TAMISEMI hili suala la vifaa vya ujenzi wa madarasa kununuliwa na Halmashauri wakati pesa zimeingizwa kwenye account za shule tupieni jicho

TAMISEMI hili suala la vifaa vya ujenzi wa madarasa kununuliwa na Halmashauri wakati pesa zimeingizwa kwenye account za shule tupieni jicho

Ndiyo, lakini force account majengo yanakuwa chini ya kiwango maana mnachukua local fundi wa mitaani tupu mnagawana nayo pesa
Kwa jibu hili unaonesha hujui chochote kuhusu force account ila unajifanya kujua
 
Mimi Sikubaliani na hii force account kwa vitu vinavyohitaji ubora wa hali ya juu. Huwezi jenga darasa litakaloishi miaka mitano no. Tumesoma shule zilizojengwa miaka ya 1924,1935 etc na majengo yamesimama. Huu ujenzi wa force account hauwezi kutoa ubora unaohitajika hili moja. Sijui mkopo huu hauhitaji kufuatilia ubora/quality and proper design and supervision? sijui kwa kweli.
 
Kuna Halmashauri nyingi hapa nchini zimetoa maelekezo kwamba vifaa vya ujenzi watanunua wao wakati huo pesa imeingizwa kwenye accounts za shule, TAMISEMI kama mmetoa maelekezo haya basi wekeni utaratibu mzuri kabisa ili wasije wakazidisha bei ya vifaa maana halmashaur zetu huko kuna shida sana na matokeo yake pesa isitoshe, maana kuna dalili za wizi hapa na tuhuma zitaelekezwa kwa walimu wakuu.

Kuna kipindi ujenzi huuhuu kuna halmashauri zilitumia njia hii matokeo yake baadhi ya shule wakajikuta wanapelekewa malipo ya saruji Tsh 18,500/ kwa mfuko wakati bei ya sokoni kwa mfuko ni Tsh 15,500/ na mifuko bado haikutosha na pesa zimeisha na ujenzi ukakwama.

Kama TAMISEMI mmeliweka katika utaratibu huu ambao ukifanyika kwa uzalendo kabisa ni mzuri sana ila tu usimamizi uwe wenye umakini ili kuepusha wizi wa kuongeza gharama na kusababisha pesa kuto tosha.
Huku tuliko hali hiyohiyo lakini sababu wanazotoa ni kupunguza gharama kwani vifaa hivyo vitanunuliwa moja kwa moja viwandani na bei kuwa chini labda na gharama za usafirishaji tuu
 
Huku tuliko hali hiyohiyo lakini sababu wanazotoa ni kupunguza gharama kwani vifaa hivyo vitanunuliwa moja kwa moja viwandani na bei kuwa chini labda na gharama za usafirishaji tuu
Kama kama wakitumia utaratibu ambao utazuia urasimu na wizi ni mfumo mzuri cha msingi walete bei zilizopo sokoni wakifanya hivyo sioni shida
 
Fedha zimeingia katika akaunti ya Shule, Mkuu wa Shule ndiye wa kwanza kuwajibika. Mkurugenzi au halmashauri ana sehemu yake ya kuwajibika
1. Fedha hizo haziwezi toka bila idhini ya mkurugenzi
2. Wahandisi, wahasibu, maafisa manunuzi, na nyaraka zote Muhimu zinatoka halmashauri.
3. N.k
 
Tamisemi imezidiwa na majukumu na wizara nyingine baadhi inaonekana zinaitegemea tamisemi Kwa kila kitu halafu zinabaki kutunga Sera Tu na kusinamia vitu vichache.
1. Kwanini Elimu isirudi wizara ya Elimu?
2. Afya irudi wizara ya Afya?
3. Kilimo kirudi wizara ya kilimo?
n.k

Tamisemi na Halmashauri zibaki na jukumu pekee la kiutawala???
Kwa sababu asilimia kubwa ya majukumu mazito ya kiutendaji yanayofanywa na Halmashauri ni ya wizara nyingine.

4. Kwanini Shule za msingi na sekondari zipo tamisemi na vyuo vikuu na vingine vipo wizara ya Elimu? Linganisha ufanisi katika utendaji kazi wake.

5. Kwanini tanroads wapo wizara ya ujenzi na tarura wapo tamisemi?? Linganisha ubora wa Kazi zao.

6. Kwanini zahanati, vituo vya afya vipo tamisemi na hospital za mikoa, rufaa zipo wizara ya Afya???. Linganisha ufanisi katika utendaji kazi.

7. N.k

Serikali iliangalie hili
 
Shuleni kuna maafisa manunuzi?
Mbona vitabu wananunua wao? Hapo ni wizi ndo uliolengwa. Nani hasiyejua mchwa waliojaaa kwenye halmashauri zetu?

