TAKUKURU tunaomba Msaada: Kijana huyu alipata ajira Serikalini lakini akaporwa kituo cha kazi na kupewa mwingine

Status
Not open for further replies.
Wewe kichwa kigumu kweli[emoji41][emoji41][emoji41] kwani ujaona amepewa na barua kabisa ya kwenda kulipoti kituo Cha kazi, au uko utumishi kwa wahuni waliobeba katika bidhaa ya ajira.
Si utumishi wenyewe wamejibu kuwa ni mistake. Sasa mtoa mada analazimisha tuone kuwa rushwa imehusika.
Rushwa haijahusika hapa, wala undugu haujahusika
 
Wewe umeshapata kazi yako fanya hivi

Ingia twitter tafuta handle ya mama Samia Suluhu utaipata, mtumie vielelezo vyote hivi, kesho yake utapata kituo cha kazi.
 
Nenda kapost na Twitter kule kuna waharakati kibao tu yaan chaap utapata haki yako maan hata Mama yetu anapenda kuperuzi kule
Huu sio ushauri mzuri,akiwatumia hao wanaharakati kumbuka hatopata msaada mzuri na pia itaonekana dogo ni mwanasiasa,apambane tu na hao hao viongozi wa kisiasa wenye dhamani serikalini
 
Udini tu, hamna lolote
 
Pole Sana Mkuu, lakini kama alivyosema Muungwana wa Mwanzo Kabisa hapo, inawezekana hii siyo riziki yako na inawezekana kabisa kuwa kuna Jambo Mungu anakuepusha nalo.
Kubali Yaishe na angalia kwingine maana tayari umeishaingia hasara kubwa.
Pole sana Mkuu.
 
Daaah, pole sana. Huyo Salum Makui ni wa Dini hiyo ya upande wa pili, kwahiyo tegemea lolote, maana wanasema na wao ni zamu yao kutesa, haijalishi kafeli usahili au nini, kikubwa ni kuitwa SALUM
Naona unataka kuharibu hii mada sasa. Sidhani kama suala la dini hapa linahusika. Hata kama linahusika kwa kuwa hakuna ushahidi basi tuachane nalo, ili lisije likazua mtafaruku mwingine.
 
Hii haikubaliki

hao wanaojiita wanaharakati hii ndio kazi yao sasa,, haki ipatikane
 
Ninakupa pole na kukupongeza kwa namna umefuatilia haki zako. Ninashauri uendelee kukomaa. Kitakachofuata hapa ni kutishwa. Usiogope, na ili kujiimarisha endelea kusambaza taarifa hii isambae kama upupu. Ukiweza tupia hata page ya ikulu, waziri mkuu n.k. Mungu akujasirishe na ushinde.

Ninaamini si mmoja anaefanyiwa hivi, ni wengi. Walaaniwe wote wenye tabia hizi
 
Kuna vijana wamefeli maisha tangu wadogo ila ni watoto wa wakubwa
Hapo naona kama mpaka waziri anapata kigugumizi ujue kaambiwa huyo ni mpwa wa fulani au mtoto wa fulani

Pole sana kama hukupata hiyo nafasi kwa kupigania kote huko basi Mungu atakupa haki yako siku moja
 
Maybe amekosea kwa hilo

ila unampangiaje mtu kituo na kumuambia ulifaulu afu akifika huko unamrusha kuwa kuna mwingine?.
Watafte pa kumuweka
 
Si utumishi wenyewe wamejibu kuwa ni mistake. Sasa mtoa mada analazimisha tuone kuwa rushwa imehusika.
Rushwa haijahusika hapa, wala undugu haujahusika
Mistake gani hizi na ugali wa watu?

acheni masihara jmn kisa mtu uko ofisini!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…