama swali bungeni leo kuhusu wabunge wa CCM kupewa rushwa ya milioni 10 katika kikao alichohudhuria PM na Kinana ili mswada wa habari na mpango wa maendeleo upite.

Ni tuhuma mbaya na chafu sana kupata kutokea tokea Uhuru kwa serikali kwa ujumla wake kutoa hongo kwa kundi moja la wabunge walio wengi.
Haijalishi kama ni milioni 10 au 5, zote ni rushwa na ninauhakika wapo wabunge wamepokea lakini nafsini mwao hawajapendezwa na jambo hilo na hapo ndio pakuanzia.

Kufuta aibu hii ya kitaifa TAKUKURU watangaze kufuatilia jambo hili na kuchukua hatua hata kama itabidi serikali yote iathirike.
Nchi zingine hata rais au mfalme kwenye rushwa anachunguzwa iweje hapa waogopwe?

Na kama Rais atazuia uchunguzi huo basi ni kuwa rushwa hiyo ina baraka zake, na jee kumbe naye pamoja na kauli zake zote ni mtoa rushwa?
TAKUKURU ikishindwa ivunjwe haina maana kuwepo

Mtu aliyeenda kugawa milioni 10 Je alikuwa na magunia mangapi ya hela. Kitu nyingine haiingii kichwani. Kwa Hali hii hizo pesa wametoa wapi. Huu ni uongo WA wazi wazi...!
 
Sio kweli tuhuma bila ushahidi zinaitwa umbeya.hakuna taasisi yoyote ya upelelezi duniani yaweza fanyia kazi umbeya .Hata vyombo vya habari makini huwa haviandiki wala kutangaza umbeya popote duniani
Wewe umejiridhisha?
 
Mtu aliyeenda kugawa milioni 10 Je alikuwa na magunia mangapi ya hela. Kitu nyingine haiingii kichwani. Kwa Hali hii hizo pesa wametoa wapi. Huu ni uongo WA wazi wazi...!
Uko dunia ya kale kweli wewe!
 
m mwenyewe nataman takukuru wafuatilie na adhabu itolewe kwa wahusika....na ikibainika mh mbowe kalidanganya bunge na watz achukuliwe hatua pia
 
Si lazima Bashe naye apewe lakini yawezekana kabisa walio wengi wamepewa
Mkuu kama hizi ni tetesi kwanini takukuru wachunguze wakati kuna tetesi ya Edo kununua ugombea kwa 12b si wangeanza na hii?
 
Achana propaganda na siasa za kibunge hizo
Wewe kweli kwa akili ya kawaida tu
Kweli unaweza amini kuwa serikali
Inaweza kuhonga mil 10 kila mbunge
Kwa kupitisha muswada wa habari?
Mimi si mshabiki wa chama chochote cha siasa ila kama kweli kabisa imetokea!kwa kweli itakuwa watoaji kama wapo?watakuwa hawana nia njema na wa TZ walio maskini kabisa pia sitashangaa sana hilo kutokea!wa TZ wenzangu hivi bado muna kumbuka suala la JAIRO?kutuhumiwa kuwahonga wabunge ili budget ya wizara ya nishati na madini budget yake ipite?tena si kwa pesa zake mfukoni bali pesa za sisi walipa kodi maskini wa nchi hii! naamini aliondolewa kwenye cheo chake kwa kashfa hiyo kwani mpaka leo hamna denial yoyote iliyo tolewa kwamba sio kweli SOURCE:VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI NCHINI VILIVYO RIPOTI HIYO HABARI
 
Sio kweli tuhuma bila ushahidi zinaitwa umbeya.hakuna taasisi yoyote ya upelelezi duniani yaweza fanyia kazi umbeya .Hata vyombo vya habari makini huwa haviandiki wala kutangaza umbeya popote duniani
Where have you been apart from TZ. Ulaya, marekani na nchi zingine hata nikipiga simu nikiwaambia kuna 1,2,3 wanakuja mbio za ajabu, hawakuambii tupe ushahidi kwa sababu wao wapo trained kutafuta ushahidi na wana nyenzo za kutafuta ushahidi.
Ndio maana nasema ni primitive governments ambazo zinamtaka mtoa tuhuma/taarifa za uhalifu atoe ushahidi. Sijakataa kuwa hilo la kumtaka mtu atoe ushahidi halifanyiki, nimesema linafanyika na primitive governments na ambazo ni ovu vilevile.
 
Mkuu huu uchunguzi wa Takukuru uliishia wapi?

Kumekuwa na tuhuma nyingi kuwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa ni Toothless bull dog na kwamba taifa linapoteza fedha nyingi kuiendesha wakati haina tija yeyote. Na haya yamesemwa mpaka na wabunge wenyewe.

Kuna tuhuma ambazo zimekuja kama swali bungeni leo kuhusu wabunge wa CCM kupewa rushwa ya milioni 10 katika kikao alichohudhuria PM na Kinana ili mswada wa habari na mpango wa maendeleo upite.

Ni tuhuma mbaya na chafu sana kupata kutokea tokea Uhuru kwa serikali kwa ujumla wake kutoa hongo kwa kundi moja la wabunge walio wengi.
Haijalishi kama ni milioni 10 au 5, zote ni rushwa na ninauhakika wapo wabunge wamepokea lakini nafsini mwao hawajapendezwa na jambo hilo na hapo ndio pakuanzia.

