TAKUKURU, Polisi waja na muarobaini wa rushwa za barabarani wakishirikiana na wadau

Kila trafik anapiga hesabu amiliki harrier tk la nyani..... Usipime
Trafik anafanya Kazi kwa siku afunge hesabu kama ataingiza 50000 au 70000
Kuna wakati kulikuwa na tuhuma ya matrafik Kupeleka hesabu kwa wakubwa zao nao?
Nkirudi kwenye suala la rushwa tz ni ngumu kuondoka

Ova
 
Ila wazee ma ofisa wa takukuru na ma police hawapendani sana aisee wakikutana kwny anga zao.

Kuna jamaa wa takukuru alipiga mzinga usiku akiwa na harrier yake tako la nyani alikua mtungi,jamaa wa police walivyokuja kupima wakawa wako fresh tu kwny mambo ya 'favour' ila walivyoambiwa tu jamaa ni takukuru wakasema safi sana ngoja tumnyooshe.

Aisee report ilitolewa bila chenga chenga kama ilivyo,jamaa alikua amelipia comprehensive insurance ya gari yake so hakulipwa chochote kwa report ile ya majamaa.
 
Rushwa na njaa vinaendana
 
Hahah kuna jamaa yangu walimkamata na escudo yake short chasis wakamwambia ndg yangu mbona unatembelea ka gari ka zamani hivi aisee,umekapiga rangi mpk kamegomaa kung'aa jitahidi ununue hata Noah basi hahah.

 
Hahah kuna jamaa yangu walimkamata na escudo yake short chasis wakamwambia ndg yangu mbona unatembelea ka gari ka zamani hivi aisee,umekapiga rangi mpk kamegomaa kung'aa jitahidi ununue hata Noah basi hahah.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
 

Mtoto acha kupiga mayowe. Cheza watu waone wenyewe
 
Kudhibiti rushwa ni rahisi sana. Ikithibitishwa askari wa barabarani amembambikia kosa dereva afukuzwe kazi baaasi
 
Wazo zuri kwa kiasi chake lakini ni wazo na mikakati ya ajabu kama taifa kutafuta tiba ya rushwa 'BARABARANI' ikiwa rushwa 'BARABARANI' inachagizwa na utuamiaji wa vyombo vya moto na watumiaji wa vyombo vya moto hawazidi 25 asilimia kama taifa. Ni ajabu!

Mikakati hiyo ingeelekezwa kila sekta na taifa kwa ujumla maana rushwa 'BARABARANI' ni theluthi tu. Zipo rushwa katika ofisi, shule na huduma mbalimbali za kijamii zinazochagiza theluthi kubwa.

Tiba ya rushwa 'BARABARANI' ni kufumua na kuanzisha jeshi la polisi upya, utuamiaji wa teknolojia, maisha bora na kutengeneza sheria zinazoendana na karne ya 21.
 
Labda itungwe sheria ya kunyongwa akipatikana mtu Ana Toa ama kuchukua rushwa!
Hapo rushwa ndiyo itapungua nchi hii

Ova
 
TAKUKURU imeeleza kuwa Kampeni hiyo imepewa jina la ‘UTATU’ ikimaanisha ni muunganiko wa pande Kuu tatu: TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau

Ni hilo tu au kuna agenda za siri?

Kwanini kampeni hiyo ipewe jina "utatu" ambalo hakuna asiyefahamu kuwa ni neno la msingi kwa imani ya kanisa.

Uislam umekuja kuweka sawa kuwa "utatu" ni shirki.

Wabaduli jina hilo. Halikubaliki na Watanzania wote.

Kampeni ni njema nia ni ovu.

Ntawashangaa sana Mashehe waliokaribishwa kuzungumzia kampeni hii kama hilo la "utatu" watalikalia kimya.

Binafsi sijaafiki kampeni hii kupewa jina hilo na nalipinga hadharani.

Jina hilo libadilishwe na liwekwe jina ambalo halihusiki na imani za watu wa Tanzania ili kuepusha fitna.
 
Rushwa=umasikini + ukosefu wa maadili.

Cctv camera kama zitafungwa maeneo wanaposimama trafiki zinaweza kusaidia kwa namna moja au nyingine.

Njaa ya mapolisi ikiwa ni pamoja na mishahara midogo ni miongoni mwa vichocheo vya vitendo vya rushwa kwa trafiki polices na ndio mzizi wa vitendo vya rushwa.

Ukosefu wa maadili nalo pia ni tatizo sugu kwenye hili swala la rushwa na imani hayo mambo hapo jui yakiboreshwa tunaweza kupiga hatua kadhaa kwenye hii vita.
 
Threat of self review. Same police who take bribe are the one who form part of the task force for the issue.

Citizen who require a meccy from police officers by being un qualified for road running are the one who also a part of the team.

Simba kapewa ulinzi wa mbuzi zizini.
 
Serikali haijaamua kutokomeza rushwa .. Hawa Askari wakifungwa Kama 20 hivi na kesi zao zikaenea nchi nzima rushwa itapungua kwa kasi.

Sehemu zote za rushwa zinajulikana na hao takukuru wanayajua Ni issue ya kisiasa tu kujifanya hawajui hayo maeneo.

Hakuna taasisi ya hovyo Kama takukuru huwa sioni kazi Yao kabisa.. Wanashindwa kuingia field wakamate watoaji na watoa rushwa eti wanasubiri alieombwa rushwa ndio aende kutoa report kwao.. Huu Ni ujinga...

Case nyingi mtaani Ni mtoaji na mtoa rushwa wanashirikiana.. kusubiri muombwaji aende takukuru huku Ni kutojua wajibu wao. Maana yake Ni kwamba wametoa room mombaji na mtoa rushwa wafanye business as usual.

Takukuru ivunjwe Kama si kurekebishwa sijawahi kuona kazi Yao ya maaana.. inabidi wawe kila sehemu kufuatilia utolewaji na utoaji wa rushwa na sio kukaa maofisini kusubiri muombwaji wa rushwa aje ...
 
Huku Moshi ndio kumeoza kabisa. Hiace inasimamisha abiria hapa hapa stendi kwenye askari wa barabarani waliopangwa kuangalia usalama wa abiria.

Magari yanatoka vijijini yamepakia abiria na madumu ya pombe (mbege). Abiria wakilalamika wanadharauliwa kwa sababu kuna wakubwa wanawalinda hao wamiliki wa magari. Tunapata tabu sana hasa magari ya Kibosho Kirima na Umbwe.
 
YEHODAYA, Yaani TAKUKURU kwa hili wanatuhadaa. Sidhani kama hawajui tatizo la trafiki . Hii ni kauli ya kinafiki. Mimi mke wangu ameamua haendeshi tena gari Arusha. Maana hata gari haina kosa lazima utoe pesa. Kuendesha gari Arusha ni kero.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…