Talaka inavyoniaribia Binti yangu mapema💔

Nadhani ni malezi pia au ukuaji wa mtoto mwenyewe
Yah ni kweli. Ila ni bora mtoto akawa mtoto. Mimi binti yangu ana maswali mengi sana lakini ni yale, unaondoka, utachelewa kurudi, unaenda wapi, baba ulikuwa wapi, huyu ni nani, mama atakuja lini kukaa na sisi kama fulani anakaa na baba na mama...
Ana image ya family lakini si ndoa wala kuolewa hayo hayaelewi elewi bado.
 
Mpaka hapo kakua ndo anakoelekea pia...mi mwanangu wa kiume ni miaka 9 pia lakini hathubutu kuniuliza maswali ambayo anajua yataniumiza japo najua anatamani kujua mengi ila anahuruma sana...huwa ananiangalia sana machoni kujua hali yangu au mood yangu.Ni mwema sana kwa kweli.
 
Kweli mkuu! Watoto wanatofautina uelewa.
Nakumbuka mimi kijana wangu alinipa wakati mgumu sana alipokuwa na miaka mitano. Alikuwa akiuliza maswali magumu na yenye kutaka majibu sahihi.
Lakini pacha mwenzie ambaye ni wa kike hakuwa na mambo hayo.
Kuna wakati nilikuwa naona aibu tunabaki tunaangaliana na mama yake.
 
Aisee🤔 MUNGU amlinde huyo mtoto wa kike.

Wazazi ni wajinga kabisa, hizi ni ndoa za ujanani au ndoa za fasheni. Watu mmezaa na watoto bado mnafikiria kuachana, kwasababu zipi za msingi?

Nyinyi wote ni viazi, akili zenu zinafanana.

Mwambiy huyo mjinga mwenzako, mlikuwa hamna sababu ya msingi ya kutengana, hakuna Jambo ambalo lilikuwa la msingi Kama kulea watoto.
 
Pole sana mkuu, ila unapaswa kujiuliza wewe upo tayari tayari kabisa kumuacha aende?

Katika maisha ya ndoa/uhusiano hua kunakipindi baina ya mmoja huwa anakengeuka. Kipindi hiki huwa ni kigumu sana ambapo kama ikikosekana umakini watu hawa hujikuta wametengana ile hali bado wanapendana.

Kingine ni mtoto anaposema jambo la kikubwa ujue limetoka/kalisikia kwa mtu mzima. Unapaswa ukae na binti yako umueleze ukweli halisi mambo yalivyokuwa kama wewe ndiye mwenye makosa au mama yake. Na usioneshe kumnyooshea zaidi kidole mama yake. Usitie uongo hata kidogo ili wewe uonekane kujisafisha. Yule ni mtoto bado ni malaika, utafanya mambo yawe magumu zaidi.

Fanya linalowezekana uongee vema na mkeo. Huyo bado ni mkeo.

Muulize kama yuko tayari kuona watoto wakiukosa upendo wa baba na mama? Yuko tayari kuruhusu hili ile hali yeye bado yuko hai?
Zungumza naye maneno ya kihisia zaidi... gusa point muhimu..
Yaani dah.. natamani hata ningekutwangia simu nikuelezee... 🤗

Hilo swali la "Kwanini uliachana na mama?" sio la mtoto ni la mama. Yang'amue vizuri maswali anayo kuuliza huyo bintiyo.

Lakini inaonesha wife bado anakuhitaji ila anashindwa ajirudishe namna gani. Hawezi kujirahisisha ataonekana bwege. Mfungulie njia umrudishe.
 
Inatokea kuzungumza kulingana na mada uliyouliza sio from no where... Hata hivyo utamficha vip na anaona kwenye movie na tamthilia??
 
Yap mazingira na nafasi Yako kushirikiana nao kwenye mambo muhimu kama ibada na masomo humo ndo maswali hutokea
 
Kwa jinsi ulivyoandika inaonekana una experience kwenye hili, hongera kwa kuArchive...

Ni kweli ulichoandika mama Yao alishatamka anajua ananipenda ila hawezi kunirudia na mbaya zaidi ananiambia siku hizi anakitembeza balaa na amekua halali kwake akiwaacha watoto wanalala na house girl tuu... Aiseeeeh ni ngumu kurudisha ili kopo naona Bora liende tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…