Uchaguzi 2020 Takwimu hazidanganyi: CCM wameshashinda Uchaguzi kwa Idadi ya Kura za Kanda ya Ziwa

Wewe mtoa mada hii, hivi jana ni shule gani ya Mwanza ambayo haikufungwa kwenda kujaza uwanja wa Kirumba? Mbona waalimu wote waliambiwa wakasaini kudhuria kampeni za ccm, kama anapendwa kwa nini wafanyakazi wamelazimishwa? wewe mpuuzi kweli
 
Anafanya kampeni kulinda na kusuport democrasia lakn pia awe bora zaid kwa kikundi cha wahuni wanaojiita wapinzani
Kumbe na bishana na lofa.kuhita wapinzani wahuni ni lazima uwe lofa wa kiwango cha juu
 
Kwa nini analazimisha watu waende kwa lazima kuhudhuria kampeni kama anakubalika?
 
Ukiachilia mbali kuwa JPM amefanya vyema katika uongozi wake wa miaka mitano, sera na mikakati kwa ilani mpya lakini pia coverage aliyoifanya JPM kuwafikia wananchi haswa wa vijijini ni kubwa mara dufu, Tunataraji ushindi mkubwa kwa CCM na JPM uchaguzi huu
 
Kweli Tundu Lissu kawashika MATAGA kunako....

Lissu shikilia hapo hapo usilegeze baba - imeisha hiyo!
Hahahaha hata wakati Mange anawahamasisha kuingia barabarani mlijipa moyo hivihivi lakini matendo ikawa sifuri. Makamanda full matumaini
 
Pole sana Magufuri siyo msubi. Hilo eneo la chato robo tatu ya wakaazi ni wasukuma ambao walihamia miaka ya katikati ya hamsini kwa ajili ya kilimo cha pamba. Si hapo tu chato wasukuma wapo shimwanyi, kyamuyolwa ambayo yako wilaya ya Muleba eneo lote la kusini ya mji wa Biharamulo hadi Kakonko mkoani Kigoma wasukuma wamejaa na sasa wameshaingia wilaya ya karagwe na wanalima mpunga na kufuga kwa kwenda mbele. Halafu eti unasema Geita Magufuri hapendwi Geita, nani anakudanganya, mkoa wa Geita una majimbo ya Uchaguzi saba na yote CCM ilishinda mwaka 2015. Aidha, kusema eti Mara ni nusu kwa nusu ni uongo, mkoani wa Mara kwenye upinzani wa kweli ni Majimbo mawili tu ya Tarime, wakati Rorya, Musoma mjini na vijijini, Bunda vijijini Mwibara pamoja na Butiama na robo tatu ya Serengeti ni CCM tu kwa kwenda mbele, sasa hiyo nusu kwa nusu unaipata wapi ? Huko Kagera upinzani ni robo tu kote CCM tu. Wadanganye wasioifahamu kanda ya Ziwa.
 
Ngoja nijibanze pembeni kushuhudia unavyovurumishiwa matusi
 
Kura Milion 11 zinatoka wapi?
 
Naona Bashiu kawatuma na mmesikia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wee jamaa vipi...

Wakulima wa hili zao letu ,walokua wanauza mzigo Uganda kwa bei kubwa.


Jiwe akaamlisha wasiuze, serikal itanunua matokeo yake, Chini ya Polisi, na wenye viti aa mitaaa, wakawa wanapita mji hadi mji. Wanakupigia hesabu yao utake usitake????

Unadhan iyo ni Bukoba mjin?????



Wee jamaa vipi weee hahahahahahah


Subiri Lissi aende.
 
Kuna kitu ukielewe.kuna watu wanaipenda ccm ila hawampendi magufuli yeye kama yeye.mimi niko kwenye hilo group na ni mwana kanda ya ziwa ila hata chato kuna watu hawampendi magu tena wengi tu
 
Magu Hana watu, Hao wanaenda wakidhani watapewa hela, watumishi wanafunzi wanalazimishwa, Malori yana Simba watu kutokamikoa ya jirani kupeleka watu, wengine wanafuata tamasha la fiesta

Hizo takwimu zinakudanganya, umeona shazi la zenji Jana?
 
Kuna kitu ukielewe.kuna watu wanaipenda ccm ila hawampendi magufuli yeye kama yeye.mimi niko kwenye hilo group na ni mwana kanda ya ziwa ila hata chato kuna watu hawampendi magu tena wengi tu
Mbona huko chato na maeneo mengine ya mkoa wa Geita wapinzani hawana jimbo hata moja ? Hao wanagroup wenzio ni kama tone la maji katika bahari kuu.
 
Mleta mada anaamini watakaojitokeza kupiga kura ni kati ya 12m hadi 16m halafu kanda ya ziwa anakuambia kwatakwimu zake mgombea wake atapata 11m ambao kwa hesabu zake ndio wapigakura waliopo kanda ya kati na ziwa pia ushahidi wake mkubwa ni kujaza mikutano ila amesahau variance za ujazaji mikutano kwa factor kama za wasanii wanaovutia watu kujaa na watoto wadogo wanaokuja kujaza mikutano ile hali upinzani ni sera tu bila wanasanii hivyo anapelekea kuwa na takwimu zisizo na uhalisia muhimu nikuruhusu uchaguzi huru na wa haki kila mmoja ahubiri hilo na mazingira hayo yawekwe hivyo na media ziwe fair kwa wagombea wote hakika mtakuja kujua hamjui na hilo liko wazi mnalifahamu.
 
Ukweli ni kwamba kukiwa na haki, magu hatapata zaidi ya 45% percent. 55% zinakwenda kwa Lissu na wengine.
 
Takwimu wa waganga 300 wa gamboshi.
 
Mbona huko chato na maeneo mengine ya mkoa wa Geita wapinzani hawana jimbo hata moja ? Hao wanagroup wenzio ni kama tone la maji katika bahari kuu.
Elewa point yangu mkuu ni kwamba ccm inapendwa ila magu hapendwi sana kivile so ubunge wanawapa ccm za urais wanagawana na akina rungwe na membe na lissu
 
Ukweli ni kwamba kukiwa na haki, magu hatapata zaidi ya 45% percent. 55% zinakwenda kwa Lissu na wengine.
Aise Kuna watu mna roho ngumu. Yaani hizo kura huyo Lissu anazitoa wapi, au haya ninayoyaona kwa TV nyie hamuyaoni. CCM pamoja na Mgombea wake kukubalika Nchi nzima, bado wamejipanga vizuri Mno ndani ya wiki moja tayari ni Kama wamefika Robo ya Inchi. CDM na viongozi wote mmelundikana sehemu moja tu.
 
Chaguo la ibilisi na malaika zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…