TAKUKURU mko wapi? Mbunge Musukuma asema wavuvi Kanda ya Ziwa walioombwa rushwa na Luhaga Mpina wako tayari kutoa ushahidi

TAKUKURU mko wapi? Mbunge Musukuma asema wavuvi Kanda ya Ziwa walioombwa rushwa na Luhaga Mpina wako tayari kutoa ushahidi

Sio kweli.... na wewe unatumia ubongo wako kuamini hilo kabisa... uuze hotel kwa 3b kulipa deni la 300m ....hakuna taasisi ya kifedha ambayo ingeshindwa kumpa mtu 300m mwenye Collateral ya 6b... acheni kuwa wajinga wajinga wakati mnaakili timamu.

Ukishapata kesi ya uhujumu uchumi mali zako haziwez Kua dhamana tena
 
Naunga mkono Mpina awajibishwe. Na wakimmaliza Mpina, wamfuate Ridhiwani aliyebatilisha hati ya umiliki wa ardhi kumpa GSM ndani ya masaa 24 tangu aapishwe kuwa Naibu Waziri. Hapa napo kuna harufu ya rushwa kali sana!

Naripoti kutoka Rubambangwe karibu na Hifadhi ya Taifa maarufu sana nchini Tanzania ya BURIGI - CHATO!
Sema unaripoti kutoka gambusi, rubambangwe, kule kwenye jengo alilojengewa mkuu wa wilaya Aishi,ikashundikana, ikashindikana kwa sababu kule ni kambi ya wachawi, baadhi akina Dauda Mpaka walishakufa
 
Msukuma alikuwa wapi? Ushujaa wa kijinga, unamlinda mtu, ukikosana nae uanze kusema madhaifu yake. Mie nashauri wa kwanza kuhojiwa na takukuru ni Dr Msukuma kwa kukalia taarifa, alikalia taarifa kwa maslahi ya nani. Ukimchunguza Msukuma anamambo ya kijinga, ilitokea kwa Lowassa, mtu amekuamini baadae kama jasusi unapeleka habari nje kwa kujipendekeza, ni ujinga!
Musukuma ni raia mwema
 
Mbunge wa Geita Vijijini Mh. Musukuma amehojiwa na chombo cha habari na kueleza kwamba wavuvi wa Ziwa Victoria waliombwa rushwa na Luhaga Mpina, wakati akiwa Waziri wa Uuvuvi, walipomnyima, basi alivunjavunja mitumbwi yao na kuchoma nyavu zao.

Baadhi wanakiri kumpa rushwa Luhaga Mpina TAKUKURU, hivi hili halitoshi kumuhoji na kumpeleka Mahakamani ili ikakate kiu ya haki ya wavuvi hawa?
Wakati Mbunge Msukuma akilishadadia la Mwenzake ( tena mwana CCM ) je, na Yeye yuko tayari Wapiga Kura wa Jimboni mwake waelezee jinsi alivyowapa Rushwa ili wamchague kuwa Mbunge katika Uchaguzi Mkuu uliokuwa wa Kibabe na wa Kimizengwe wa mwaka 2020?
 
Akina Msukuma jibuni kwanza hoja za Luhaga. Hizo sarakasi zenu hazina mashiko
 
Wakati Mbunge Msukuma akilishadadia la Mwenzake ( tena mwana CCM ) je, na Yeye yuko tayari Wapiga Kura wa Jimboni mwake waelezee jinsi alivyowapa Rushwa ili wamchague kuwa Mbunge katika Uchaguzi Mkuu uliokuwa wa Kibabe na wa Kimizengwe wa mwaka 2020?
Musukuma alishinda kihalali, ni mbunge maarufu na anapendwa sana na Wana Geita
 
Mpina akiwa Waziri aliwatesa sana watu wa kanda ya Ziwa.

