Apewe muda, kwani mfumo uliyotengenezwa na mabeberu wa kuinyonya Afrika umefika mbali na kuota mizizi si rahisi kuondoa mara moja, na kuendesha nchi kwa jinsi anavyofanya Traore usitegemee matokeo yatakuwa kama chumvi kwenye chakula, hata hivyo mpaka sasa hajafeli kitakwimu, na jitihada yake yote ya kutaka kujinasua kutoka katika unyonyaji wa wazungu ni mchakato mgumu unaouhitaji uthubutu, ujasiri na subira, na hii haiwezi kufanywa na mtu mmoja bali iwe ndiyo dira na sera ya nchi katika kuleta mabadiliko ndani ya nchi kwa maana hiyo hata leo Traore akiondoka madarakani basi mrithi wake awe na msimamo huohuo kama wa aliyeondoka.
Na katika mambo anayoyafanya Traoré ni:
- Anapinga ukoloni mamboleo na kuikataa France kuendelea kuchota raslimali za Afrika.
- Ameimarisha ulinzi wa ndani kwa kupambana na makundi ya kigaidi bila msaada wa nchi za Magharibi.
- Anahamasisha uzalendo na kujitegemea (kuondoa mitazamo ya utegemezi).
- Ameshajinasua kutoka kwa vibaraka wa kisiasa waliokuwa watiifu kwa mabeberu.
Wabukinabe wastahamili katika hichi kipindi kigumu lakini wakipita salama watafurahi na hali ya ustawi wa taifa lao.