TAKUKURU sasa yasema inaanza kuchunguza Vyama vya Siasa kuhusu fedha za mfuko wa jimbo

TAKUKURU sasa yasema inaanza kuchunguza Vyama vya Siasa kuhusu fedha za mfuko wa jimbo

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Najua kuwa mlengwa mkuu ameshajulikana na hapa Lema alicheza kama Pele.

Ilikuwa ni suala la muda tu kwa wabunge waliopita wa CHADEMA kuanza kukumbwa na mshike mshike wa fedha za mfuko wa jimbo. Kama mlikuwa hamjui basi hii ndiyo sababu kubwa ya wao kuangushwa na mamlaka huko majimboni.

Tuwaombee nusura ila yajayo kwao yanafurahisha.

TAKUKURU leo amesema wanaanza kuvichunguza vyama vya siasa kwa wabunge wao waliopita katika bunge la 11 kabla ya uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka huu ambao uliamua hatima yao ya ubunge, kuhusu fedha za mfuko wa jimbo walizokuwa wakipewa wakati wakilitumikia bunge la 11 kama zilitumika kwa usahihi.
 
Tulia, tunataka Sasa kuona Mbeya nzima iko planned
IMG_20201216_080103_2.jpg
 
Wameshindwa kuua upinzani sasa wanaendela kuleta vioja.
Kwa hiyo upinzani mnaogopa nini, mnajua mlifanya hujuma katika hiyo pesa?

Nachojua hata wabunge wa CCM nao watakumbwa na hilo, cha kushangaza kudhibiti pesa za umma nalo ni kosa?
Vijna wa upinzani sasa mmechoka kiakiri.

Kama walitumia vibaya wazilipe tu kisha maisha yaendelee na kama walikula bila kubakiza wacha yawakute.
 
Ccm na upinzani nani wana wabunge wengi? Naona hawajalidhika na wizi na hujuma walizowafania ila kabla hawajapata roho wajiandae kwenda kuzimu.
 
TAKUKURU na hela za mfuko wa Jimbo[emoji23][emoji23][emoji23]

Mwanzoni tulikuwa tunaimba Tanzania ya Viwanda. Mwanzoni tulikuwa tunakemea UFISADI, RUSHWA, UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA.

Sasa ni Tanzania ya DPP kukusanya fedha, TAKUKURU kuangalia matumizi ya fedha za mfuko ya Majmbo, TRA kufunga biashara kwa madai ya malimbikizo ya madeni.

'Wale watu ambao tulikuwa tunasema wanachelewesha Maendeleo sasa hivi hawapo na MUNGU ni mwema wameamua wakae kimya kabisa, badala ya kufanya kazi tuone ufanisi wenu mmeamua kuibua hoja zisizo na mashiko.'

[emoji124][emoji124][emoji124]
 
Fedha za jimbo zinamlenga Mkurugenzi,kwasababu taratibu za matumizi zinaratibiwa na Mkurugenzi.
Mbunge yeye ni muibuaji tu wa mradi.
 
Hahaha wapinzani gani tena ?! Hawa 19 +1 au wale wa ACT?!
 
Kwa hiyo upinzani mnaogopa nini, mnajua mlifanya hujuma katika hiyo pesa?

Nachojua hata wabunge wa CCM nao watakumbwa na hilo, cha kushangaza kudhibiti pesa za umma nalo ni kosa?
Vijna wa upinzani sasa mmechoka kiakiri.
Kama walitumia vibaya wazilipe tu kisha maisha yaendelee na kama walikula bila kubakiza wacha yawakute.
Mkaguzi Mkuu wa fedha za Umma ni CAG. Takukuru wanaingiaje hapo?? Tunafahamu nn kinaendelea baada ya Chama fulani kukataa kuwatambua wale Covi-19.

Viongozi wa Chama kile wako tayari kwa lolote lkn kamwe hawatabadili msimamo wao.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom