Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Ni aibu kubwa sana kwa Biden!Sio hata aibu. Sio Taliban iliwaleta Marekani na wenzake Afghanistan - ni al-qaida na mission iko accomplished! Kama al-qaida itaanza tena basi kutakuwa na mtazamo mwingine.
Mkuu, huwa unapata heshima yangu lakini kumlaumu Biden kwa hili hukuangalia vizuri.
a) Trump alifanya makubaliano/mazungumzo na Taliban akiitenga serikali ya Afghanistan. Baada ya hapo Taliban wakafanya mazungumzo butu na serikali. Trump set a wrong tone!!
b) Russia walifanya vita na hata wao waliondoka kama Wamarekani. Hakuna kitu Marekani wangefanya kama wamefundisha wanajeshi na special forces ambazo baadae wana-surrender!! Taliban ni itikadi ya kidini na hivo ina nguvu ya ushawishi kwa raia wengi sana (hakuna urahisi wa kuondoa itikadi hii)!
Marekani ataondoka na itasemwa ameshindwa lakini maana yake ni kuwa angetaka kubaki, angebaki muda mrefu sana!! Biden kachukua uamuzi mgumu sana lakini ukweli ni kuwa hakukuwa na sababu ya kubaki mwaka mmoja zaidi! Kubaki ilimaanisha miongo kadhaa!!
At times pursuing the impossible makes no sense! It can be costly!
Biden huyu huyu na timu yake ndo walisimamia mauaji ya Benghazi! Unabisha?
Marekani haikupaswa kuondoka ilivyoondoka!
Walau wangeondoka kama walivyoondoka kule Vietnam, nchi isingeangukia mikononi mwa Taliban haraka kiasi hiki!
Liko wapi jeshi la watu 300,000 lililoanzishwa na kupewa mafunzo na Marekani?
Ni wapi hilo jeshi limetoa hata resistance ya uongo na kweli?
Biden ndo kaamua kukurupuka kutoka. Biden ndo anawajibika kwa kila linalotokea na kwa kila litalotokea chini ya Taliban kuanzia sasa na kwenda mbele.