TAKUKURU yaanza kuichunguza CHADEMA kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

tatizo huna elimu na maarifa kaongeze
 
Pole sana,
Waonaje ukiwaachia wenye ufahamu na pia wamejaaliwa hekima/busara ndio waongee. Mwenyekiti wa chama ni taasisi. Hata hivyo nawe kama unavyo vielelezo basi kimbia kuvipeleka. Yowe za aina yako hazina msaada wowote kwenye mjadala wa mambo ya msingi. Amen
 
Hii habari kama ni kweli basi ni sawa na kulima bustani ya mchicha kwa kutumia bludoza/katapila.
Kwa hali ilioko kwa sasa ndani ya CHADEMA kupambana nayo hakuhitaji nguvu kubwa ya kiasi hicho.Yaani vyombo vyote vya dola vinashiriki kwenye mapambano
"Ubeberu hauna rangi, ubeberu ni ubeberu tu" Samora Machel 1975
 
Najua umeanza kuona kwamba siko kiwango chako. Huu ni uwanja wa majadiliano. Unaposhindwa kujadili unanituma niende sijui wapi. Tuko hapa JF kwa majadiliano na tunafahamu huko nje pakoje. Kama una ufahamu lete facts. These are things they don't teach you at school.
 
Najua umeanza kuona kwamba siko kiwango chako.
Ni kweli kabisa,
kwangu mimi kama twiga ni kichekesho sana kuacha majani safi ya juu mti na kuja kula nanyi, majani ya wa aina yako/yenu ya huko chini.
Over & out
 
Ni kweli kabisa,
kwangu mimi kama twiga ni kichekesho sana kuacha majani safi ya juu mti na kuja kula nanyi, majani ya wa aina yako/yenu ya huko chini.
Over & out
Boss! Quote message yote ili busara ionekane. Nilichokiandika ni:
 
Sio kweli TRA wamekuwa wakifanya special audit kibao watu wanadaiwa Kodi kibao za miaka ya nyuma yakiwemo mashiririka ya umma
Kwani huko TRA wanakofanya special audit kunakaguliwa na CAG?
 
Naunga mkono kufanyika kwa huo uchunguzi ili wadau tuweze kufahamishwa kama ni kweli kuna huo ubadhirifu au ni nongwa tu ya wale makada wanao kihama chama.
Usitangulize lawama zisizo na msingi ,jiulize takukuru kisheria wanayo hiyo haki ya kufanya hivyo?,kama wanayo usimlaumu Mbungo,najua ingekuwa wanahojiwa Nccr Mageuzi ungepiga shangwe la kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiulize kwanza
1. Kwanini.muda huu
2. Kwa nini tuhuma za ccm hazijawahi kwenda takukuru
3. Kwanini ile 1.5tr takukuru hawakugusa
4. Kwanini wanao hama wanatetewa na ccm
5. Kwanini wanao acha ubunge tola chadema wanapewa kugombea ccm bila kupingwa?

Kuna mambo mawili
1. Nccr kuwa kuchaka cha kutetea mambo ya hovyo yanayo fanywa na ccm

2. Ccm kufa 2025 na NCCR magufuli kuchukua nchi.


Niliwahi sikia mkui aliwahi chukua card ya nccr mageuzi

Pia nccr mageuzi inekua inapngozwa na watu wa system toka enzi za mrema.

Mbatia ni mtu wa ccm ameletwa upinzania kwa sababu maalum

Kwanini serikali inaiogopa chadema, si waache tuu chadema ishiriki uchaguzi na waibe kura.
 
hatutaki porojo wala utani wala siasa illiterate DJ asakwe popote alipo awekwe mtu kati kujibu wizi wake za mwizi arobaini, watu wa ndani na ni watu wazima wenye heshima zao wabunge wa jamhuri hawa wameripoti kuibiwa chenji zao uchunguzi uwe serious DJ lazima akamatwe afilisiwe sababu “kufa kwa nyoka ni kukatwa kichwa”
 
hivi upotevu wa Tsh tririon 1.5 ilichunguzwa na nani baada ya report ya CAG...,TAKUKURU nayo inaenda kuingia kwenye mtego wa siasa za kilaghai za ccm...poor them
 
**** msemo mmoja yesu aliwaambia mafarisayo kuwa, MKIWAZUIA HAWA WATU KUONGE, NITAYA HAMRU MAWE YAONGEE. HAKIKA NAWAAPIA NDG ZANGU NA MARAFIKI WA JF, HATATOKEA BINANADAMU KATIKA KARINE HII WA KUIZUIA DEMOCKRANSIA, Hata chadema wakifugwa, Viongozi wakiama na hata baadhi ya wanachama, LAZIMA TU WATOKEE WATU WA KUOJI.
 
Kwa hiyo TAKUKURU wameamua kufanya kazi ya CAG?
PCCB wanakagua tuhuma. CAG ni kitu kingine kabisa. Tuhuma toka kwa wabunge waliokihama chama na baathi ya wanachama wasiojulikana wanalalamika. Wanasema kuna ubadilifu kwenye pesa walizozichanga na Ruzuku. CAG alikagua matumizi na madeni ya chama. Ruzuku ilivyotoka na kufanya kazi. Wanaoana ni safi. Kumbe hile safi kuna matumizi asiye halali, kulipa kasich halali kwa mfano
 
Kwani huko TRA wanakofanya special audit kunakaguliwa na CAG?
Ndio special audit za TRA hazibagui wewe Ni private au taasisi ya serikali ambayo CAG hukagua .CAG sio final .TRA ,Takukuru waweza zuka wakati wowote
 
Huna unachofahamu wewe! CAG anakagua matumizi na mapato yote ya chama, haijalishi ni michango au ruzuku. Hivyo tuhuma zote zinatakiwa kuanzia kwa CAG.
 
Ndio special audit za TRA hazibagui wewe Ni private au taasisi ya serikali ambayo CAG hukagua .CAG sio final .TRA ,Takukuru waweza zuka wakati wowote
Soma vizuri katiba ya nchi utaelewa mamlaka ya CAG katika fedha za umma. TAKUKURU inakaguliwa na CAG lakini TAKUKURU haiwezi kumkagua CAG. TAKUKURU inachoweza kufanya kwa CAG ni kuchunguza jinai.
 
Hivi yule Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo aliyetuhumiwa kupora zaidi ya Bil . 1 katika kikao cha madiwani wa Ubungo vipi Takukuru wamefikia wapi na Kesi yake?

Vipi kuhusu yule Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo (TADB) aliyejichotea mahela akaenda kukarabati nyumba ya kupanga nae vipi kesi yake imefikia wapi? Manake hizi ni kesi zilizotangulia kabla ya kesi ya cdma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…