TAMISEMI: Mwanafunzi Josephat John aliyevaa mabango hakuchaguliwa ECA na hakuwa na sifa za kuchaguliwa PCB

TAMISEMI: Mwanafunzi Josephat John aliyevaa mabango hakuchaguliwa ECA na hakuwa na sifa za kuchaguliwa PCB

Kama wame-edit watajua wenyewe. Ila dogo mwache aende Songea huko kwa Wayao.

Chuo kizuri sana kile. Mazingira safi, maisha cheap.

IMG_20210605_160447.jpg
 
Mwanafunzi Josephat John hakuchaguliwa ECA na hakuwa na sifa za kuchaguliwa PCB

OR-TAMISEMI,DODOMA

Mwanafunzi Josephat John aliyekuwa anasoma kidato cha nne shule ya Sekondari Kom iliyopo kwenye Manispaa ya Shinyanga alizua taharuki baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya biashara (ECA) ambayo anadai hajawahi kusomea kwani yeye amesoma masomo ya Sayansi(PCB)

Mwanafunzi huyu amepata Div II:21 na masomo ya sayansi anayodai amesomea amepata DCC yenye jumla ya pointi 10. Mwisho wa pointi za wanafunzi waliopangiwa Tahasusi hii ni 8 sawa na BCC, hivyo mwanafunzi huyu hajakidhi vigezo vya kuchaguliwa katika Tahasusi hii ya PCB kulingana na idadi ya nafasi zilizopo mwaka huu.

Hata hivyo Mwanafunzi huyu hajapangiwa Tahasusi ya Biashara (ECA) kama anavyodai, bali amepangiwa kusoma Stashahada Maalumu ya Ualimu kwa Masomo ya Physicis na Hesabu katika chuo cha Ualimu Songea ambapo ni miongoni mwa Maeneo aliyochagua katika machaguo ya vyuo alianza na Ufundi, Afya kisha Elimu.

OR TAMISEMI inaendelea kumtafuta mwanafunzi huyu ili iweze kufahamu nia na shida ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia kufanya kitendo hiki.

OR TAMISEMI inaendelea kusisitiza kama kuna mzazi au mlezi yoyote anahitaji ufafanuzi wowote awasiliane na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 0735-160201 na 0262-160201 kuandika barua pepe kwenye anwani yetu . huduma@tamisemi.go.tz

PIA SOMA
- Mwanafunzi avaa mabango na kukaa barabarani akipinga kuchaguliwa masomo ya ECA ambayo hajayasomea
Hivi wanavyotaka watu watumie barua pepe huwa wapo serious au ni kuepusha usumbufu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dogo muongo sana hajafaulu alafu anataka alete janjajanja huyu mtoto no yake ya mtihani ni S2652-0102-2020 utaona matokeo yake,pia ukienda kwenye selection kachakuliwa ualimu sasa sijui nia yake yakufanya hivyo labda nikuichafua serekali au alikua na mategemeo yakwenda A level ,japo naona ana tahasusi moja ilio balance HKL ana CCC
 
Dogo na CCD yake anataka kupiga PCB aje kuwa Pharmacist,Doctor n.k..hataki chaki.
Mkuu,hata angekubaliwa ufaulu wake kwenye hiyo combination akaze msuli DCC sio poa kabisaaa.
 
Huyu bado ni mtoto atafutwe aelekezwe pia asaidiwe kufikia malengo yake sio kwamba Hana akili ni hiyo D moja Tu imeharibu na Kwa mazingira ya huko Kom huwezi linganisha na Mijini. Yupi ana nafuu anaelilia kusoma PCB au anaevuta bangi?.
 
Hiyo PCB anayodai amefaulu, siku hizi inafundishwa O-Level?
Fikiria upya ulichoandika,ujiridhishe km uko sahihi na dogo hajui anachopigania,kwamba alifaulu masomo yanayounda combination ya PCB kwa ajili ya kujiunga kidato cha tano.

Kwamba O-level hawasomi physics,chemistry na biology? Yanayounda combination ya PCB kwa advance level.
 
20a1a3bc-8d1c-4594-a551-bf77c7346fc7.jpg
 

Attachments

  • 850013e8-9b03-48e3-b814-77091d7750b3.jpg
    850013e8-9b03-48e3-b814-77091d7750b3.jpg
    86.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom