TAKUKURU mchunguzeni Mkuu wa Wilaya Morogoro, anaitumia ofisi yake vibaya

SIRI IMEFICHUKA! Kumbe vile vibanda vya wajasiriamali (wamachinga) katika Soko Kuu la Chifu Kingalu vilivyojengwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando kwa kushirikiana na benki fulani, vimegeuzwa mradi wa kupigia pesa na kuiibia serikali? Hatari sana.

Itakumbukwa kuwa DC Msando alisema anakatwa kiasi fulani cha mshahara wake kila mwezi kulipia deni la benki alilokopa ili kujenga vibanda vile, tena alisema anajitolea.

REJEA: Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando anasema anakatwa rejesho la mkobo wa kujenga vibanda

Imekuwaje leo anadai alipwe na Halmashauri? Lengo lake lilikuwa ni kufanya biashara? Kuilaghai Serikali? Kusaka umaarufu wa kisiasa au kutapeli Wajasiriamali?

Tetesi zilianza kuenea kutoka kwa wajasiriamali wenyewe ambao walidai DC aliwaelekeza kulipia kati ya laki 5 mpaka laki 7 kila mwezi kwa kila kibanda, tena fedha hizo alitaka zilipwe kwenye akaunti yake binafsi. Tetesi hizo zikadaiwa ni uzushi.

Yakaibuka madai mengine kwamba baada ya kushindikana kuwalipisha machinga kiasi hicho kufuatia serikali ya mkoa kuelekeza wamachinga walipe tu bei elekezi kwa soko ili kuipatia halmashauri mapato, DC kuona amekwama akaagiza H/Manispaa imrudishie fedha zake takribani milioni 106 ili alipe deni la benki kwa sababu zilitumika kwenye mradi wa maendeleo, jambo ambalo lilipingwa pia kwa sababu sio utaratibu wa serikali mtu binafsi kukopa na kuja kudai bila kufuata sheria na kanuni. Madai hayo nayo akayakanusha kupitia vyombo vya habari na kudai Mkuu wa Mkoa na Mbunge wanakwamisha jitihada za serikali (yeye) kuwasaidia wamachinga.

REJEA: DC Alberto Msando akopa milioni106 benki ili kuwajengea wamachinga sehemu ya kufanyia biashara

Hivi sasa yapo madai mengine kwamba ameagiza alipwe jumla shilingi milioni 279, huku akitaja majina ya wazabuni wawili waliojenga vibanda hivyo, majina ambayo hayatambuliki na Halmashauri wala mchakato wa zabuni haukufanyika. Na madai haya atayakanusha?

Mbaya zaidi, inasemekana Mkurugenzi na watumishi wa Halmashauri wametishiwa kufukuzishwa kazi endapo hawataidhinisha malipo hayo batili. Kama ni kweli, lazima kuna vielelezo vya barua, wasiogope, waweke mambo wazi.

MY TAKE: Kwa sababu hili ni jambo lenye harufu ya rushwa, wizi na matumizi mabaya ya ofisi na fedha za umma; ipo haja ya TAKUKURU na vyombo vya dola kufika Morogoro na kulichunguza kwa undani.

Inaumiza kusikia watu wanataka kuibia Serikali kwa sababu tu wameaminiwa na kupewa dhamana. Watanzania wa leo sio wajinga kiasi hicho. HILI LISIACHWE LIPITE HIVI HIVI!
Arudishe pesa yake bana.

Mnazingua sana nyie. Yaani mtu atumie ada za wanae kuwakopea kisha asipate hata dusko?
 
Sasa si angefuata utaratibu? Kwanini aseme anatoa msaada halafu aje kudai tena na cha juu nje ya utaratibu?
 
Msando mzee wa deal. Watu hawajui pesa anatoa wapi! Acheni wivu mwacheni DC apige kazi acheni majungu! Kama alitoa pesa zake kusaidia watu sasa akizidai kuna ubaya gani? kwani ye padri!! wamlipe tu.

Wamlipe kwa utaratibu upi? Si angetangqza zabuni kisha pesa ikopwe kwa jina la serikali, leo alipwe kwa makubaliano yapi? Hivi unaelewa hata unachotetea kweli 😃😃
 
Haikuwa busara kuanzisha mradi ule pale kwenye like Soko Kwa sababu kutokana na hivyo vibanda vya Msando Frem zisizo Ndani ya Soko kuu zimekosa wateja na pia kuongeza msongamano

Inavyoonekana alibuni mradi ili ajinufaishe kupitia ofisi ya serikali. Watu wamemshtukia. Kama alitoa msaada akaushe, ila kama ni mkopo angedeclare mapema na kufuata taratibu za kisheria.
 
Haikuwa busara kuanzisha mradi ule pale kwenye like Soko Kwa sababu kutokana na hivyo vibanda vya Msando Frem zisizo Ndani ya Soko kuu zimekosa wateja na pia kuongeza msongamano
Vile vibanda angepeleka soko la nane nane au angetafuta eneo mafiga stendi maana wengi wao wale ni wauza mitumba na walikuwa na wateja wao tayari vile vibanda vimechafua taswira ya soko
 
Alijenga kisiasa na inaonekana tayari alikuwa na hesabu zake kichwani.
 
SIRI IMEFICHUKA! Kumbe vile vibanda vya wajasiriamali (wamachinga) katika Soko Kuu la Chifu Kingalu vilivyojengwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando kwa kushirikiana na benki fulani, vimegeuzwa mradi wa kupigia pesa na kuiibia serikali? Hatari sana.