Madai ya mbuzi kununuliwa laki 5 na halmashauri ni kitu cha kawaida,kalamu ya bick kununuliwa 1000,vipi kuhusu fungu la mchicha kununuliwa 30,000? Usisahau Kuna halmashauri iliwahi kuagiza mabati Uganda. Haya ni baadhi ya mambo yaliyowahi kuibuliwa na PAC,madudu ya kutosha ni wezi wasio na aibu.
 
PAC wenyewe wakifika halmshauri huwa wanataka mzigo tena hakuna watu wabaya kama hao mkuu
 
10% kwa mtu asiye mzalendo ni chanzo cha tatizo na nina dhani miongoni mwa sababu ni hii ingawa likisimamiwa vizuri ni jambo linalo punguza sana usumbufu wa upatikanaji wa rasilimali
Mzalendo ni mtu mwenye sifa zipi? Naomba unipe elimu
 
Tamisemi imezidiwa na majukumu na wizara nyingine baadhi inaonekana zinaitegemea tamisemi Kwa kila kitu halafu zinabaki kutunga Sera Tu na kusinamia vitu vichache.
1. Kwanini Elimu isirudi wizara ya Elimu?
2. Afya irudi wizara ya Afya?
3. Kilimo kirudi wizara ya kilimo?
n.k

Tamisemi na Halmashauri zibaki na jukumu pekee la kiutawala???
Kwa sababu asilimia kubwa ya majukumu mazito ya kiutendaji yanayofanywa na Halmashauri ni ya wizara nyingine.

4. Kwanini Shule za msingi na sekondari zipo tamisemi na vyuo vikuu na vingine vipo wizara ya Elimu? Linganisha ufanisi katika utendaji kazi wake.

5. Kwanini tanroads wapo wizara ya ujenzi na tarura wapo tamisemi?? Linganisha ubora wa Kazi zao.

6. Kwanini zahanati, vituo vya afya vipo tamisemi na hospital za mikoa, rufaa zipo wizara ya Afya???. Linganisha ufanisi katika utendaji kazi.

7. N.k

Serikali iliangalie hili
Hapa kuna tatizo la kimuundo wa utawala, hili lilianzia tangu kwenye ugatuaji wa madaka kupeleka mikoani kutoka kwenye centralised socialistic nature. Huku kunatokana pia na uoga wa central government kuogopa kuunda kitu kikubwa kitakachoweza kuchallenge weledi wake. Kwa hiyo power zimeachiwa kimagumashigumashi tu. Na wala sio halmashauri haziwezi kufanya kazi kama watu wengi wanavyosema ni zaidi ya hapo. Dawa ni kuzipa mikoa/majimbo power through wananchi wachague viongozi wa majimbo yao na waunde serikali zao za majimbo waajiri na kukaribisha compitent staff wakiwa na power ya kuajiri na kufukuza. Centra Gov inakumbatia power zote na kubuni mbinu jaribishi hambazo mara nyingi zinaishia kushidwa na kuota blames kwa halmashauri. Halmashauri zimenyanganywa mapato yote na kupelekwa central Gov. na kipewa na kijiko cha chai na blames kibao pamoja na mipango mipya mara force account mara hili mara lile. Tuwaachie wananchi madaraka ya kuamua uongozi wanao wapenda kuanzia Governors to Municipal directors etc. Wananchi sio wajinga kiasi hiki wanauwezo wa kuwawajibisha viongozi wabovu.
 
Mkuu babati sio kila anaecomment au kupost katika uzi huu ni Teacher na hata kama ni Teacher siendeshwi na masrahi binafisi bali naendeshwa na masrahi ya Umma na nchi yetu kwa ujumla.Issue hapa ni kuwa halmashauri itafanyaje manunuzi ya vifaa kwa kutumia fedha ambazo ziko kwenye account za shule au hospitali?.
Sisi tunaopaza sauti tunawasaidia walimu wasio na SAUTI.
Maslahi
 
Anayekaguliwa si DED mkuu? Head teacher anauelewa wa manunuzi au ujenzi pamoja na masuala ya fedha?
Fedha ikiingia kwenye account ya shule anayekaguliwa ni mkuu was shule .Anayefanya mchakato was matumizi mpaka kupata bidhaa ndiye anajibu hoja.
 
Shuleni kuna maafisa manunuzi?
Maafisa manunuzi ni Wala ten percent ndiyo maana wanang'ang'ania waendelee kuwanunulia wanavijiji mahitaji yao ya ujenzi urasimu mwingine ni kujitia hasara tu,rip JPM
 
Back
Top Bottom