Namkumbuka jamaa wa Mwanza aliyelazimika kuiuza hotel yake aliyoijenga kwa bilioni 6, akaiuza kwa bilioni 3 ili apate hela milioni 300 za kulipa kwa kile kilichotajwa faini ya uhujumu uchumi kwa vile kwenye underground floor ya hotel yake yalipatikana makokoro.

Baada ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya mwezi, akaona aheri awape hiyo hela ili awe huru.
Hiyo task force yao ilimchomea moto boti yake Rafiki yangu mmoja,

Huko kusini Kuna mvuvi nakumbuka walimpiga risasi ya kichwa
 
Ccm bana, Upinzani haupo Bungeni Sasa Upinzani ni wao kwa wao! Magufuli ametuharbia Taifa sana.
Huwa mnaandika akili zenu hazina late balanced story au hata machapisho mbalimbali?.

Although siwezi kukulaumu ila lazima ujue mambo ya siasa za nchi hii kiundani linapokuja suala la wananchi na mtu kuwa chawa.

Kwa kipindi tulichopo elewa kila mbuge anavuta kamba kulingana na nguvu zake.
Mwisho Mwl. Nyerere alisema mpinzani wa kweli atatoka ccm.
 
Mbunge wa Geita Vijijini Mh. Musukuma amehojiwa na chombo cha habari na kueleza kwamba wavuvi wa Ziwa Victoria waliombwa rushwa na Luhaga Mpina, wakati akiwa Waziri wa Uvuvi, walipomnyima, basi alivunjavunja mitumbwi yao na kuchoma nyavu zao.

Baadhi wanakiri kumpa rushwa Luhaga Mpina. TAKUKURU hivi hili halitoshi kumuhoji na kumpeleka Mahakamani ili ikakate kiu ya haki ya wavuvi hawa?
Msukuma hanaga msimamo. Alimtosa Mzee Lowasa kwa kupewa vipande vya pesa na sasa kalambishwa asali na kina Makamba ili atetee uongozi uliopo madarakani kwa kudhani anakubalika kanda ya ziwa. Subirini 2025 mtajua hamjui. Mpina yuko sahihi
 
Ulikuwa wapi, Msukuma na jiwe walikuwa karibu kwa nini akumripoti hatua ichukuliwe, mbona aliweza kumripoti mkurugenzi wa kahama, huyu alishindwa nini? Unafiki.
Hakuna unafiki mnafiki niwewe rais alisema secta yauvuvi amechaguwa waziri kichaa kama yeye kwahali hiyo unamripoti wapi kichaa upate haki kwasasa uongozi wajuu na ccm yote pamoja naserekali yasasa kwanza watuombe radhi wavuvi pili waturudishie Mali zetu nafidia kwa kutuletea viongozi kichaa na kumteuwa kichaa asante utakuwa umeelewa kuhusu mpina
 
Mbunge wa Geita Vijijini Mh. Musukuma amehojiwa na chombo cha habari na kueleza kwamba wavuvi wa Ziwa Victoria waliombwa rushwa na Luhaga Mpina, wakati akiwa Waziri wa Uvuvi, walipomnyima, basi alivunjavunja mitumbwi yao na kuchoma nyavu zao.

Baadhi wanakiri kumpa rushwa Luhaga Mpina. TAKUKURU hivi hili halitoshi kumuhoji na kumpeleka Mahakamani ili ikakate kiu ya haki ya wavuvi hawa?

Kwanini mnataka kumziba mdomo asiongee?

Kwani hiyo rushwa kala jana? Mbona hamkutoa taarifa Takukuru mnasubiri aongee ndio muone ni tishio kwa ugali wenu?

Mpina ongea usiache itatusaidia kujua wapi kuna tatizo, hata kama ulikuwa na madudu yako wakati ukiwa Waziri potelea mbali maana hawakusema maana yake ni waovu pia
 
Unamtetea huyo muhalifu
 
Stori zingne mwatunga... Kwanini asiweke bond hotel.. badla ya kuiuza..

Back
Top Bottom