NAWATAFUNA
JF-Expert Member
- Nov 14, 2019
- 13,284
- 24,047
kwanza kwa nini mbowe akiulizwa kuhusu fedha za chama anakuwa mkali?Ndungai alikula bilion 12 , na bilion 251 zilipotea wizara ya ujenzi Mbona Taifa limekaa kimya? Kipo wapi kivuko cha Dsm Bagamoyo?
TAKUKURU wamechukua hatua sahihi tutajua mbivu na mbichi
Wao ahadi yao ilikuwa kufuta upinzaniWatanzania waliwatuma Maendeleo, na Siyo kazi ya Kuhangaika na Mbowe.
Ona Sasa Maisha Magumu, Uchumi umeshuka, kila siku ni Mbowe.
Wanajeshi wakiwa jwtz hawapindishi wakitoka nje wanapindisha sana ndiyo maana kaacha kuchunguza bilion 12 za Ndungai kaenda kuchunguza chademaWanajeshi hawapendi kupindisha mambo mmezoea kupindisha sana mlisema mko safi leo maji ya shingo
Kama nyie ni wasafi mnaogopa nini na hati zenu safi
Asante Kwa mapendekezo, Lakini Kwa nini nyie Chama ambacho ni safi, mbona ni kama mnaogopa kuchunguzwa?Takukuru wachunguze Ndungai akiwa Hosptal India kwanza
Weee jamaa sio bure comments zako nyingi huwa sizielewi kabisa sijui huwa unacomment bila kifiria unaandika nn? Usije sema nimekitukana,comments zako nyingi zimekaa vibaya sana,hebu kaa ujitafakari vizuri na hebu onyesha ni wap Ccm au Chadema ni Mpango wa MunguNachokiona hapo ni njaa za ccm / chadema nimpango wa Mungu
Mkimaliza kuchunguza what the next ....
Waliahidi viwanda viwanda sasa imekuwa Nchi ya kesi kesi kesiWao ahadi yao ilikuwa kufuta upinzani
TRA pia wadai Chao kwa Mbowe kwakinachoitwa walikilikopesha chama kwa riba.Je Mbowe kasajiliwa benki kuu akapewa leseni ya kuendesha biashara ya mikopo? Wote wanaosema walikopesha chadema kwa RIba TRA na BOT washukieni Kama mwewe.TRA daini chenu na malimbikizo ya Kodi ya hiyo ribaKumekucha ufipani.
Wewe mwenyewe mchafu jichunguze wewe kwanza ukiwa msafi ndipo unaanza kuwachunguza wengine waanze na kivuko cha Dsm Bagamoyo bilion 12 za Ndungai, bilion 251 wizara ya ujenzi na zingine nyingi huko CCM kwanza kabla hawajaenda popoteAsante Kwa mapendekezo, Lakini Kwa nini nyie Chama ambacho ni safi, mbona ni kama mnaogopa kuchunguzwa?
Au ndo mlikuwa mnakula pamoja na mkuu wenu, mbona ni kama mnajitetea Sana mkuu
Kudadeki watulie sindano iingie walitaka wenyewe .chama hiki kimejaa rushwa sana rushwa ya ngono na rushwa ya vyeo na rushwa ya pesawanalia sababu wanaona c haki kuchunguzwa na aliyeteuliwa na mwenyekiti wa ccm
Tayari lengo ni kusaka kisingizio cha kuahirisha uchaguzi kwani endapo chadema watasusia uchaguzi itabidi kuahirisha
Kama CAG alishafanya ukaguzi na ikaonekana hakuna ubadhilifu, TAKUKURU wanaingiaje hapo?TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imeanza kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
“Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, kuna matumizi mabaya ya fedha za michango ya wanachama, ambayo kwa mujibu wa katiba yao wanadai imeanishwa wachangie.”
“Lakini, matumizi yake ndio wanatilia mashaka, kuna fedha nyingi zinatumika ndivyo sivyo, kwa mujibu wa makubaliano yao,” amesema Jenerali Mbungo.
“Kwa hiyo, tunachunguza matumizi yasiyo sahihi ya fedha zao, Takukuru inayomamlaka ya kuchunguza taasisi yoyote iwe ya umma, watu binafsi, chama, klabu, iwe chochote Takukuru wanaingia kufanya uchunguzi, ilimradi kuwe na ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha na rushwa,” amesema bosi huyo wa Takukuru.
