TAMISEMI ongezeni muda wa kutuma maombi ya ualimu na afya

TAMISEMI ongezeni muda wa kutuma maombi ya ualimu na afya

Duuh, kweli wewe ni Sayansi piwa, umecharanga mwandiko wa kitabibu.

Hebu fikiria hili.

1.Kuna mtu hadi sasa hana hata namba ya nida.

2.Kuchukulia poa, mambo ya msingi.

3.Kuna mtu hapo unamtetea, lakini alipewa hela yote ya kupata vyeti au leseni na asifanye yanayohitajika

4.Zimamoto.

5.Serikali inajua watu wanavyo vyeti, lakini hiyo ni njia pia ya kupunguza jam, kazi chache ila watu wengi.
Nimependa point namba 5🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wa TZ wanapenda deadline.Mtu amemaliza chuo mwaka juzi mpaka sasa hajachukua cheti chake.

Mimi nafikiri muda usiongezwe kwani hii ni njia ya kupunguza watu.🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Isshue ya Leseni imeletwa juzi. Haikuwepo. Shida sio kujua shida no urasimu wa upatikanaji
Acha mambo yako wewe leseni zipo muda sana na kupata leseni hakuna urasimu wowote. Shida sisi watanzania tunapenda sana kulialia kuonewa huruma, chuo umemaliza miaka 2, 3 nyuma kwanini usifatilie leseni na vyeti vyako mapema?

Kupata transcript nacte sio lazima uende headquarter zipo ofisi za nacte kila kanda Arusha, mwanza, mbeya, tabora, mtwara, dodoma kwanini uende headquarter?

Vijana badilikeni siku 20 zilizotolewa ni nyingi sana acheni mambo ya zimamoto unatakiwa kuwa tayari muda wowote kama mwanajeshi.
 
Wewe kama hukuandaa vitu vyako mapema usiandike ujinga humu,
Kwanza kupata Nacte transcript haichukui hata week tatu wewe useme ukweli umeanza kushugulikia vitu baada ya ajira kutangazwa
Hauko serious na mambo yako

Utajijua
Wiki 3 ni nyingi sana sasa hivi siku 5 tu transcript inakuwa collected
 
Niongeze maoni.

Kuhusu idara ya afya kitengo cha USTAWI WA JAMII mwaka jana walitoa nafasi zisizo zidi 50 kati ya nafasi za afya zote maelfu.

Wanao omba hiyo ustawi unaweza kukuta ni wengi sana zaidi ya mamia lakini wanachukuwa watu 40+

Kingine ni mwaka!!! KUMBE KWENYE AFYA HUKU hawaangalii mwaka wa kuhitimu ???


Kuna watu wamechukuliwa wa mwaka 2006,7,8,9,10 wa mwaka 2015 kuendelea wapo 3

Hii ipoje [emoji115]

Kwa mjibu wa nafasi za mwaka jana 2022.

Vipi mwaka huu?
 
Sababu ambazo umeandika ni dhaifu sana mkuu. nijuavyo Mimi sababu ambazo ninaweza kuongezwa muda kutuma maombi ni;
1. Tatizo la mtandao au mfumo wao kuwa changamoto.
2. Marekebisho ya tangazo baada kutolewa mara yakwanza then wakafanya marekebisho ya tangazo.
 
Umesema kitu kizuri sana hila tambua hata wakisema deadline iwe mwezi wa 12 bado kuna watu watakuja kuomba mdah wa nyongeza wakamilishe maombi watakuja na hoja lukuki cha msingi hapo tamisemi fungeni huo mfumo hicho cha mdah nacho ni kigezo cha kupunguza watu nb sio lazima mwaka huu tafuta vyeti mwakani pia zitatangazwa ajira mpya utaomba omba uzima tu
 
Scan barua yako ya maombi ya cheti na leseni, fanya mawasiliano kwa 0765920855,haraka sana,vitu vyako vitafuatwa pale MCT,kwasasa wako Jakaya Kikwete.Gharama ni za kawaida.Fanya kama wenzako,utahudumiwa kwa haraka.
 
