Tambua wakati mzuri wa kutafuta mwanamke wa maisha!

Tambua wakati mzuri wa kutafuta mwanamke wa maisha!

Wanaume hamna maana mtu anakukubalia ukiwa na hali ngumu lakini pindi mkahangaika wote mkapata, mnaanzaga kutafuta anaejua matumizi. Yule wa shida anawekwa pemben kwanza fedha zinatumika na yule aliekuta zipo tayari. Sasa ya nini kuvumilia tabu za m'ume, aiseee ajipange tu kwanza. Na mwanaume usipokuwa vizur una asilimia 80% ya kuchapiwa...
Ok,wewe umeshasaidia wanaume wangapi?kwa hiyo ukiwa tajiri hauwezi kuchapiwa?
 
Sio zama hz aisee, unamkubali mwanaume hana kitu, unamsaport kwa kila hali, hela za nauli za kwenda kwny interview unamtafutia hata kwa kukopa, unamsaidia kutafuta matangazo ya kazi, kuaply, kusaka vibarua huku na huku, lkn akishainuka na kupata ajira na hela basi wewe unaonekana screpa!!! Anaanza kushoboka na wavaa mawigi wanaojua kujichubua na kutumia hela wasizozitafuta!!!! Mwisho wa siku anakubwaga kweupe na kashfa juu ati wewe sio hadhi yangu...wasengerema kweli hawa viumbe.
Huyo wa hivyo hakufaa kuwa wako kabisa. Ila inauma sana kuna watu wanajisahau sana.
 
Ndo hawa mwisho wa siku wanakimbilia kusaka dawa za nguvu za kiume kumbee hana tatizo bali msongo wa mawazo tuu..
Kweli kabisa mkuu, wasijitutumue kwa vitu visivyohitaji kujaribu.
 
kwa hiyo tusubiri tukishafirisika ndio tutafute wachumba?
 
Habari wana jf!

Je ni wakati gani mzuri wa kutafuta mwanamke wa maisha yake kwa mwanaume?

1)je ni wakati ambao mwanaume ana maisha magumu ,hana Ajira,yani kipindi ambacho mwanaume anapambana na hali yake kutoka kwenye dimbwi la umaskini?au!

2)je ni wakati ambao mwanaume ana maisha mazuri,ana ajira nzuri,ameshatoka kwenye Dimbwi la umaskini na mwenye mafanikio ya kiuchumi?

Binafsi naona wakati mzuri wa mwanaume kutafuta mwanamke wa maisha yake,ni wakati ule mwanaume anapokuwa na maisha magumu,kwa sababu Dunia nzima hakuna mtu anaependa maisha magumu na umaskini labda awe chizi,na hapa Duniani kuna uchizi wa aina mbili tu "uchizi wa matatizo ya akili na uchizi wa mapenzi"lakini uchizi wa mapenzi ni mzuri maana huwa ni kiwango cha juu sana cha upendo, kwa mantiki hiyo ukimuona mwanamke amekubali kuishi maisha magumu na mwanaume maskini wakati kuna wanaume wenye maisha mazuri wanahitaji kuwa nae,unatakiwa ujue huyo mwanamke amechizika na mapenzi yani kwa tafsri nyingine "amependa kweli"na wahenga husema "Rafiki wa kweli ni yule akufaae kwa dhiki",ni bahati mbaya sana siku hizi wanaume wengi hutafuta wachumba pindi wanapokuwa wamefanikiwa ndio maana ndoa nyingi siku hizi hazidumu!

Hakika nawaambieni"ukweli ni vigumu kumpata mwanamke anaekupenda kweli ukiwa maskini lakini ni vigumu zaidi kumpata mwanamke anaekupenda kweli ukiwa Tajiri"sasa wewe subiri ufanikiwe ndipo utafute mchumba wa kuoa halafu uone mara ume filisika baada ya kuoa,hapo ndipo utakapojua kuwa kuna wanawake wenye Destiny ya umaskini,kwa sababu wanajua kutumia tu pesa hawajui kuzalisha na hawana upendo wa kweli!


Huu ni mtizamo wangu sio sheria,toa na wewe mtizamo wako!
kweli kabisa, kwa sababu hutajua kama anakupenda mama lah
 
Back
Top Bottom