TAMISEMI: Mwanafunzi Josephat John aliyevaa mabango hakuchaguliwa ECA na hakuwa na sifa za kuchaguliwa PCB

Hakuna media yeyote iliyofanya nae interview? Tumsikilize na yeye. Maana hapo hapaeleweki.
 

Una uhakika hujachanganyikiwa? PCB ni tahasusi ya A-Level, huko chini mnasoma masomo yote.... kwanini adai alifaulu PCB!

Well, inawezekana alitamani kusoma tahasusi hiyo na alichagua apangiwe ikiwa atafaulu... lakini je alifaulu masomo hayo kuliko mengine? Anachagulia kwa hisia zake!

Kwa upande wako unayemuunga mkono, mshauri aende shule binafsi zipo kibao... atasoma akipendacho.

This is... another bullshit.
 
Ok.. Good Clearance.
 
Hapo kuna namna wamefnya hawa watu ni wahuni kupindukia pia hayo mawasiliano wanayosema wanatoa ni waongo mara nyingi ukiwapigia hupati msaada wowote unasubirishwa mpka simu inakata yenyewe.....
Badala ya kupeleka lawama TAMISEMI, ni vema mngejiridhisha na majibu yaliyotolewa na TAMISEMI, kwani huyo jamaa hayajui matokeo yake ya kidato cha nne? Tamisemi inaweza kubadili matokeo ya NECTA? Tuwe na hoja zenye mashiko tunapokuja jf
 
AMISEMI inaendelea kumtafuta mwanafunzi huyu ili iweze kufahamu nia na shida ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia kufanya kitendo hiki.
 
Tanzania ni moja ya nchi zinazopuuza elimu!! Nchi nyingi sasa hivi mwalimu wa shule ya msingi ana shahada ya ualimu!!

Shule ya msingi ni muhimu sana lakini mwalimu wake ni yule ambaye hata kidato cha 5 hakuiingia. Tuna shida!!!
Acha ukosoaji mkuu. Unataka kusema kumpa mtoto elimu ya msingi inahitaji mtu awe na shahada hii ya makaratasi ndio atoe elimu bora?

Ualimu hasa wa msingi ni wito. Leo hii madaktari, wahandisi, wahasibu na wanasiasa wanajivunia elimu ya msingi waliyoipata kwa walimu wenye cheti.

Ualimu wa msingi ni masomo ya kawaida, saikolojia na malezi kwa watoto. Walimu tunalijua hilo
 
Washamponza Dogo... Ila hata kama ni kweli itakua wamebadilisha haraka haraka...
 
Tanzania ni moja ya nchi zinazopuuza elimu!! Nchi nyingi sasa hivi mwalimu wa shule ya msingi ana shahada ya ualimu!!

Shule ya msingi ni muhimu sana lakini mwalimu wake ni yule ambaye hata kidato cha 5 hakuiingia. Tuna shida!!!
Wailokuwa na degree za primary education huwa wanadakwa na International schools. Hata hivyo dogo aambiwe kwamba anaweza kujiendeleza mpaka hata phD ikiwa anayo nia hiyo. Akimaliza diploma aende degree halafu Masters na phD
 
Kweli kabisa ualimu ni wito na mbinu za kuwahamasisha watoto jinsi ya kupenda kusoma na kuweza kuandika na kufanya michanganuo. Sisi wengine wa miaka ile ya nyuma tulifundishwa na walimu wa darasa la nane, na mpaka leo tunawakumbuka jinsi walivyohangaika kutuwezesha kukamata kalamu na kuandika mwandiko mzuri.

Mwenyezi Mungu awarehemu walimu wangu wa msingi waliokwisha fariki.
 
Wewe Ni msengerema fulani ivi ambaye huna lolote kichwani. Hiyo PCB ya A level utaipataje km O level hujasoma physics, chemistry and biology.

Tatizo vijana wa siku hizi uwezo wa kureason kihesabu ni mdogo sana.

Halafu hoja yangu haikuwa ty kufaulu au la ktk hayo masomo,hoja yangu ni we kudai hakuna PCB o level ukasahau PCB Ni physics,chemistry and biology.Ni suala la kufikiri kikomavu tu.

Ulienda shule kukariri ujinga,Mpumbavu flani ww, nimekupuuza!! Kwanza ni kosa sana kuargue na vitoto vilivyofeli form 4.
 
Ualimu si wito! Ila ni wito kwa shule zenye malengo madogo.wasio na dira ya mafanikio makubwa ktk taasis zao.

Ualimu ni kazi kwa shule na taasisi zenye malengo makubwa. Watu siriaz.
 
 
Shukrani kwa ufafanuzi,
 
Kuna shida moja inajitokeza hapo, walimu wa shule husika wanabadilisha hizo combination wanapojaza kwenye mfumo ili kuwezesha shule zao kupeleka wanafunzi wengi kidato Cha nne, kwahiyo huwajazia combinations ambazo possibility ya kufaulu ni kubwa na hii inaweza kuwa tofauti na chaguzi la mwanafunzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…