TAKUKURU yaanza kuichunguza CHADEMA kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

TAKUKURU yaanza kuichunguza CHADEMA kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Huyu mkuu wa takukuru pamoja na kuwa ametoka kwenye taasisi inayo heshimika kama JWTZ lakini amekubali kutumika kunyanyasa wananchi wasio na hatia kwa manufaa ya CCM.

Hii ndio hatari kubwa ya kutumia wanajeshi sehemu ambazo sio zao

Wakisha zoea kupindisha mambo ipo siku watapindisha sehemu siyo lwa manufaa yao wenyewe.

Wait and see.
Induce positivity in your mind just once, if it's just allegation why jumping to conclusions?

General Mbungo katoka kutuambia kuhusu TFF juzi tu na kesi bado inaendelea. Mbona kule hukusema katumwa au ndio kila jambo lifanyikalo kwenu ninyi ni siasa?
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Da hii kitu inawezeka au nakubali Takukuru kufanya kazi yake pale inapo bidi ila nionye au nishauri kufanya uchunguzi kipindi hiki ambapo ni mwaka wa uchaguzi,inaleta ukasisi kwa wananchi dhidi ya chama dola ,kwa nini msisubili mwakani bahada ya uchaguzi ili kuondoa hisia za kwamba wenda ni mpango wa chama dola ili kuifuta chadema?
Maana wananchi watajiuliza hata mgekuta madudu sahii kwamba why 2020 out of 5yrs,kwamba pamoja na serikali kua na mkono mrefu ililala?
Je kamati ya ushauri ya chama dola hamjaliona hili kwamba matukio kama haya yanawaongezea umarufu watani zenu na wao wamekaa kimia kama vile hawapo ila wanajua kadri mnavyo wataja ndivyo mnawapigia kamben?
Mwisho
Chama ambacho tiyari kimewai pokea viongozi wakuu katika nchi si cha kubeza na tiyari kina mikakari mingi hasa wenda ya siri zaidi so kukimaliza lazima uje na mikakati ya kisayansi zaidi na kutumia akili kubwa
Uko sahihi, tatizo ni mbowe na ile fukuza fukuza yake. Nimemsikiliza Lijualikali akisema jinsi CHADEMA walivyokwepa kodi kwa udanganyifu wa kutumia misamaha ya wabunge. Siri za aina hiyo zinapokuwa wazi kipindi hiki ni tatizo.

Lakini pia Duniani kote, uchaguzi huwa ndo njia ya kuibua skandali zote!! Hata US ndo msimu wa kuibuka waliotongozwa na kuibiwa, nk.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Wanamtafuta Mbowe na CHADEMA kuiua. Hakuna lolote hapo, ni sawa na ya Idriss, magoti et all na wengine wanaotafutiwa visa kuwafunga. Wamemkosa Mbowe kote, sasa wanamtafuta pa kumbambikia uhujumu uchumi, utakatishaji fedha!
Hapa JF na mitandao mingine, iliibuka clip ya Komu na Kubenea siku zile wakisema wazi kwamba udhaifu wa Mbowe ni wizi wa pesa. Kwa hiyo siyo ngeni, inaeleweka ila nadhani waliiacha makusudi ili iwavuruge CHADEMA.
 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imeanza kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, kuna matumizi mabaya ya fedha za michango ya wanachama, ambayo kwa mujibu wa katiba yao wanadai imeanishwa wachangie.”

“Lakini, matumizi yake ndio wanatilia mashaka, kuna fedha nyingi zinatumika ndivyo sivyo, kwa mujibu wa makubaliano yao,” amesema Jenerali Mbungo.

“Kwa hiyo, tunachunguza matumizi yasiyo sahihi ya fedha zao, Takukuru inayomamlaka ya kuchunguza taasisi yoyote iwe ya umma, watu binafsi, chama, klabu, iwe chochote Takukuru wanaingia kufanya uchunguzi, ilimradi kuwe na ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha na rushwa,” amesema bosi huyo wa Takukuru.

Mbungo amewataja baadhi ya watakaohojiwa ni; Dk. Vincent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema, ambaye kwa sasa amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje Chadema, pamoja na mhasibu mkuu wa chama hicho, Dk. Roderick Lutembeka.

Aidha, Jenerali Mbungo amesema wameshindwa kumhoji Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuhusu sakata hilo, kwa kuwa aliieleza TAKUKURU kwamba yuko nje ya jiji la Dar es Salaam.

Amesema, taasisi hiyo imeshaanza kukusanya nyaraka mbalimbali, zinazohusiana na tuhuma hizo.

