TAKUKURU waonesha Rushwa ya ngono ilivyokithiri vyuoni

TAKUKURU waonesha Rushwa ya ngono ilivyokithiri vyuoni

Nilijua tutawekewa ka video pia

Ova
 
Mnawaonea wahadhiri tu kuna wale wafundisha mazoezi wanawake nao wanatafuna wake za watu hatareee fireeeee.


Ndukiiiii [emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Kabisa tena iyo ipo sana wale wamama wanagongwa sana na ile mijamaa yenye mbavu za tembo wanajiita walimu wa mazoezi ongereni sana wanaume mnaowapeleka wake zenu Jim wakati viwanja vya mazoezi vimejaa kama vyote
 
Wapo ambao wanawawekea mitego makusudi ili kuwalazimisha hiyo ni mbaya. Zipo zile wao wanapewa tuu. Huo ni ukarimu ila usiathiri taaluma.
 
MBINU inayoongoza kutumiwa na baadhi ya wahadhiri, kushawishi wanafunzi wa vyuo vikuu watoe rushwa ya ngono ni tishio la kuwapa alama za chini kwenye mitihani, imefahamika.

Mbinu nyingine wanayotumia wahadhiri hao ni kujiunga kundi moja la whatsapp na wanafunzi na wahadhiri; na vitisho wanavyotoa kwa wanafunzi hao vya kutofaulu kabisa masomo husika.

Hayo yamebainishwa kwenye ripoti ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu tatizo la rushwa ya ngono katika vyuo vikuu viwili vya umma nchi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).

Utafiti ulifanyika kwenye vyuo hivyo kutokana na ukongwe UDSM, lakini pia idadi kubwa ya wanafunzi wanaodahiliwa na vyuo vyote viwili kwa mwaka.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watumishi 65 sawa na asilimia 29.9 na wanafunzi 174 sawa na asilimia 18.7, walieleza kuwepo kwa ushawishi wa makusudi ili kujipatia huduma kutoka kwa wenye mamlaka.

Takwimu za utafiti huo zinabainisha kuwa mbinu ya vitisho vya alama za chini kwa UDSM iliongoza kwa asilimia 40.5 na UDOM asilimia 38.6, vitisho vya kufeli mitihani ilifuatia kwa asilimia 28 UDSM na asilimia 31.1 UDOM.

Kwa mujibu wa utafiti huo, mbinu nyingine zinazotumika ni pamoja na ahadi ikiwemo ya kuolewa, cheo, chumba chuoni, nafasi ya uongozi, na kuongezewa alama za ufaulu.
Aidha, imebainika kuwa ushawishi wa makusudi kufanya ngono kufanyika kwa asilimia 26.5 UDSM na asilimia 22.4 UDOM.

Aidha, utafiti huo ulibainisha mbinu nyingine zinazowaingiza mtegoni wanafunzi kwenye vyuo hivyo kuwa ni wahadhiri kuwaita wanafunzi kwenye mazingira yasiyo rasmi kwa ajili ya kukagua utafiti inayofanyika kwa asilimia 3.9 UDSM na asilimia 7.5 UDOM.

Mbinu nyingine wanayotumia wahadhiri ni kujiunga kundi moja la whatsapp na wanafunzi, na imefahamika kuwa hilo kufanyika kwa asilimia 1.1 UDSM na asilimia 0.6 UDOM.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utafiti unaeleza kuwa wahadhiri wanafahamu kwamba mwanafunzi anakuja chuoni kwa lengo kuu la kupata tuzo za kitaalum,a hivyo hutumia mwanya huo kwa kuwapa alama ndogo za masomo, kubadilisha alama za ufaulu, kuwafelisha au kuzuia matokeo yao ili kuandaa mazingira ya kuwashawishi kingono.

“Kuwepo kwa ucheleweshwaji wa fomu za mikopo kwa makusudi au jina la mwanafunzi kurukwa ili malipo yake yasikamilike kwa wakati. Hii imekuwa moja ya njia wanayoitumia kushawishi rushwa ya ngono” hiyo ni sehemu moja ya shuhuda kwenye ripoti hiyo.

