TAKUKURU tunaomba Msaada: Kijana huyu alipata ajira Serikalini lakini akaporwa kituo cha kazi na kupewa mwingine

Status
Not open for further replies.
[emoji122][emoji122][emoji122] pambania haki yako mkuu ,wanamazoea mabovu, watu tunapoteza nauli nyingi kutoka Katavi mpaka dsm hafu wanakuwa na watu wao
 

C O N N E C T I O N
 
Huyo dogo hata ka ni kigogo ndo imshinde waziri si wangetangaza hata nafasi ka tatu ili kumweka mtu wao na afanye hyo interview maana wengi hupewa majibu. Hao waja wamezingua kumpoka dogo kazi yake I wonder hata akirudishwa watamtesa tu bure maana hyo kuwekwa ni kutoka juu.
 
Mara unasema aliyeajiriwa hakufanya usaili,

Mara unasema aliyeajiriwa alifeli usaili.

Are you ok?

Pia ikumbukwe kuwa sekretarieti inaweza kumuajiri mtu aliyefaulu usaili katika usaili wa nyuma na kumuacha aliyefaulu katika usaili uliotangazwa.

Waliofaulu wote huwekwa kwenye kanzi data na wengine hupangiwa kazi kulingana na uhitaji na waliobaki hukaa kusubiri nafasi zingine. Ikitokea nafasi hawa hupangiwa hata bila usaili.

Je, aliyeajiriwa alifeli katika usaili ?

Ulipewa nakala ya matokeo ya usaili ya huyo unayesema kuchukua nafasi ya mdogo wako?

Je, imepita miezi mingapi tangu afanye usaili na kuajiriwa?, Ni zaidi ya miezi 6?
 
Kijana kawasiliana Hadi na waziri mchengerwa naye kampiga chenga ya mwili bila msaada
 
Japo huyo wanamuita jina gani! Lakini ujinga huu alikuwa hakubaliani nao.

Tumerudi zama zile za "unanijua"

Upinzani haujipangi lakini kama ungekaa sio kivurugu tu hata hiyo Katiba kuwatoa hawa tungeitaka tena kipindi hiki na kuwatoa.
Huwezi kufanya dhuluma kupitia cheo chako.

Paza sauti dogo. Hao akina Mchendelwa wako ki maslahi bado na kauli za "mkono mtupu haulambwi"
 
Nenda kapost na Twitter kule kuna waharakati kibao tu yaan chaap utapata haki yako maan hata Mama yetu anapenda kuperuzi kule
 
Tarehe 10 mwezi wa 8 Kama utakuwa bado hujapata majibu mazuri nitafute pm nitakutumia nauli toka kijijini toka na nguo nzuri za heshima na documents zako zote uje tunane nikupele kwa hakimu mkuu, anaweza kuhukumu chochote akitaka😭😭😭😭😭 nchi yangu Nani kakuloga?
 
ni magufuri pekee angeweza kukusaidia sababu maugomvi yake yalikuwa na wanasiasa ila kwenye hii sekta alikuwa mwepesi sana kudili na wapumbavu kama hao,ila kwa SAMIA huna utachoambulia maana huwa kama hana time kabsaa na wananchi wake hasa wa chini...
 
Kiukweli kabisa mimi na hao sekretarieti ya ajira sina hamu nayo kabisa,mwenye wa 5 walituita kwenye usaili ambao tuliitwa elfu 3 lakini tuliohudhuria tulikuwa kama elfu 2,tumeingia kwenye usaili Dodoma udom kiukweli kabisa ni kichekesho na maajabu niliyoyaona kwa macho yangu,

mtihani wa writing ulivuja tena sana nilikaa na jamaa pembeni yangu yaani alikuwa anajua kila kitu aliingia na karatasi ya majibu,kiukweli niliishiwa nguvu ya kuendelea na mtihani.

Mamlaka za juu wanatakiwa waichunguze hii tume ya ajira kiukweli kabisa haina maana kuita watu kila pembe ya nchi ilihali wanajua saili wanazofanya hazina maana,heri waite watu wao tu na wawape kazi kuliko mausumbufu kama haya
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…