TAMISEMI njooni muondoe wezi Tanga Jiji na Mkinga

TAMISEMI njooni muondoe wezi Tanga Jiji na Mkinga

Ningekushauri umwandikie rasmi Boss wake ili awatume watendaji wake kuja kufanya uchunguzi, ukiweka open hivi hapa inakuwa kama majungu
Niushauri mzuri lakini hata mitandao ya kijamii ni njia sahihi pia ya kupaza sauti zetu

Asante mkuu kwa muda na ushauri wako kwenye uzi huu
 
Niushauri mzuri lakini hata mitandao ya kijamii ni njia sahihi pia ya kupaza sauti zetu

Asante mkuu kwa muda na ushauri wako kwenye uzi huu
Upo sahihi kuandika hapa hujakosea ila unge muaddress kiongozi husika, kama ni waziri wake, katibu Mkuu wake, au hata RC wake...

Kama alivyoandika huyu ndugu hapa


Japo nayeye hajatumia polite request
 
Waliopo ofisi zote za TSC Mkinga na Tanga msikubali mtakapoambiwa muwe masignatori mpaka hao wezi wafanyiwe ukaguzi.
Wameiba sana na wakurugenzi hawawabani kwasababu nao ndio vile tena
 
Kwasababu maafisaelimu baadhi hawajielewi.
Wanaendekezatu ngono na wanajificha kwenye mgongo wa ukada.
Wakurugenzi wao ndio deshi kabisa
Tatizo lipo kwenye mfumo wa kuwapata hao maafisa.Wengi walihonga kupata hizo nafasi,miaka hiyo.Kwahiyo hawana weledi wa kufanya kazi zaidi ya figisu zisizo na nyuma wala mbele.
Poleni Nkinga
 
Elimu inachezewa mno.Hapo kuna kufaulisha kwel?
 
Ila waalimu bwana sijui nani aliwaroga.

Hivi kwanini hamtaki kujikubali kuwa nyinyi ni jeshi kubwa sana? Mnajua mkiungana mnaweza amua chochote na Serekali itatekeleza? Mnajua hicho kitu? Mnashindwa na jeshi la boda boda yaani
 
Mbona umetumia muda mwingi kuwapiga tu vijembe huyo Afisa Elimu na huyo Katibu wa TSC? Badala yakuelezea sababu hasa ya wewe kufukuzwa kazi?

Na kamaa umeonewa, mbona una haki ya kukata rufaa kwenye ngazi za juu za kiutumishi! Sasa kuja kulia lia humu ndiyo itakusaidia kurudishwa kazini?

Ulitakiwa uelezee ukweli wa kilichotokea, na pia kuomba ushauri wa kisheria ili usaidiwe. Badala ya kutoa shutuma zisizo na ushahidi.
 
Kwanza TSC ipo chini ya Mkurugenzi?wanawajibika kwa Mkurugenzi?kuwa kwenye jengo la Mkurugenzi hainamaana wako chini yake.Hawo pamoja na udhibit ubora hawawajibik moja kwa moja kwa Mkurugenz,Wanawajibika kwa Katibu mkuu
 
Mkurugenzi wa jiji la TANGA ndio wakuanza nae,pamoja na yule afisa elimu waliemtoroshea korogwe mji
 
Majungu at fleek.[emoji855]
Maofisini Kuna majungu sana
 
Tatizo lipo kwenye mfumo wa kuwapata hao maafisa.Wengi walihonga kupata hizo nafasi,miaka hiyo.Kwahiyo hawana weledi wa kufanya kazi zaidi ya figisu zisizo na nyuma wala mbele.
Poleni Nkinga
Kombo hamna kitu anajichekeshatu
 
Mkurugenzi wa jiji la TANGA ndio wakuanza nae,pamoja na yule afisa elimu waliemtoroshea korogwe mji
Nasikia mkurugenzi wa Jiji la Tanga anaogopeka maana anaundugu na Magufuli.
Anajikadiria anachotaka na haguswi. Akisema hamtaki mtumishi kwenye halmashauri yake imepita hiyoooo

Huyo Afisaelimu aliyehamishiwa korogwe simjui mkuu
 
Ninawasalimu wanajukwaa wa JF

Wakati Mh.Rais akitembea na kauli mbiu ya kazi iendelee,wapo manaibu makatibu wawili wa Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC) wa wilaya za Tanga Jiji na Mkinga Halmashauri kauli yao itakua wizi unaendelea. Wanafanya wizi wa dhahiri,unyanyasaji,uonevu na ukandamizaji wa haki za walimu.

Manaibu Makatibu hao Naima Twalib wa Tanga Jiji na Thomas Mnkande wa Mkinga Halmashauri wamegeuza ofisi kua pango la kupigia fedha za umma. Makatibu hao wote wawili kwa nia ovu kabisa wamekua hawawashirikishi wasaidizi wao katika masuala yakiofisi ikiwemo kushuhulikia kero za watumishi ndani ya Halmashauri zao.

