TAKUKURU mchunguzeni Mkuu wa Wilaya Morogoro, anaitumia ofisi yake vibaya

Nasema hivi, Msando alikubali hicho cheo sio kwa ajili ya mshahara, bali ni sehemu ya upigaji. Sijawahi kusifia wahuni wa aina ya Msando.

Nimekuelewa, lakini hili jambo hata mamlaka haiwezi kulivumilia. Mbaya sana kutumia cheo kutapeli wananchi unaowaongoza badala ya kuwasaidia kutatua changamoto zao.
 
Si waliambiwa wale kwa urefu wa kamba zao!! Wana kibali cha kufanya hayo wafanyayo.

Mh unataka kuleta siasa tena, urefu wa kamba ni kuridhika na kipato chako (mshahara + benefits)
 
Kuna tofauti kati ya kufukuzwa na kufukuzishwa. Soma kwa umakini.

Halafu migogoro ya DCs na Wakurugenzi haipo Morogoro tu, unajua sababu ni nini?

Think.
Sababu ya migogoro ni pesa na madaraka.
Kwenye suala la kufukuzishwa kazi ina maana mamlaka zinazoteua na kutengua hazifanyi uchunguzi kabla ya kufukuza kazi watu au kutengua teuzi?
 
Sababu ya migogoro ni pesa na madaraka.
Kwenye suala la kufukuzishwa kazi ina maana mamlaka zinazoteua na kutengua hazifanyi uchunguzi kabla ya kufukuza kazi watu au kutengua teuzi?

Huijui fitna wewe
 
Yaani mbuzi amchunguze fisi?
 
DC ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, TAKUKURU ataanzia wapi kumchunguza na ni mteule wa Rais?

Takukuru hawana mipaka kwenye kazi zao hata kwa wateule wa Rais mkuu.
 
Abood
 
Takukuru hawana mipaka kwenye kazi zao hata kwa wateule wa Rais mkuu.
Hayo ni maneno tu ya mkosaji, mbona walimshindwa Sabaya mpaka pale alipotenguliwa uteuzi wake? Hii nchi imejaa sanaa sn angekuwa Mtendaji wa mtaa mbona sahivi angekuwa mahakamani
 
Hebu zitaje mkuu maana miye Moro nakujua.

Hawezi kujibu kwa hoja huyo, atakupotezea muda tu na kuleta ushabiki.

Hoja za msingi;

1. DC Alijenga vibanda vya wajasiriamali kama mtu binafsi au kiongozi wa serikali? Kama mtu binafsi kwanini?

2. Kwanini aliita ujenzi wa vibanda hivyo ni msaada na kujitolea huku akisema anakatwa zaidi ya 80% ya mshahara wake kila mwezi? Aliudanganya umma? Kwa maslahi gani?

3. Kama alijenga kama kiongozi wa wilaya, alifuata utaratibu gani? Kwanini hakutangaza zabuni kama sheria inavyoelekeza?

4. Kama ilikuwa ni mradi wa serikali, kwanini alichukua mkopo benki kwa jina lake binafsi badala ya kuchukua kwa jina la ofisi na sasa kuitaka Halmashauri kumrejeshea fedha zake pasipo makubaliano yoyote ya awali?

5. Kwanini alitaka wamachinga wamlipe kila mwezi laki 7 kwenye akaunti yake binafsi badala ya kulipa kwa uongozi wa soko ambazo zitaenda moja kwa moja Halmashauri?

Maswali haya ndio yanapaswa kujibiwa na sio blah blah. Kama hakuna majibu, basi TAKUKURU waanzie hapo na hatua zichukuliwe.
 
Ashughulikiwe inavyostahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…