Mbungo amewataja baadhi ya watakaohojiwa ni; Dk. Vincent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema, ambaye kwa sasa amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje Chadema, pamoja na mhasibu mkuu wa chama hicho, Dk. Roderick Lutembeka.
Aidha, Jenerali Mbungo amesema wameshindwa kumhoji Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuhusu sakata hilo, kwa kuwa aliieleza TAKUKURU kwamba yuko nje ya jiji la Dar es Salaam.
Amesema, taasisi hiyo imeshaanza kukusanya nyaraka mbalimbali, zinazohusiana na tuhuma hizo.
“Tumeshapata nyaraka kutoka sehemu mbalimbali, wametupatia nyaraka, wamekuwa wanatoa ushirikiano katika hili,” amesema Mbungo.
Jumamosi ya tarehe 23 Mei 2020, Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, alikanusha tuhuma hizo, akisema kwamba, hakuna uthibitisho unaoonesha chama hicho kina matumizi mabaya ya fedha.
Kigaila alisema, fedha za michango ya wabunge na zinazotoka kwa wadau wengine wa Chadema, matumizi yake hupangwa na vikao vyake vya chama, wakati bajeti ya matumizi hayo ikipitishwa na baraza kuu, kisha taarifa zake hutolewa na kamati kuu ya chama hicho.
Kigaila alisema, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hukagua taarifa za matumizi ya Chadema, na kwamba kwa mujibu wa ukaguzi huo, hakuna ushahidi kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
CCM wameshindwa kuchunguza bilion 12 za Ndungai sasa wanaenda kudhoofisha chadema kisa uchaguzi mkuu
Unayajua majukumu ya TAKUKURU mpaka useme wamechukua hatua sahihi mkuu?TAKUKURU wamechukua hatua sahihi tutajua mbivu na mbichi
Billion 8 zote na kwenye mahesabu ya CAG haionekani hahahahaiwezekana mbowe achukue bilioni 8.9 michango ya wabunge wa chadema alafu taifa likae kimya
Hali yenu ngumu sana mnaishi kwa hofu kuuKatika nchi ya wabambika kesi, ambapo tumeshuhudia Sugu asiye na kosa "akitumikia" kifungo, na mchakato wa rufaa yake kucheleweshwa kiasi kwamba hata alipokuja tangazwa "hana hatia" tayari ishakuwa JUSTICE DELAYED IS JUSTICE DENIED".
Mchezo huo umerudiwa kwenye kesi dhidi ya viongozi wa CHADEMA , ambapo wahalifu wa ukweli, CCM, NEC na Jeshi la Polisi, wameachwa. Wahanga, AKWILINA na CHADEMA, wamekosa haki. Na CHADEMA wakahukumiwa vifungo na faini hevi, baada ya kutumia miezi kibao wakihangaika na hiyo kesi feki, huku Ndugai akidai kwamba Mbowe ni mtoro bungeni.
CCM "wamefanikiwa" kudesign njia za kuwasumbua viongozi wa CHADEMA, kuwaondoa mchezoni kwa mfululizo wa kesi feki, kucheza na sheria ili waadhibiwe bila kihukumiwa, kwa kuhakikisha hawapati dhamana, nk.
Ni TAKUKURU hii hii iliyoletewa ushahidi kuhusu vitendo vya rushwa alivyofanya Alexander Mnyeti, enzi hizo akiwa DC, dhidi ya madiwani na wabunge wa CHADEMA , ili "waunge mkono juhudi". Takukuru "wakiukataa" ushahidi huo kwa kisingizio kuwa ilishavujishwa mitandaoni!
Lakini wenye akili tulijua TAKUKURU hawana ubavu kumpeleleza kipenzi wa Magufuli.
Chombo sahihi cha kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizi ni ofisi ya CAG. TAKUKURU ni rahisi kutumika ili kuwasumbua viongozi wa CHADEMA , kipindi hiki cha uchaguzi, ili kuwatoa mchezoni. Wanaweza kuwafungulia kesi feki kama zile zingine. CAG akishachunguza ripoti yake hatimaye hutua bungeni ambapo kila kitu kitaanikwa wazi. Huu ni mchakato ambao hautakuwa na manufaa sana kwa CCM.
Ndio maana "maagizo kutoka juu" yameelekezwa kwa TAKUKURU.
Mnaishi kwa hisia mpompo tuChadema hata wakiwa safi watatafuta kisingizio wata-force chochote ili mradi wapate pa kuwakandamiza