Badala yake wanapokea maelekezo kutoka kwa wakurugenzi na maafisa elimu ili kuwakandamiza walimu. Ofisi hizo zimegeuka kama wapo chini ya wakurugenzi na maafisaelimu. Hata kesi za kinidhamu hawawashirikishi watumishi kwenye ofisi zao bali wanashuhulikia mashauri ya walimu kwa matakwa ya wakurugenzi. TSC Tanga na Mkinga sio watetezi wa walimu bali niwapiga dili kupitia Naima na Mnkande

Wanaminya haki za watumishi wenzao ndani ya ofisi kwakiburi na dharau eti kwasababu wao niwakongwe hawataguswa na mtu yeyote. Pia wanajisifu kwamba wana watu wao TSC Makao Makuu Dodoma na Ummy Mwalimu nae eti ni wanammudu.Hiyo ni aina ya rushwa serikali liangalieni

KUBWA KULIKO ZOTE NI WATUMISHI HAO KUSAINIANA ILI WATOE FEDHA ZA OFISI. Ukweli ni kwamba naibu katibu wa Tanga Jiji amekua ndio signatory wa TSC Mkinga na yule wa TSC Mkinga amekua signatory wa Tanga Jiji tena kwa muda mrefu sasa.Huu ni wizi wa dhahiri na mamlaka zimewafumbia macho.

Manaibu makatibu hao wameota pembe zaidi maana hata TSC Makao Makuu wameshapewa taarifa za uvunjaji huo wa taratibu za fedha lakini hawachukui hatua. Inaonekana KUNA MGAO WANAPELEKA MAKAO MAKUU NDIO MAANA WANALINDWA. Hii inadhihirika pale watumishi wa ofisi za TSC Tanga na Mkinga wakilalamika kwa mamlaka zao Dodoma hakuna hatua zozote.

Wakaguzi wa ndani hawajaona huu uvunjifu wa sheria ndani ya hizi halmashauri? Wakurugenzi hawajaona huu wizi? Au kwakua wanabebana wanapopeana maelekezo. Inakuaje mtu atoke Tanga Jiji akasaini Mkinga na mwingine atoke Mkinga Halmashauri akasaini Tanga ikiwa ofisi zote zina watumishi wenye vigezo vya kufanya mambo hayo?Wizitu na kufanya kazi kimapenzi na kwamazoea kwa wazee hawa vikomeshwe.

Wanatembeza mgao na kupiga sana tunguli ndio maana hawaguswi. Kutwa kucha wanapigiana simu za kujadili waganga wazuri walipo ili waendelee kushikilia ofisi. Wala hawajali maslahi ya watumishi sanasana wanaibatu hela za serikali.

Waziri Ummy awashuhulikie hawa wazee wanaofanya kazi kimapenzi na kwamazoea waondoke ofisini waletwe viongozi wanao wajali na kuwasikiliza watumishi na sio hawa wazee wawili ambao wapotu kwaajili ya kupokea maelekezo kutoka kwa wakurugenzi na maafisaelimu kwa lengo la kukandamiza watumishi.

Ummy usiwalinde hawa tunakuamini wewe ni mchapakazi kama ulivyofanya kwa wale wakurugenzi wa halmashauri hawa nao wasimamishe wapishe uchunguzi. Niwezi wa mchana kweupe tena wezi wazee ukiwaona wanatia huruma lakini niwezi sana.

Mh. Ummy lifanyie kazi. Katibu mkuu Tamisemi na Utumishi sikieni kilio cha walimu wa Tanga na Mkinga
Hii mambo haijakaa sawa sana. Mmlaka za kidhamu za watumishi hawa wa TSC zilifanyie kazi hili suala. Maana, bila kujali wanahusika ama hawahusiki, viongozi wa TSC HQ wamechafuliwa sana.

Na hiki in tatizo sio tu LA Mkinga na Tanga mjini, ni almost wilaya karibia zote malalamiko kama haya yanasikika.
 
"Hata kesi za kinidhamu hawawashirikishi watumishi kwenye ofisi zao"

Makatibu wasaidizi wa TSC Wilaya, wamewafanya watuhumiwa wa kinidham kuwa saccos. Tena wanakutana na watuhumiwa majumbani, sehemu zenye starehe n.k.

Lkn pia, taarifa za kimanunuzi so za kweli hata kidogo. Wananunua risit za kielektroniki tu basi, hawanunui stationeries, wino n.k. kula pesa za wajumbe na viposho vya watumishi wenzao ndo kazi waliobaki nayo.


TSC HQ fuatilieni. Kinyuma chake mtaonekana mnashirikiana na hawa makatibu walafi wa fedha za Umma.
Pitieni huko mawilayani mtayasikia mengi.
 
Kwanza nimeshangaa sana huyo Omari Kombo eti ni afisaelimu sekondari wa Halmashauri.Huyo bwana miaka ya 1988 kuendelea alikuwa mwalimu hapo Maramba sekondari wakati huo nikiwa mwanafunzi.Alikuwa ni mbabaishaji sana katika kufundisha na huku akifanya biashara ya kupiga picha pale shuleni.Kweli kupata cheo TZ ni kuwa na connection na siyo utendaji wa mtu, ndiyo maana nchi inaendelea kwa kuchechemea.
 
Back
Top Bottom