Kufuta aibu hii ya kitaifa TAKUKURU watangaze kufuatilia jambo hili na kuchukua hatua hata kama itabidi serikali yote iathirike.
Nchi zingine hata rais au mfalme kwenye rushwa anachunguzwa iweje hapa waogopwe?

Na kama Rais atazuia uchunguzi huo basi ni kuwa rushwa hiyo ina baraka zake, na jee kumbe naye pamoja na kauli zake zote ni mtoa rushwa?
TAKUKURU ikishindwa ivunjwe haina maana kuwepo
 
MONDAY, NOVEMBER 7, 2016
Takukuru yachunguza Sh10 milioni za wabunge CCM

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola.

Kwa ufupi
Wiki iliyopita, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe wakati akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliibua tuhuma dhidi ya wabunge hao akidai kwamba walipewa fedha hizo ili wapitishe mpango wa maendeleo ya Taifa na muswada wa Sheria za Huduma za Habari.

By Peter Elias, Mwananchi pelias@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imeanza kuchunguza tuhuma za wabunge wa CCM kupewa Sh10 milioni kila mmoja ili kupitisha Muswada wa Sheria za Huduma za Habari.

Wiki iliyopita, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe wakati akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliibua tuhuma dhidi ya wabunge hao akidai kwamba walipewa fedha hizo ili wapitishe mpango wa maendeleo ya Taifa na muswada wa Sheria za Huduma za Habari.

Hata hivyo, swali hilo halikujibiwa na Waziri Mkuu baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kumkingia kifua akidai swali hilo halikuwa la kisera.

Mbowe licha ya kusisitiza kwamba swali hilo ni la kisera kwa sababu masuala ya rushwa na maadili ya viongozi wa umma ni ya kisera, aligonga mwamba.

Suala hilo liliibuka tena kwenye mahojiano kati ya Rais John Magufuli na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, na Rais alisema vyombo vinavyohusika vinalichunguza ili kupata ukweli.

“Ninafahamu kuna kanuni za Bunge na nina uhakika vyombo vya PCCB (Takukuru) vitauliza kupata ushahidi. Tuna vyombo vyetu vinavyoshughulikia rushwa, bahati nzuri sheria sasa imeshapitishwa, sheria namba 3 ya mwaka 2016, watakwenda kuthibitisha huko,” alisema Rais Magufuli wakati akijibu swali la Henry Mhanika ambaye ni Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (Moat).

Akizungumzia suala hilo jana, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola alisema wameanza kufanya uchunguzi juu ya suala hilo kwa sababu ni jukumu lao na watalifanya kiuhakika.

Alisema: “Kama Rais amesema tunachunguza suala hilo, mnataka mimi niseme nini? Ndiyo, tumeanza kuchunguza, Takukuru ni chombo chake na tumeanza kazi hiyo. Kama na wewe una ushahidi tuletee tuufanyie kazi.”

Alipoulizwa kama analifanyia kazi suala hilo, Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Kaganda alisema: “Takukuru ndiyo wenye kazi hiyo kwa sasa, watafute uwaulize.”

Hata hivyo, muswada wa habari ulipitishwa na Bunge Jumamosi iliyopita licha ya kupingwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya habari na wabunge wa upinzani.

Wachambuzi mbalimbali wamezungumzia tuhuma hizo kwamba zimelichafua Bunge na kuhatarisha uhuru wa chombo hicho, ambacho kina dhamana kubwa ya kutunga sheria zinazoongoza Taifa hili.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Faraja Kristomus alisema tuhuma hizo ni nzito kwa chombo cha kutunga sheria na kwamba siyo mara ya kwanza kutolewa kwa tuhuma za rushwa kwa wabunge.

Alisema tuhuma hizo zinaibua maswali mengi ikiwamo hamu ya wananchi kutaka kujua kama kweli wabunge walipokea Sh10 milioni, na kama ndiyo jumla ya fedha zilizotolewa ni kiasi gani na fedha hizo ni za nani kati ya CCM au Serikali.

“Inabidi Bunge lichunguze na kutoa majibu kuhusu suala hili, nashindwa kusema moja kwa moja kwamba muswada huo umepita kwa sababu ya rushwa hiyo, lakini safari hii wabunge wa CCM wameonekana kuungana sana ukilinganisha na mabunge yaliyotangulia,”
alisema.

Alisisitiza kwamba uongozi wa Bunge usilifumbie macho suala hilo hata kama liliulizwa nje ya kanuni kwa sababu linatoa picha kwamba wabunge wote ni wala rushwa na hilo litafanya sheria hiyo isipokelewe na wananchi kama sheria halali.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema Takukuru inatakiwa kuzifanyia kazi tuhuma hizo kwa sababu ni rushwa kama yalivyo matukio mengine ya rushwa.

Alisema endapo itabainika kwamba tuhuma hizo ni za kweli, wananchi watakosa imani na Bunge lao kwa sababu litakuwa limeshindwa kutumia uhuru wake katika kufanya maamuzi yenye manufaa kwa Taifa.

“Tusubiri tu taarifa ya vyombo vinavyofanya uchunguzi, hapo ndiyo tutapata ukweli wote. Inawezekana pia zikawa ni siasa ndani ya Bunge, lakini uchunguzi ni muhimu kwa sababu lisemwalo lipo,” alisisitiza Profesa Mpangala.
 
Back
Top Bottom