Ushuhuda mwingine ulionukuliwa kwenye ripoti iyo ya utafiti ni “Mwanafunzi alitakwa kingono na mhadhiri akamkatalia, baada ya kumkatalia mwanafunzi alianza kuona madhara yake kwa kuwekewa alama za chini”

Nukuu nyingine ya ushuhuda wa vitisho vya kushawishi rushwa ya ngono ni “Mhadhiri aliomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi aliyekuwa amefaulu mtihani wa majaribio (test) alikuwa amepata alama 84…lakini mhadhiri hakumrudishia karatasi yake ya mtihani na kumweleza kuwa amefeli mtihani na hivyo yuko tayari kumwongezea alama hadi zifike 84 iwapo atampa rushwa ya ngono,”

Kwa mujibu wa utafiti huo, mwanafunzi huyo alipoenda ofisini kwa mhadhiri, alimkuta yuko na mhadhiri mwingine na alipoomba karatasi yake alikataliwa, kwa madai kwamba yupo kwenye mazungumzo.

“Kwa bahati mhadhiri mwenzake bila kujua kinachoendelea alimshauri mhadhiri huyo amsikilize mwanafunzi, ndipo alipatiwa karatasi yake na kubaini kuwa alikuwa amefaulu kwa kupata alama 84,” ilibainisha ripoti hiyo.

Ushuhuda mwingine uliobainishwa kwenye ripoti hiyo ni kuwepo tabia ya baadhi ya wahadhiri kuwatongoza wanafunzi mapema wanapofika kuanza masomo chuoni kwa njia mbalimbali, zikiwemo kuwapigia simu na kuwatumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za kiganjani.

“Wanafunzi wanapokataa wahadhiri hao huwatishia kuwa watahakikisha hawafaulu katika masomo wanayofundisha...kuna wanafunzi walilalamika kwa uongozi wa chuo kutokana na kukataa kutoa rushwa ya ngono kwa mtuhumiwa uongozi wa chuo ulielekeza usahihishaji wa somo hilo ufanyike upya na matokeo yalionesha kuwa wanafunzi hao walifaulu, uongozi ulichukua hatua za kiutawala dhidi ya mtuhumiwa,” ilisema sehemu ya ushuhuda katika ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa matokeo hayo, yanaonesha kuwepo kwa vitendo vya makusudi vya baadhi ya wahadhiri kulazimisha ngono kwa wanafunzi.

“Vitendo hivyo vinakiuka kifungu cha 25 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Sheria hii inaharamisha kitendo chochote cha mtu mwenye mamlaka kumuwekea kigezo cha ngono mtu yeyote anayetaka huduma yake,” ilieleza ripoti hiyo ya Takukuru.


HabariLeo

Nini kifanyike kukomesha haya
 
Serikali itangaze zawadi nono kwa atakaye kuja na suluhisho kwenye tatizo hili
 
Serikali nayo ijaribu kuwaboreshea maruprup! Kuna mhadhiri mmoja alisema wahadhiri tuna mazingira magumu kiuchumi na hapa chuo wanakuja mabinti wazuri mno kiasi kwamba ukiamua kumtongoza kwa pesa zako basi ukavunje benk na mahtaji ya familia yako uyape kisogo! Maana atakudai ada, matumizi na vingine vingi! So njia nyepesi ni kumalizana nae kwenye coursework!
Hivyo kungeangaliwa upya interraction ya mwalimu na mwanafunzi kwenye hizo coursework!
 
Nina mke wangu anasoma Udom dah aiseee sijui atamaliza salama chuo au Ndio chakula cha wahadhiri
Kama haliwi na ma lecture Basi analiwa na viwana chuo wanyoa viduku au maafisa wa wizara pala dodoma
 
Tufanyeje sasa mkuu?

Watu wanaoa jamii yao humu humu,hawawezi oa people from Mars..wafanyeje?

Wasioe sasa sababu tu Wahadhiri walikula?

Hii ndio Tragedy of Commons
Binafsi sina solution, ya hili. Hapa kila mtu anajifariji kivyake.

