TAKUKURU wanamgwaya Tundu Lissu kumuhoji kuhusu rushwa ya Abdul

Abdul ni yule mtoto wa mama Abdul
 
Umeandika ujinga tupu.kwa hiyo Abdul humjui?
 
Wanamhoji Tundu Lissu kama mtoa rushwa au mpokea rushwa?
 
Tundu Lissu akili kubwa. Ukimuhoji lazima aibu itamwangukia huyo Abdul na Maza wake.
Kwahiyo hakuna wa kukubali aibu imwendee Maza
Wakimuhoji lazima ugali wao Maza ataumwaga
Lissu kuchangiwa/kugaiwa gari na raia ambae hana cheo kwenye chama cha kisiasa wala hana cheo serikalini ni jambo ambalo CHADEMA walipigia kampeni.

Mm nahisi wamuhoji mambo mawili, moja lengo binafsi la mtoa gari, na ni nani na nani viongozi wengine wa CHADEMA waliotajwa kupewa "rushwa" na Huyo 'an-duli'. Ambapo pia sio rahisi kulithibitisha hilo mahakamani na serikali kupitia TAKUKURU wataishia kupata hasara tu kwa kumlipa 'an-duli'.
 
Ndio maana bi mkubwa akampa jina la kilabu fulani kibovu kibovu.
 
Wahoji nini na wakati ni kweli? Kwa Lisu kuna CCTV camera Abdul alifuata nini pale?
 
Usijitoe ufahamu, alishamtaja wazi kabisa kuwa ni Abdul Ameir Hafidh mtoto wa Samia Suluhu Hassan.
 
Wanamhoji Tundu Lissu kama mtoa rushwa au mpokea rushwa?
Tundu Lissu ametoa tuhuma za Abdul kusambaza rushwa kwa viongozi wa Chadema na kwamba tayari kuna viongozi wamepokea. Kwa hiyo ahojiwe kuhusu tuhuma hizo zinazochafua CCM na serikali!
 
Tundu Lissu ametoa tuhuma za Abdul kusambaza rushwa kwa viongozi wa Chadema na kwamba tayari kuna viongozi wamepokea. Kwa hiyo ahojiwe kuhusu tuhuma hizo zinazochafua CCM na serikali!
Mtoa taarifa ndiye huojiwa au anayetuhumiwa?
 
Wanaogopa kumuangushia jumba bovu Mama Dulla
 
Mtoa taarifa ndiye hutakiwa kutoka maelezo kwa Jamuhuri kabla hatua za ukamataji hazijaanza!
Naweza kukubaliana nawe, ila tatizo langu nafuata njia aliyokuwa alitumia mwanasayansi na mwanafalsafa mmoja Mfaransa Rene Descartes. Njia hii aliita 'methodical doubt' kwamba atatlia mashaka claims zote kama kuwe na uthibitisho kwamba ni za kweli. Na kwa msingi huo, nitaamini kama maelezo yako ni ya kweli ukiniwekea kifungu cha sheria na sheria inayosema hivyo.
 
Mimi siyo mwanasheria lakini nafahamu uendeshaji wa kesi wa Wafaransa na huu tunaofuata sisi wa Waingereza ni tofauti. Wafaransa wewe unayelalamika ndiye unaendesha kesi lakini Waingereza Jamuhuri ndiyo inayoendesha kesi kwa niaba ya mlalamikaji, kwa hiyo unaweza kuona tofauti hiyo!
 
Nilichosema si procedure ya uendeshaji wa kesi mahakamani, ni njia aliyotumia huyo mwanasayansi na mwanafalsafa, na ambayo hata mimi ninayotumia, kujiridhisha nisije nikadanganywa au kudanganyika. Mimi nimekuomba kifungu cha sheria au sheria ya hapa kwetu inayosema hivyo ulivyodai.
 
Huo ni mtego, TAKUKURU wameshausoma na wanaukwepa.

Ukiona choo kwenye ndoto hata kama umebanwa vipi ogopa kukiendea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…