TAMISEMI ongezeni muda wa kutuma maombi ya ualimu na afya

Nimependa point namba 5🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wa TZ wanapenda deadline.Mtu amemaliza chuo mwaka juzi mpaka sasa hajachukua cheti chake.

Mimi nafikiri muda usiongezwe kwani hii ni njia ya kupunguza watu.🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Isshue ya Leseni imeletwa juzi. Haikuwepo. Shida sio kujua shida no urasimu wa upatikanaji
Acha mambo yako wewe leseni zipo muda sana na kupata leseni hakuna urasimu wowote. Shida sisi watanzania tunapenda sana kulialia kuonewa huruma, chuo umemaliza miaka 2, 3 nyuma kwanini usifatilie leseni na vyeti vyako mapema?

Kupata transcript nacte sio lazima uende headquarter zipo ofisi za nacte kila kanda Arusha, mwanza, mbeya, tabora, mtwara, dodoma kwanini uende headquarter?

Vijana badilikeni siku 20 zilizotolewa ni nyingi sana acheni mambo ya zimamoto unatakiwa kuwa tayari muda wowote kama mwanajeshi.
 
Wewe kama hukuandaa vitu vyako mapema usiandike ujinga humu,
Kwanza kupata Nacte transcript haichukui hata week tatu wewe useme ukweli umeanza kushugulikia vitu baada ya ajira kutangazwa
Hauko serious na mambo yako

Utajijua
Wiki 3 ni nyingi sana sasa hivi siku 5 tu transcript inakuwa collected
 
Niongeze maoni.

Kuhusu idara ya afya kitengo cha USTAWI WA JAMII mwaka jana walitoa nafasi zisizo zidi 50 kati ya nafasi za afya zote maelfu.

Wanao omba hiyo ustawi unaweza kukuta ni wengi sana zaidi ya mamia lakini wanachukuwa watu 40+

Kingine ni mwaka!!! KUMBE KWENYE AFYA HUKU hawaangalii mwaka wa kuhitimu ???


Kuna watu wamechukuliwa wa mwaka 2006,7,8,9,10 wa mwaka 2015 kuendelea wapo 3

Hii ipoje [emoji115]

Kwa mjibu wa nafasi za mwaka jana 2022.

Vipi mwaka huu?
 
Sababu ambazo umeandika ni dhaifu sana mkuu. nijuavyo Mimi sababu ambazo ninaweza kuongezwa muda kutuma maombi ni;
1. Tatizo la mtandao au mfumo wao kuwa changamoto.
2. Marekebisho ya tangazo baada kutolewa mara yakwanza then wakafanya marekebisho ya tangazo.
 
Umesema kitu kizuri sana hila tambua hata wakisema deadline iwe mwezi wa 12 bado kuna watu watakuja kuomba mdah wa nyongeza wakamilishe maombi watakuja na hoja lukuki cha msingi hapo tamisemi fungeni huo mfumo hicho cha mdah nacho ni kigezo cha kupunguza watu nb sio lazima mwaka huu tafuta vyeti mwakani pia zitatangazwa ajira mpya utaomba omba uzima tu
 
Scan barua yako ya maombi ya cheti na leseni, fanya mawasiliano kwa 0765920855,haraka sana,vitu vyako vitafuatwa pale MCT,kwasasa wako Jakaya Kikwete.Gharama ni za kawaida.Fanya kama wenzako,utahudumiwa kwa haraka.
 
Nimeona shule ziko bushi ndani ndaan toka tangazo litoke. Hadi leo waombaji wako 20
 
messenger wa dodoma kaanza na yakee...aya fwateniii
Tuko pamoja,hiyo ni moja ya shughuli zinazofanyiwa kazi kwa wale wanaochukua kwa mara ya kwanza na hata wanaorenew.
Malipo yanafanyika baada ya kilakitu kukamilika,ambapo wahusika hupigiwa nyaraka zao picha,nakuwatumia wahakiki kweli zimechukuliwa na ni zenyewe,baada ya hapo,husema modality ya utumwaji wa hizo parcels,kama ni kwa njia ya BUS au vinginevyo.
Epuka gharama zinazoepukika, DODOMA MESSENGERS ni jibu la tatizo lako.
0765920855 ndiyo namba ya mawasiliano,iwe WhatsApp au kwa call za kawaida.Hakikisha kama ni WhatsApp,unaona picha hiyo iliyopo hapo kwenye profile.
 
Mtaomba ajira zijazo sio lazima wote tutume maombi.
 
Muda wamepewa mwingi sana ni uzembe tu, na ujinga ujinga mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…