DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nchi ikishakua na namba moja alafu kilaza na asieweza fanya maamuzi basi nchi hiyo inakua imefeli sana. Hilo swala la nida nakiri kweli wanazingua japo sina ushahidi wa mtu kutoa hela ila wanausumbufu njoo kesho njoo kesho mpka ukipata namba umesota na bado vitambulisho vikifika serikali za mtaa kukutafuta napo uanze kuomba sana yaani tabu tupu
 
Yani inafika hatua unazisoma comment humu hadi unasikitika tu, kwasababu huna cha kufanya na inaumiza sana.
 
Kuhusu mafuta utayaona Jumatano maana bei itapanda sana kutokana na dollar
 
Kuna mahali nimekuta waganda kama 20 wasiojua hata kuongea kiswahili vizuri, cha ajabu wote wana Tanzania ID
Sasa wa Rw, ndio husema waziwazi, kwamba ukiwa na hela ya kutosha, unapata tu bila shida.

Na kweli wameunga unga makaratasi na wanavyo.

Tumepuuza mambo makubwa na ya msingi sana nchi hii
 
Kwanza nikupe hongera sana mwandishi kwa uzalendo!!

Mara kadhaa nimekuwa nikitoa lawama kwa watu wa usalama kushindwa kulisaidia taifa katika mambo mengi sana.

Mifano ni mingi sana lakini hili la rasilimali za taifa kutumiwa hovyo na watu kwa maslahi ya watu wachache linaumiza sana. Juzi kati tu tumeshuhudia wazawa wakihamishwa kwenye makazi yao rasmi waliopatiwa na mwenyezi Mungu ili tu mwekezaji wa nje apewe hilo eneo afanye kwa manufaa yake, nchi yake na wale waliompatia. Inaumiza sana watu wa usalama ambao kwa kweli ndiyo wanatakiwa kuona ustawi wa mwananchi mmoja mmoja unaheshimiwa lakini wamegeuka kuwa watafutaji na walinzi wa wezi wa rasilimali za taifa.

Hatujakaa vizuri kuna hii issue ya bandari naona nayo kuna upigwaji mkubwa kwa taifa. Hata kama haujui sheria lakini ukiwasikiliza watu wa serikali na ukasikiliza wale wanaooupinga kwa facts unaona kabisa upande upi uko kwa maslahi ya nchi na upi unaangalia matumbo ya watu wachache.

Kuna wakati hii idara inatakiwa isiangalie sura ya mtu ijikite katika kuliangalia taifa maana sisi sote tutapita lakini taifa hili litaendelea kuwepo. Kwanini idara isione kuwa mwaka 2500 taifa letu litakuwa linaiongoza dunia? Nasema hivyo nikimaanisha kwamba lazima waone kuwa rasilimali za taifa hili zikisimamiwa vizuri zinaweza kuifanya nchi kupiga hatua kubwa baadaye. Mfano Magufuli japo alikuwa na madhaifu yake lakini kuna namna alilifanya taifa lianze kuonekana linapiga hatua kwa kasi na usimamizi wa rasilimali za nchi ulikuwa unaona angalau huyu mtu anajali. Hata mirafi mingi ya kimkakati ilikuwa inawapa moyo sana wananchi na ndiyo maana walianza kulipenda sana taifa lao.

Tiss tafadhali msipuuze yanayosemwa na watu nyinyi viapo vyenu ni kwa ajili ya maslahi ya taifa na si kwa ajili ya maslahi ya chama fulani au kikundi fulani cha watu.
 
Ila kumbuka TISS kazi yao si kutekeleza, wao ni kutafuta taarifa,kuchakata ,kisha kuzipeleka kwa boss wao
Hilo nalijua wazi kabisa.

Ila tusibeze nguvu yao ya ushauri, wana njia nyingi za kuhakikisha ushauri wenye manufaa unafanyiwa kazi
 
Point kubwa sana uliyosema kwamba sisi na watoto wetu tutapita, lakini Taifa na vizazi vijavyo vitakuwepo.

Kuna mambo makubwa sana ya msingi hao wenye viapo wameyapuuza.

Leo elimu yetu haizalishi watu wenye ujuzi. Imekuwa elimu ya ovyo.

Leo umaskini unazidi viwango kila siku.


Wengine wana tozwa tozo. Wengine wanaiba hizo hizo tozo.
Ukihoji, Waziri mzima anakwambia hamia Burundi. Huyo ni Waziri kabisa wa serikali.!
 
Ndugu umefanya vizuri kuandika haya! Lakini kwa sisi wazee wa zamani kidogo tunachojua ni kuwa TISS haipo tena kwa maslahi ya taifa! Rais Mwinyi alijitahidi kuboresha kwa kuajiri wataalamu wazuri na kuanzisha idara kamili ya TISS kila wilaya, Mkoa na Taifani. Akawapa vitendea kazi vya kutosha nakumbuka mapajero 500 yaliagizwa mwanzoni!. Muda unavyokwenda hawa jamaa wakawa sehemu ya ufisadi na uasi dhidi ya wananchi. Unakumbuka wasiojulikana na madhara yake? Sasa nani kama mama amewapa nguvu na kinga ya kutoshtakiwa! Aliwarudisha ikulu wamlinde yeye anapouza nchi na raslimali za taifa! Hakuna aliyeshitukia haya.

Wanachoweza ni Ulevi tu kila club wapo wanalewa 24/7 hours. Na kuonyesha vibastola vyao!

Wa kuaminiwa ni TPDF na idara yake ya Intelgence! \Tutafute namna ya kuwafikia!
 
So ni Rushwa kwa kwenda mbelee ..
 
Sasa wa Rw, ndio husema waziwazi, kwamba ukiwa na hela ya kutosha, unapata tu bila shida.

Na kweli wameunga unga makaratasi na wanavyo.

Tumepuuza mambo makubwa na ya msingi sana nchi hii
Kuna siku akili itatukaa sawa
 
Kwani tunapuuza mambo ya msingi kama nchi.?!

Hivi kweli unaweza tazama tu mradi mkubwa kama wa Mbagala mwendokasi unajengwa chini ya viwango?!

Na hujali! Then unajiita na kuji proud sisi, ndio TISS.

Kuhusu Military Intelligence umesema la maana, ila je , unajua ni mara ngapi imezidiwa nguvu ya siasa na hii TISS iliyopo! Anyway tuishie hapo,
 
Umedadavua mambo mengi ya maana sana.

Halafu hii kila mara wakikosolewa wanakimbilia kudai wewe hujui, kazi yetu ngumu sana, tunakesha tunakulinda, wewe umelala usingizi. . .kama ulivyosema mbona wamo tu kila siku kama kazi ni ngumu, lakini si ndio wanalipwa kwa kazi hiyo?!

Na mengi uliyosema, ueledi unapuuzwa sana kwa sababu ya maslahi binafsi, hata ya mtu asiyekuwa serikalini, ana access na hawa wana intelligence, wananchi watakuwa manamba na watumwa ktk nchi yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…