“Tumeshapata nyaraka kutoka sehemu mbalimbali, wametupatia nyaraka, wamekuwa wanatoa ushirikiano katika hili,” amesema Mbungo.

Jumamosi ya tarehe 23 Mei 2020, Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, alikanusha tuhuma hizo, akisema kwamba, hakuna uthibitisho unaoonesha chama hicho kina matumizi mabaya ya fedha.

Kigaila alisema, fedha za michango ya wabunge na zinazotoka kwa wadau wengine wa Chadema, matumizi yake hupangwa na vikao vyake vya chama, wakati bajeti ya matumizi hayo ikipitishwa na baraza kuu, kisha taarifa zake hutolewa na kamati kuu ya chama hicho.

Kigaila alisema, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hukagua taarifa za matumizi ya Chadema, na kwamba kwa mujibu wa ukaguzi huo, hakuna ushahidi kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
hawa wanajeshi wakimalizana na chadema watampindua jiwe
 
Chadema sasa hamueleweki ujue, unapopinga ukaguzi huu, maana yake mnabariki ya kina waitara na Lijualikali kwamba ni kweli yanatendeka

Sasa tuambieni tujue moja, mnakaguliwaaa hamkaguliwi?

Halafu ni kama hamna huruma na M/kit wenu mjue, hizi tuhuma zooote hizi zinazomwendea mnadhani yeye ana moyo wa chuma?

Acheni aondokane na uzushi huo bhana!!!

Takukuru, pekenyeni mpaka chumbani huko
 
  • Thanks
Reactions: mmh
PCCB ina wahasibu, mainjinia, wanasayansi, kila taaluma! Maana yake huwa ni hiyo na wana uwezo wa kukusimamisha mahakamani. CAG hana madaraka hayo.

Hata hivyo, huyo boss wa CHADEMA, Mbowe, kwa nini busara yake iko kwenye kunyamazia tuhuma na matatizo ya kifedha? Akisimama huwa anajibu mambo ya mitaani tu! Fedha huwa anakwepa utadhani ni mara ya kwanza kumtaja ktk ufisadi. Sasa yanakuja ya Lijualikali juu ya kukwepa kulipa kodi ya magari kwa udanganyifu. Hayo ndo matatizo ya kutoheshimu waovu wenzake.
Mkuu punguza jazba hijengi mfano
Lijua Kali amekua mbuge chadema miaka mitano na alikiri kwamba anamuogopa mungu kwenye press yake na kwamba ataki siku moja chomwa moto ndo maana akaamua ongea ukweli swali.
Kama aliyajua mapema yote haya why hakuwai kupeleka tahalifa hewani ambapo Wenda TAKUKURU ingekua imefanya Nazi yake,mpaka asubili kujitoa kwenye Chama?
Kujibu kwa hoja inaweza ikawa inatusaidia sana kuliko kuweka ushabiki Wa vyama vyenu Mbele mkuu
 
Such nitwits.

Toka lini matumizi mabaya ya fedha yakawa kosa kisheria ?????

Huyo kamanda wa TAKUKURU ataje kifungu cha sheria kinachosema mama watoto akiona baba mwenye nyumba anaendekeza starehe na kufuja hela ya familia basi anaweza kumuitia TAKUKURU.
 
Mkuu punguza jazba hijengi mfano
Lijua Kali amekua mbuge chadema miaka mitano na alikiri kwamba anamuogopa mungu kwenye press yake na kwamba ataki siku moja chomwa moto ndo maana akaamua ongea ukweli swali.
Kama aliyajua mapema yote haya why hakuwai kupeleka tahalifa hewani ambapo Wenda TAKUKURU ingekua imefanya Nazi yake,mpaka asubili kujitoa kwenye Chama?
Kujibu kwa hoja inaweza ikawa inatusaidia sana kuliko kuweka ushabiki Wa vyama vyenu Mbele mkuu
Dunia hii haina watu wema kiasi hicho. KWamba kila siku wakiona maovu wanasema. Wema wapo waovu wapo. Iko siku wote hao wanaamua kusema ukweli. Hata waovu kuna siku wanaamua kusema yote! Tatizo la Mbowe na wenzake ni kwamba wanashindwa kuwaheshimu waovu wenzao ili siri ya uovu wao ubakie ndani.
 
TAKUKURU wakishamaliza uchunguzi wanapeleka kwa DPP? hiyodouble standard vepeee kamanda? kwani unajua matokeo ya uchunguzi tiari?....[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
mkuu hao wote c walamba viatu vya jiwe,wakilinda mkate wao wa siku
 
Back
Top Bottom