Jana kule Mtwara kumefanyika tamasha la wasafi ambalo limeacha historia kwa kufurika watu kwa kiasi ambacho haijapata kutokea watu kujaa namna ile kwenye uwanja wa Nangwanda.
Pia kule wilaya ya Kahama msanii Ali Kiba naye amefanya tamasha ambalo limeacha gumzo kwa kujaa watu.
Kitendo cha watu kujaa kwenye matamasha haya kimeenda kinyume kabisa na CHADEMA ambao wamekuwa wakieneza propaganda kuwa uchumi umeshuka na watu hawana pesa mfukoni.!!
Chadema ,hasa Tundu Lisu wamefikia hatua ya kuichafua nchi kimataifa kuwa eti Tanzania kwa sasa hali ni mbaya kiasi kwamba watu wanashindia mlo mmoja.!
Sasa tuwaulize nyie chadema ,hivi mtu ambaye anashindia mlo mmoja atatoa wapi hela ya kulipia tamasha na kushangilia mwanzo mwisho kama tulivyoona kule Mtwara na Kahama?
Ifike mahali mkubali tu kuwa kasi ya rais Magufuli ni kubwa kuliko uwezo wenu wa kufikiri.