Mm naona wafunge tu hata Leo kuna demu ni mwalimu wa phy na chem aliomba siku ya kwanza kabisa mpaka Leo shule alizoomba ipo hivi

Shule ya kwanza wapo 2

Shule ya pili na ya tatu yupo yeye tu

Shule ya nne wapo 5

Shule ya tano wapo 3

Alafu kuna sehemu English wapo watu 756 [emoji23][emoji23]
Nimeona shule ziko bushi ndani ndaan toka tangazo litoke. Hadi leo waombaji wako 20
 
messenger wa dodoma kaanza na yakee...aya fwateniii
Tuko pamoja,hiyo ni moja ya shughuli zinazofanyiwa kazi kwa wale wanaochukua kwa mara ya kwanza na hata wanaorenew.
Malipo yanafanyika baada ya kilakitu kukamilika,ambapo wahusika hupigiwa nyaraka zao picha,nakuwatumia wahakiki kweli zimechukuliwa na ni zenyewe,baada ya hapo,husema modality ya utumwaji wa hizo parcels,kama ni kwa njia ya BUS au vinginevyo.
Epuka gharama zinazoepukika, DODOMA MESSENGERS ni jibu la tatizo lako.
0765920855 ndiyo namba ya mawasiliano,iwe WhatsApp au kwa call za kawaida.Hakikisha kama ni WhatsApp,unaona picha hiyo iliyopo hapo kwenye profile.
 
Ndugu zangu ningeomba tutumie huu Uzi kutoa maoni Kwa kuwaomba TAMISEMI kuongeza Muda wa watanzania kutuma maombi ya Kazi za ualim na Afya.

Kwanza muda uliotolewa no siku ambazo sio Chini ya 20 na yawezekana wengi wasiombe na kukosa Fursa ya Kuajiriwa(Kwa wale watoto wa maskini) ambao hawana plan yoyote ile.

Tunaomba Mama yetu ANGELA KAIRUKI uongeze Muda ili wafuassi wako wapate kupona. Sababu kubwa za Kuomba muda uongezwe no hizi hapa;
1. Ucheleweshaji wa Transcript na Leseni za MCT
Kwa ambao mmenda NACTE pale Kuna watu waliomba Transcripts za Kada ya Afya Kwa muda mrefu lakini Huwa zinacheleweshwa. Mtu analipa ili atumie Transcripts mkoani anaisubiri haimfikii anaamua Kufunga safar mpaka NACTE ili apatiwe anatumia siku Mbili Toka Mkoani mpaka Dar akifika pale tayari muda unakuwa umeisha kabisa au anapewa majibu ya subiri.

2. Ulazima wa kuwa na Leseni za MCT na Bodi nyingine kama Za Famasia na Uuguzi Kwa Nursing. Kama mnavyojua anayemaliza chuo Kwa Afya ili afanye kazi lazima awe na leseni. Hii wengi hawaipingi ila tatizo ni pale ambapo Leseni hizi zinachelewa. Mfano mtu kamaliza chuo 2020 ama 2021. Akishamaliza chuo anapaswa awe na leseni leseni kuipata sio Chini ya 400K yaani ada zake na Enrollment Fees. Kwa watanzania walio wengi kupata Laki nne ya kulipa ili apewe leseni kwanza ni Kizungumkuti. Pili Kwa wengine akishalipia Leseni haifiki Kwa wakati. Mfano hapo MCT Kuna mtu alilipia leseni Wiki Iliyopita Jumanne akaambiwa ndani ya Siku Tano itapatikana akaamua Kurudi Mkoani amekwishafika anaisubiri anaambiwa bado. Ina maana Mpaka Deadline inafika atakua hajaipata.

Kama mnavyojua wengi hufuatilia vyeti vyao pale ambapo kazii hutangazwa lakini Kuna yrasimu MKUBWA wa kupata vyeti haswa vya kitaaluma na ukitoa wiki mbili owe deadline ya kutuma maombi watu wengi wanaumia
Zipo sababu nyingi sana ambazo zinachelewesha watu kutokupata Documents zote za kuombea kazi.

Tunawoamba TAMISEMI kuongeza Muda hata wa wiki mbili au zaidi ili watu wapate Fursa ya Kuomba Kazi na kuijenga Nchi.
Mtaomba ajira zijazo sio lazima wote tutume maombi.
 
Huo muda wa maombi uliotolewa unatosha, mtu anapaswa kufuatilia vyeti na document nyingine punde anapomaliza masomo. Sasa umemaliza 2020 au 2021 hadi leo hivyo viambata huna, tatizo la nani hapo? Na utake upate mapema kwa kuwa ajira zimetolewa, huo ni uzembe wako.

Kama tatizo lilikuwa pesa huko nyuma. Leo umeitoa wapi?
Muda wamepewa mwingi sana ni uzembe tu, na ujinga ujinga mwingi
 
Back
Top Bottom