TAKUKURU: CHADEMA badala ya kulalamika wanapaswa kusoma sheria, mwisho wa uchunguzi waweza kuwa mwanzo wa uchunguzi mwingine


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imejibu madai ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa inatumika kisiasa, baada ya kuwahoji baadhi ya wabunge wa chama hicho kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zilizokuwa zikikatwa kwenye mishahara ya wabunge pamoja na michango.

Taarifa iliyotolewa jana na Afisa Mahusiano wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Brigedia Jenerali, John Mbungo imeeleza kuwa Takukuru ni chombo kinachojitegemea na kinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Imewataka wanachama wa Chadema kuendelea kutoa ushirikiano kuhusu tuhuma hizo kwa sababu wanatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007.

“Takukuru inawashauri wanachama wa Chadema kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi unaendelea,” imeeleza taarifa hiyo.

Kapwani ameeleza kuwa wanachama wa Chadema ndio waliowasilisha malalamiko yao wakihoji matumizi ya fedha zilizokuwa zinakatwa kwenye mishahara ya wabunge wa viti maalum na wabunge wa majimbo.

“Hatua hii ni muendelezo wa uchunguzi unaofanywa na Takukuru Makao Makuu kuhusu malalamiko juu ya matumizi ya fedha za chadema, ambapo hatua ya sasa ni kuwahoji wabunge 69 wa chama hicho pamoja na wanachama wa zamani wa chama hicho,” imeongeza taarifa hiyo.

Takukuru walianza kuchukua hatua kuhusu tuhuma hizi baada ya waliokuwa wabunge wa chama hicho waliohamia vyama vingine kudai kuwa walikuwa wanakatwa mishahara yao tangu Juni 2016.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa katika malalamiko hayo ilidaiwa kuwa kila mbunge wa viti maalum wa Chadema alikuwa anakatwa Sh. 1,560,000 kwenye mshahara wake wa mwezi, na wabunge wa majimbo walikatwa Sh. 520,000 kwa kila mwezi kwenye mshahara wake.
 
Tena wakitulize kabisa maana wao ndio wanashitaki
 
Sawa hao wanachama wa Chadema wawe watulivu lakini sisi tunataka wasichelewe kuwapeleka mahakamani. Hizo ni pesa za umma na wavuja jasho ndio walizilipa kama kodi. Wapelekwe mahakamani haraka Bia yetu
 
Tilion ndio iliyosababisha watoto wako wanasoma bure wewe mlugaluga, ndio imesababisha Magufuli apeleke umeme kijiji kwenu, ndio mke wako anajifungua bure hospital
Kwa maana hiyo Magu hajui hesabu kiasi cha kushndwa kumwelewesha CAG?
 
Watulie sindano iwaingie wapone!
 
Taasisi hizi zijitafakari, TAKUKURU, TRA, UHAMIAJI, OFISI YA MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA, OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI, POLICE, BUNGE pamoja na MAHAKAMA.
 
Siijui hii ufafanuzi toka kwa wajuvi tafadhari. !Uchunguzi dhidi ya,upo na Public updates?!
 
Playing politics......
 
TAKUKURU, kama kweli mnajua kazi, chunguzeni kwanza hiyo miradi kibao inayoendelea bila kupitishwa na bunge na tenda za kawaida kama ilivyo ada!
 
Chadema hawataki kabisa kuguswa kuhusu pesa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…