LGE2024 TAMISEMI: Wananchi 26,769,995 wamejiandikisha katika Daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi kufikia Oktoba 19, 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kufikia Oktoba 19, 2024, Jumla ya watanzania wenye sifa Milioni 26,769,995 sawa na asilimia 81% wamejiandikisha kwenye daftari la Mpigakura, tayari kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Waziri Mchengerwa ametoa takwimu hizo leo Jumapili Oktoba 20, 2024 akiwa Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, akiitaja Mikoa ya Tanga, Pwani, Mwanza, Dar Es salaam na Dodoma kuwa Vinara katika uandikishaji huo.

Mhe. Mchengerwa kando ya Kutangaza kutoongezwa kwa siku za kujiandikisha, amewashukuru watanzania wote waliotumia haki yao Kikatiba katika kujiandikisha kwenye Daftari hilo, akiwataka pia wale wote wenye sifa za kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi kujitokeza kwa wingi kuanzia Oktoba 26, 2024 ili kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali kwenye serikali za Mitaa.

Mhe. Mchengerwa kadhalika ametoa wito kwa wasimamizi wa Uchaguzi na wadau wote wa Uchaguzi kuendelea kuzingatia sheria na taratibu zinazosimamia Uchaguzi huo, akihimiza pia suala la usimamizi na utekelezaji wa falsafa ya 4R za Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha haki, usawa na Uhuru wa kuchagua unatamalaki kwenye Uchaguzi huo wa baadae mwaka huu.
Huo ni uongo bwana,hakuna ,ni uongo!

View: https://youtu.be/B9D0iuBx7n0?t=21
 
Chadema mshakata tamaa jitoeni kwenye siasa sajilini saccos maana hamna mnachoweze
Ni kweli kabisa, cdm hawawezi siasa za hadaa, hivyo ni bora wakae pembeni wawaachie ccm wanaoweza siasa za hadaa.
 
Kama 2.6M nchi nzima ntakubaliana nae ila kwa namba ya 26 million. Haikubaliki duniani wala mbinguni🤣!

Daftari la kujiandikisha limesusiwa kama msiba wa shoga.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kufikia Oktoba 19, 2024, Jumla ya watanzania wenye sifa Milioni 26,769,995 sawa na asilimia 81% wamejiandikisha kwenye daftari la Mpigakura, tayari kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Waziri Mchengerwa ametoa takwimu hizo leo Jumapili Oktoba 20, 2024 akiwa Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, akiitaja Mikoa ya Tanga, Pwani, Mwanza, Dar Es salaam na Dodoma kuwa Vinara katika uandikishaji huo.

Mhe. Mchengerwa kando ya Kutangaza kutoongezwa kwa siku za kujiandikisha, amewashukuru watanzania wote waliotumia haki yao Kikatiba katika kujiandikisha kwenye Daftari hilo, akiwataka pia wale wote wenye sifa za kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi kujitokeza kwa wingi kuanzia Oktoba 26, 2024 ili kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali kwenye serikali za Mitaa.

Mhe. Mchengerwa kadhalika ametoa wito kwa wasimamizi wa Uchaguzi na wadau wote wa Uchaguzi kuendelea kuzingatia sheria na taratibu zinazosimamia Uchaguzi huo, akihimiza pia suala la usimamizi na utekelezaji wa falsafa ya 4R za Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha haki, usawa na Uhuru wa kuchagua unatamalaki kwenye Uchaguzi huo wa baadae mwaka huu.
CCM nawashauri kwa nguvu zote waendelee kuhamasisha watu kujiandikisha na kwenda kupiga kura na mwisho wa zoezi hili waibe kura kama ilivyo kawaida yao kudharau na kutukana maamuzi ya wananchi.Hii ya kuendelea kuiba kura na kujipigia kura itatengeneza UASI mzuri dhidi ya serikali ya wezi inayojichagua kwa kujipigia kura bila ridhaa ya wananchi.Maana ni ajabu kuona eti katikati ya maisha magumu waliyonayo watanzania eti chawa wanamwambia mama yao kwamba bado anapendwa sana na watanzania,ni mwehu tu,machawa na wapambe ndio wanaweza kuamini hivyo.
 
Nashaur siku ya kupiga kura zaidi ya kura zao za maruhani walizozoea,waweke watu mahsusi wachkue idadi sahihi ya walioenda kupiga kura ili wabaki na ukweli waujadili kwenye vikao vyao,itawasaidia,wajiulize maswali ya msingi na wajijibu kwa dhati.
Tumefikaje hapa?
Tunaelekea wapi?
Hadi lini tutafanya hivi?
Kwa maslahi ya nani haswaa tunafanya hivi?
Inajenga nini mioyoni mwa wanaoongozwa?

Koz siku yaja, isije kama mwizi!
 
Ukweli huu wanaujua, ila hawana uthubutu wa kuujadili maana ni ukweli unaoumiza.
 
Mcherengwa ameamua kuwa jambazi kabisa 😂, let's see his final destination
Final destination ni ataendelea alipoishia.

Pelekeni hii kitu mahakamani uchafuzi huu usitishwe. Otherwise acheni kujisemesha kama hamna la kufanya.

Upinzani msijidanganye kwa kusema ‘yana mwisho’ huo mwisho ni lini? Acheni kulalamika, msijifariji eti watake wasitake blhbla..

Hii tactic imetumika over n over na wameendelea kujitangazia ushindi.

Wananchi wamelala tamaa hawana matumaini na vyama vya siasa..

Vyama vya siasa vinatengeneza mazingira ya kuchukua ryzyku the rest haiwahusu.

Vyama vyote ni dugu moja!
 
Sawa
 
Zoezi limefungwa jana jioni asubuhi hii tayari Mchengerwa ana data za Tanganyika yote, ni uongo wa kiwango cha juu sana, angesubiri hata zipite japo siku tau ndiyo atoe hizi takwimu zake za kupika.
 
Back
Top Bottom