LGE2024 TAMISEMI: Wananchi 26,769,995 wamejiandikisha katika Daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi kufikia Oktoba 19, 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Waziri anafikiri kila mtu ni mjinga ,kuna demu wangu ni mtendaji mpaka sasa yupo ofisini anawasubiri waandikishaji wampelekee idadi ya leo
Amekudanganya bwana. Sio kwamba zinatumwa kwa njia ya simu kila siku jioni? Huyo atakuwa na lake jambo huko ofisini 😄
 
Waziri anafikiri kila mtu ni mjinga ,kuna demu wangu ni mtendaji mpaka sasa yupo ofisini anawasubiri waandikishaji wampelekee idadi ya leo
Pole
FB_IMG_1699990708879.jpg
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kufikia Oktoba 19, 2024, Jumla ya watanzania wenye sifa Milioni 26,769,995 sawa na asilimia 81% wamejiandikisha kwenye daftari la Mpigakura, tayari kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Waziri Mchengerwa ametoa takwimu hizo leo Jumapili Oktoba 20, 2024 akiwa Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, akiitaja Mikoa ya Tanga, Pwani, Mwanza, Dar Es salaam na Dodoma kuwa Vinara katika uandikishaji huo.

Mhe. Mchengerwa kando ya Kutangaza kutoongezwa kwa siku za kujiandikisha, amewashukuru watanzania wote waliotumia haki yao Kikatiba katika kujiandikisha kwenye Daftari hilo, akiwataka pia wale wote wenye sifa za kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi kujitokeza kwa wingi kuanzia Oktoba 26, 2024 ili kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali kwenye serikali za Mitaa.

Mhe. Mchengerwa kadhalika ametoa wito kwa wasimamizi wa Uchaguzi na wadau wote wa Uchaguzi kuendelea kuzingatia sheria na taratibu zinazosimamia Uchaguzi huo, akihimiza pia suala la usimamizi na utekelezaji wa falsafa ya 4R za Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha haki, usawa na Uhuru wa kuchagua unatamalaki kwenye Uchaguzi huo wa baadae mwaka huu.
Hivi hawa viongozi kwanini wanatuonea watanzania kuwa ni wajinga kiasi cha kutudanganya bila aibu?
 
Kwahapa Sio kweli
Japo Waliamua Kupita Nyumba kwa nyumba Mtaani Ila Hiyo idadi ni Uongo
 
Kujumlisha kiteknolojia kunachukua dakika ngapi?
Sikutegemea swali kama hili kutoka Kwa mtu kama wewe!! Kweli?
Issue siyo kujumlisha tu Bali ni kukusanya taarifa zenyewe kutoka Halmashauri zaidi ya 180...!halafu ndio waanze kuzijumlisha . Huoni kama waziri amepika data?
Tufikiri hiyo taarifa ni kweli, kwahiyo maana yake siku ya UCHAGUZI tutegemee midururu mirefu ya wapiga kura. Haitakaa itokee
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kufikia Oktoba 19, 2024, Jumla ya watanzania wenye sifa Milioni 26,769,995 sawa na asilimia 81% wamejiandikisha kwenye daftari la Mpigakura, tayari kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Waziri Mchengerwa ametoa takwimu hizo leo Jumapili Oktoba 20, 2024 akiwa Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, akiitaja Mikoa ya Tanga, Pwani, Mwanza, Dar Es salaam na Dodoma kuwa Vinara katika uandikishaji huo.

Mhe. Mchengerwa kando ya Kutangaza kutoongezwa kwa siku za kujiandikisha, amewashukuru watanzania wote waliotumia haki yao Kikatiba katika kujiandikisha kwenye Daftari hilo, akiwataka pia wale wote wenye sifa za kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi kujitokeza kwa wingi kuanzia Oktoba 26, 2024 ili kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali kwenye serikali za Mitaa.

Mhe. Mchengerwa kadhalika ametoa wito kwa wasimamizi wa Uchaguzi na wadau wote wa Uchaguzi kuendelea kuzingatia sheria na taratibu zinazosimamia Uchaguzi huo, akihimiza pia suala la usimamizi na utekelezaji wa falsafa ya 4R za Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha haki, usawa na Uhuru wa kuchagua unatamalaki kwenye Uchaguzi huo wa baadae mwaka huu.
hii nchi tumechagua uongo kuwa sehemu ya maisha yetu.
Too bad!
 
Back
Top Bottom