TAMISEMI: Mwanafunzi Josephat John aliyevaa mabango hakuchaguliwa ECA na hakuwa na sifa za kuchaguliwa PCB

Walimu msikomae na mapindi tu kila siku, pia washaurini hawa madogo kuhusu maisha n.k .. Haya maisha unatakiwa kuflow kama maji ukikuta jiwe mbele unapita pembeni ili maisha yaendelee, Otherwise tutakuja kupeteza maisha ya watu kizembe.
 
Div II 21pts anaenda kusomea stashahada ya ualimu? Kweli miaka inasonga sana.
 
Duh noma sana, au wamembadilishia maks juu kwa juu ili kumkomoa, nashauri iundwe tume huru
Mimi pia nawaza hivi...

Sidhani kama huyu mwanafunzi hakuona kama kachaguliwa Ualimu.

Tamisemi baada ya kusikia yale maandamano najua waliangalia na kama walikosea ndio wakabadili gia angani ili waweza kuficha aibu na kumjibu huyu muandamanaji
 
Dogo angejua maisha ni biashara asingeibeza ECA.
Wanakuwa hawana washauri, wanafuata ambition zao tu......hata mimi mwalimu wetu wa book-keeping alikuwa anatubeza kukazania na kufaulu masomo ya sayansi wakati masomo ya biashara ndo yenye kazi zenye mpunga mrefu, hatukumwelewa sasa hizi tunatumia akili mingi mshahara mbuzi......wakati usawa huu ningepiga ECA ungekuta kwa sasa ningekuwa Managing Director wa kampuni kubwa unalamba si chini ya 40m. per month.
 
Mwanafunzi Josephat John hakuchaguliwa ECA na hakuwa na sifa za kuchaguliwa PCB

OR-TAMISEMI,DODOMA

Mwanafunzi Josephat John aliyekuwa anasoma kidato cha nne shule ya Sekondari Kom iliyopo kwenye Manispaa ya Shinyanga alizua taharuki baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya biashara (ECA) ambayo anadai hajawahi kusomea kwani yeye amesoma masomo ya Sayansi(PCB)

Mwanafunzi huyu amepata Div II:21 na masomo ya sayansi anayodai amesomea amepata DCC yenye jumla ya pointi 10. Mwisho wa pointi za wanafunzi waliopangiwa Tahasusi hii ni 8 sawa na BCC, hivyo mwanafunzi huyu hajakidhi vigezo vya kuchaguliwa katika Tahasusi hii ya PCB kulingana na idadi ya nafasi zilizopo mwaka huu.

Hata hivyo Mwanafunzi huyu hajapangiwa Tahasusi ya Biashara (ECA) kama anavyodai, bali amepangiwa kusoma Stashahada Maalumu ya Ualimu kwa Masomo ya Physicis na Hesabu katika chuo cha Ualimu Songea ambapo ni miongoni mwa Maeneo aliyochagua katika machaguo ya vyuo alianza na Ufundi, Afya kisha Elimu.

OR TAMISEMI inaendelea kumtafuta mwanafunzi huyu ili iweze kufahamu nia na shida ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia kufanya kitendo hiki.

OR TAMISEMI inaendelea kusisitiza kama kuna mzazi au mlezi yoyote anahitaji ufafanuzi wowote awasiliane na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 0735-160201 na 0262-160201 kuandika barua pepe kwenye anwani yetu . huduma@tamisemi.go.tz

PIA SOMA
- Mwanafunzi avaa mabango na kukaa barabarani akipinga kuchaguliwa masomo ya ECA ambayo hajayasomea
"OR TAMISEMI inaendelea kumtafuta mwanafunzi huyu ili iweze kufahamu nia na shida ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia kufanya kitendo hiki".

Hapa itakuwa kuna jambo.
Kwa nini OR TAMISEMI itoe ufafanuzi kabla hata hawajajua tatizo la huyo dogo?
 
Mwanafunzi Josephat John hakuchaguliwa ECA na hakuwa na sifa za kuchaguliwa PCB

OR-TAMISEMI,DODOMA

Mwanafunzi Josephat John aliyekuwa anasoma kidato cha nne shule ya Sekondari Kom iliyopo kwenye Manispaa ya Shinyanga alizua taharuki baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya biashara (ECA) ambayo anadai hajawahi kusomea kwani yeye amesoma masomo ya Sayansi(PCB)

Mwanafunzi huyu amepata Div II:21 na masomo ya sayansi anayodai amesomea amepata DCC yenye jumla ya pointi 10. Mwisho wa pointi za wanafunzi waliopangiwa Tahasusi hii ni 8 sawa na BCC, hivyo mwanafunzi huyu hajakidhi vigezo vya kuchaguliwa katika Tahasusi hii ya PCB kulingana na idadi ya nafasi zilizopo mwaka huu.

Hata hivyo Mwanafunzi huyu hajapangiwa Tahasusi ya Biashara (ECA) kama anavyodai, bali amepangiwa kusoma Stashahada Maalumu ya Ualimu kwa Masomo ya Physicis na Hesabu katika chuo cha Ualimu Songea ambapo ni miongoni mwa Maeneo aliyochagua katika machaguo ya vyuo alianza na Ufundi, Afya kisha Elimu.

OR TAMISEMI inaendelea kumtafuta mwanafunzi huyu ili iweze kufahamu nia na shida ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia kufanya kitendo hiki.

OR TAMISEMI inaendelea kusisitiza kama kuna mzazi au mlezi yoyote anahitaji ufafanuzi wowote awasiliane na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 0735-160201 na 0262-160201 kuandika barua pepe kwenye anwani yetu . huduma@tamisemi.go.tz

PIA SOMA
- Mwanafunzi avaa mabango na kukaa barabarani akipinga kuchaguliwa masomo ya ECA ambayo hajayasomea
Duuh mapya haya!
 
Wanakuwa hawana washauri, wanafuata ambition zao tu......hata mimi mwalimu wetu wa book-keeping alikuwa anatubeza kukazania na kufaulu masomo ya sayansi wakati masomo ya biashara ndo yenye kazi zenye mpunga mrefu, hatukumwelewa sasa hizi tunatumia akili mingi mshahara mbuzi......wakati usawa huu ningepiga ECA ungekuta kwa sasa ningekuwa Managing Director wa kampuni kubwa unalamba si chini ya 40m. per month.
Una elimu gan?
 
Tanzania ni moja ya nchi zinazopuuza elimu!! Nchi nyingi sasa hivi mwalimu wa shule ya msingi ana shahada ya ualimu!!

Shule ya msingi ni muhimu sana lakini mwalimu wake ni yule ambaye hata kidato cha 5 hakuiingia. Tuna shida!!!
 
Matokeo yake yawekwe hapa tujue kama mwanafunzi au TAMISEMI ndo wanasema ukweli
6CF75CD9-9946-4815-8282-3F02CD7D33B6.jpeg
 
Back
Top Bottom