Wote tuna pita humo humo lakini ukimuuliza mkeo kabla yangu nani alikuwepo, atakwambia HAKUNA na ukimuuliza bikira ilitokaje atakwambia alipanda mti akapata ajali kisha ikawa imetoka hivyo, anyhow atakudanganya tu.

Mimi nasema wanawake ni mama zetu, bibi na dada zetu. Tuwaheshimu tu walivyo.

Hata wale vyangudoa wa kinondoni ,buguruni na sinza, wakitaka kuolewa anahama mji tu utasikia mtu kanasa, harusi na mwisho ndoa.

Kuna dada kaolewa Arusha huko na alikuwa changu Dar es Salaam, niliwahi kukutana naye akanambia, aliacha uchangu akaamua kuolewa.

Kumbe wanaaamua tu, usijali mimi najiaminisha mke wangu ni safi hakuguswa kabla yangu, that's it.
 
Hawa takukuru bwana nishida tyuuu,Hawa watu wanakazi nyingine na hisi siyo kupambana na rushwa.minaona hiki kitengo kifutwe
 
Mimi sidhani kama mtu mzima huwa analazimishwa kufanya jambo baya.
Na kama unasema huwa wanatoa ngono kwa sababu ya kutishiwa kufelishwa ni wanafunzi wangapi waliwahi kwenda kushitaki na kuweka wazi?
Safi, wakikataa kwa nguvu zao zote wanaweza hata kupewa mtihani ukasahihishwa na jopo la wahadhiri wengine
 
Sio kutoa ngono nakwambia hujakutana na hzo scenario zilivo so usione wanawake wanalalamika ukafikiria ni vichaa, shukuru hujakutana na hyo kadhaa na uombe Mungu isije mkuta mwanao au ndugu

Mimi naishi jirani na chuo kimoja jina kapuni. Marafki zangu wengi ni wahadhiri na mara nyingi nakua nao kwenye ulabu.

Ni kweli kwamba kuna cases za wahadhiri kutumia ubabe kupata ngono, ila in my opinion hizo ni very rare cases. Labda ni asilimia chini ya 5 ndio wanafanya hivyo. Ila kwa hali halisi ilivyo sasa, kwa necha ya mabinti wa vyuo, mhadhiri akitaka kula mwanafunzi hahitaji kutumia nguvu yoyote. Kwanza wanafunzi ndio wanapenda sana kuliwa na malecturer! Nakumbuka wakati tunasoma wanafunzi wakike walikua wanapigana vikumbo kutoka na malecturer huku wakija kujisifu darasani na kuonyesha picha za mitoko, zawadi na meseji wanazotumiana. Kwa jinsi navyoona ma lecturer walivyo na access ya wanawake wengi wanaowasumbua, ni nadra sana kumkuta anahangaika kufosi penzi la mwanafunzi.

Wewe ukitaka kujua aina ya wanafunzi wa vyuo tulio nao sasa, nenda kwenye night clubs. Wanafunzi ndio wateja wakuu wa sehemu za starehe kiasi kwamba kipindi vyuo vikifungwa (kama sasa) club kunadorora kabisa mpaka vifunguliwe tena. Ingia instagram kwenye page zao uone picha wanazopost humo. Mabinti wa vyuo wanapenda starehe kupita maelezo na wanaliwa na kila mtu sio wahadhiri tu, wanaliwa na bodaboda, madereva teksi, wapiga picha, wauza maduka ya nguo na vipodozi, wafanyakazi wa benki, wafanyabiashara, vigogo serikalini na mpaka sisi wenyewe mtaani huku ndio tunapoponea maana hawana gharama wale mradi uwe na usafiri mkali wa kwenda kum "pick" chuo.
 
Safi, wakikataa kwa nguvu zao zote wanaweza hata kupewa mtihani ukasahihishwa na jopo la wahadhiri wengine
Yes,ni mwanafunzi mmoja tu wa NIT ndio aliwahi kujitokeza na kushitaki kuombwa ngono na yule mhadhiri alishitakiwa na vyombo vya sheria.
Hao wengine waliobaki wanapenda wenyewe.
 
Back
Top Bottom