Itakumbukwa kuwa DC Msando alisema anakatwa kiasi fulani cha mshahara wake kila mwezi kulipia deni la benki alilokopa ili kujenga vibanda vile, tena alisema anajitolea.

REJEA: Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando anasema anakatwa rejesho la mkobo wa kujenga vibanda

Imekuwaje leo anadai alipwe na Halmashauri? Lengo lake lilikuwa ni kufanya biashara? Kuilaghai Serikali? Kusaka umaarufu wa kisiasa au kutapeli Wajasiriamali?

Tetesi zilianza kuenea kutoka kwa wajasiriamali wenyewe ambao walidai DC aliwaelekeza kulipia kati ya laki 5 mpaka laki 7 kila mwezi kwa kila kibanda, tena fedha hizo alitaka zilipwe kwenye akaunti yake binafsi. Tetesi hizo zikadaiwa ni uzushi.

Yakaibuka madai mengine kwamba baada ya kushindikana kuwalipisha machinga kiasi hicho kufuatia serikali ya mkoa kuelekeza wamachinga walipe tu bei elekezi kwa soko ili kuipatia halmashauri mapato, DC kuona amekwama akaagiza H/Manispaa imrudishie fedha zake takribani milioni 106 ili alipe deni la benki kwa sababu zilitumika kwenye mradi wa maendeleo, jambo ambalo lilipingwa pia kwa sababu sio utaratibu wa serikali mtu binafsi kukopa na kuja kudai bila kufuata sheria na kanuni. Madai hayo nayo akayakanusha kupitia vyombo vya habari na kudai Mkuu wa Mkoa na Mbunge wanakwamisha jitihada za serikali (yeye) kuwasaidia wamachinga.

REJEA: DC Alberto Msando akopa milioni106 benki ili kuwajengea wamachinga sehemu ya kufanyia biashara

Hivi sasa yapo madai mengine kwamba ameagiza alipwe jumla shilingi milioni 279, huku akitaja majina ya wazabuni wawili waliojenga vibanda hivyo, majina ambayo hayatambuliki na Halmashauri wala mchakato wa zabuni haukufanyika. Na madai haya atayakanusha?

Mbaya zaidi, inasemekana Mkurugenzi na watumishi wa Halmashauri wametishiwa kufukuzishwa kazi endapo hawataidhinisha malipo hayo batili. Kama ni kweli, lazima kuna vielelezo vya barua, wasiogope, waweke mambo wazi.

MY TAKE: Kwa sababu hili ni jambo lenye harufu ya rushwa, wizi na matumizi mabaya ya ofisi na fedha za umma; ipo haja ya TAKUKURU na vyombo vya dola kufika Morogoro na kulichunguza kwa undani.

Inaumiza kusikia watu wanataka kuibia Serikali kwa sababu tu wameaminiwa na kupewa dhamana. Watanzania wa leo sio wajinga kiasi hicho. HILI LISIACHWE LIPITE HIVI HIVI!
Mwacheni Msando alambe asali,Sasa inawezekana vipi msimamizi wa mzinga akose asali?
 
Kwa hiyo mnataka afilisiwe na benki! ? Hivi mnadhani anahitaji Jimbo la Morogoro, kweli?
 
Dada beth umeniuliza kwann nimesema hkn mchaga boya mm nimezaliwa kazkazni nawajuwa vzr Sana hvyo nimesema tukae nao kwa umakini

Yeye na kina mawala na mawakili wengine wameupata utajiri kwa ishu za kitapeli Zaid

Nikadhani unasifia wizi na dhuluma kumbe unatoa tahadhari. Safi.
 
Siku huyu bwana alivyongazwa kuwa Ni mkuu wa wilaya nilishtuka Sana yaani mtu aache dili zake zinazomuingizia mabilioni ya pesa aende kuwa dc ameacha the don na mke mzuri kweli kwenda kuwa dc Tena wa morogoro niliona Kuna kitu kitafanyika mnk huyu jamaa pesa anazo eti Sasa huu udc kwake CYO kitu Ni Kama cheo tu Ila akiki zake zote zipo ktk dili zake za uwakili
 
Niliwahi kusikia pia kuwa hakuwa mwaminifu kwenye masuala ya fedha. Leo yanapoibuka haya basi yasipuuzwe. Vibanda zaidi ya 500 ni vingi sana kama kiongozi atavitumia kwa maslahi yake binafsi. Suala hili lazima lifanyiwe kazi haraka.
Nimepita hapo karibuni yaani vibanda vingi havitumiki vimeachwa tu,hela imeenda bure.
 
Siku huyu bwana alivyongazwa kuwa Ni mkuu wa wilaya nilishtuka Sana yaani mtu aache dili zake zinazomuingizia mabilioni ya pesa aende kuwa dc ameacha the don na mke mzuri kweli kwenda kuwa dc Tena wa morogoro niliona Kuna kitu kitafanyika mnk huyu jamaa pesa anazo eti Sasa huu udc kwake CYO kitu Ni Kama cheo tu Ila akiki zake zote zipo ktk dili zake za uwakili

Inasikitisha sana kijana wa umri wake kutokuaminika kiasi hiki. Unaweza kudhani anachukiwa lakini wanaomfahamu wengi wanasema hiki unachokisema hapa.
 
Vile vibanda vimeharibu taswira nzima ya soko, alafu 106 kwa mbao na mabati yale hapana, parefu sana. Pia afunguke km kweli alitoa msaada wenye maaharti ya kuwa mkopo kwa Manispaa ya Moro. Hata hivyo serikali haifati utaratibu huo wa ujenzi ktk kuanzisha project yeyote.
 
Back
Top Bottom