Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) kuhusu mkataba baina ya Tanzania na DP World

Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) kuhusu mkataba baina ya Tanzania na DP World

Brother kama kweli ww ni muumini, basi kuna jambo kubwa la kujitafakari elimu dunia wengi wameipa kisogo, ni muda muafa wa kuhimizana on the long run haisaidii. Maana nchi haiendeshwi na imani
Hiyo elimu dunia yako haijakusaidia chochote,maana umeandika togwa tu hata mwenyewe ukisoma unashangaa
 
Kuna matabaka ndani ya uongozi

Kuna baadhi ya viongozi hawakubaliani na utawala uliopo wanamuwekea tu poker face kumhadaa ili ajue yupo pamoja nao.
Hii naunga mkono na inatugharimu kwelikweli
 
Ansar Sunna wameniangusha Sana. Nao wameingia kwenye shimo. TEC inanguvu sana , kauli moja tu wote wametoka mafichoni. Bado Tamko la Ahmadiya.
Hao hawajaingia kwenye shimo

Walikuwepo kwenye shimo tangu kitambo we ndo umechelewa kujua
 
Helo Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) Wameshutumu Vikali kile wamepita Undumilakuwili na Ukosefu wa Uadilifu Kwa Wanaopinga mkataba wa Bandari kwa kile wameita kugumbia macho Mikataba ya hovyo iliyowahi ingiwa hapo kabla.
---
Mimi nimeiona mipasho tu na chuki kwa Wakatoliki;hoja za msingi zinazobishaniwa hazijaguswa kwa Waraka wa TEC.Bado naamini Waraka wa TEC umeandaliwa kisomi,ukiwa na akili ndogo huwezi kuelewa.
Mwisho:Ndugu zangu Waislamu wekezeni nguvu kwenye Elimu Dunia naona mmebobea kwenye Elimu ahera na Dunia inawaacha nyuma kwa kasi sana!
 
Hiyo elimu dunia yako haijakusaidia chochote,maana umeandika togwa tu hata mwenyewe ukisoma unashangaa
sawa mkuu ila ukipata muda soma vizuri apo kwa makini ata kwa baadae inaweza saidia maana wengine sisi ni waandishi wabovu,

Swali la kufungia umeona watu wa imani ambao ni wasomi wakisapoti tamko hili??
 
Helo Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) Wameshutumu Vikali kile wamepita Undumilakuwili na Ukosefu wa Uadilifu Kwa Wanaopinga mkataba wa Bandari kwa kile wameita kugumbia macho Mikataba ya hovyo iliyowahi ingiwa hapo kabla.
---

Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) likielezea kuhusu makubaliano ya uendeshaji na uendelezaji wa bandari."

BASUTA haturidhishwi na 'undumilakuwili' na ukosefu wa uadilifu wa wapingaji wa mkataba ambao walifumbia macho mikataba mingi ya hovyo huko nyuma katika sekta mbalimbali ikiwemo madini na hawakutaka ifutwe lakini wako tayari kwa gharama yoyote kuhakikisha mkataba huu unafutwa na unakufa".
---
TAMKO LA BARAZA KUU LA JUMUIYA ZA ANSAAR SUNNAH TANZANIA (BASUTA) KUHUSU MKATABA BAINA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KUHUSU USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA KIJAMII KWA AJILI YA UENDELEZAJI NA UBORESHAJI WA

UTENDAJI KAZI WA BANDARI TANZANIA

MJADALA WA MKATABA WA BANDARI USITAWALIWE NA UZUSHI NA CHUKI ZA KIDINI

Utangulizi
a) Kwa kuwa katiba ya nchi yetu ya mwaka 1977 toleo la 2000 ibara ya 18 (1) na 19 (1)

zinatoa haki ya kila mtu kuwa na uhuru wa kuwa na maoni yake na kutoa nje mawazo yake;

b) Kwa kuwa katiba yetu inatoa haki sawa kwa raia wote pasina ubaguzi wowote kwa

misingi ya dini, rangi, kabila, jinsia au vyovyote vile;

c) Kwa kuwa watu wengine wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini,

wanataaluma, wanahabari na wadau wengine wamekuwa wanatoa maoni yao kuhusu

suala la Mkataba baina ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya

Dubai kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na

Uboreshaji wa Utendaji kazi wa Bandari Tanzania kupitia kampuni ya DP World

inayomilikiwa na serikali ya nchi hiyo;

d) Kwa kuwa katika mijadala hiyo kumekuwa na upotoshaji mwingi wa makusudi wa

matukio na taarifa kuhusu Mkataba huo wa bandari kwa chuki au kwa ajili ya kutetea

maslahi binafsi ya kiuchumi, kisiasa au ya kidini ya makundi fulani

e) Na kwa kuwa na sisi, BASUTA, ni Watanzania, viongozi wa taasisi ya dini, kama ilivyo kwa viongozi madhehebu mengine yaliyotoa maoni.

Hivyo basi, sisi viongozi wa Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania, kwa kujali maslahi mapana ya taifa,

tumeamua leo Agosti 23, 2023 kutoa tamko letu kuhusu mwenendo wa mjadala wa

Mkataba huo wa bandari, kama ifuatavyo:

Maoni Yetu

1.0 Kuhusu maudhui ya Mkataba wenyewe

a) Kwa kuwa, tunaamini Serikali kupitia wataalamu wake imetoa ufafanuzi wa kutosha

kwa wadau wanaokosoa baadhi ya vifungu vya Mkataba huo na hivyo kutaka yafanyike

maboresho na kundi jingine (ambalo hatukubaliani nalo) linalopinga Mkataba wote;

b) Na kwa kuwa wanaopinga Mkataba wote na kutaka ufutwe, walifungua kesi

Mahakama Kuu ya kuomba tafsiri ya kisheria ambayo, kama utawala sheria unavyotaka,

ilisikilizwa kwa haki na uwazi; kisha hukumu kutolewa kwamba, licha ya kasoro ndogo

ndogo Mkataba huu ni halali kwa mujibu wa sheria za nchi na unaweza ukaendelea.

c) Na kwa kuwa serikali sikivu ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais Dr Samia Suluhu Hassan imeahidi kusikiliza na kurekebsha kasoro zote zilizoainishwa kwa maslahi ya taifa.

Hivyo basi, sisi BASUTA tusingependa kujikita kwenye mjadala wa vipengele mahususi

wa Mkataba wenyewe wa bandari tukiamini mchakato unaenda vizuri na maslahi mapana ya taifa yatafikiwa.

2.0 Katika mjadala wa Mkataba huu, BASUTA haturidhishwi na undumilakuwili na ukosefu

wa uadilifu wa wapingaji wa Mkataba ambao walifumbia macho mikataba mingi na ya

hovyo zaidi huko nyuma katika sekta mbalimbali, ikiwemo madini, na hawakutaka

ifutwe; lakini wako tayari kwa gharama yoyote kuhakikisha Mkataba huu unafutwa na

unakufa. Wanasahau kuwa huu si Mkataba wa kwanza wa ukodishaji wa uendeshaji

bandarini, bali awali ilipewa jukumu hilo kampuni ya TICTS na kufanya kazi hiyo kwa

miaka takriban 22. Hadi TICTS inaondoshwa, hakujawahi kuwa na mijadala ya hisia

kama hii kupinga sera za uwekezaji na eti kutaka Watanzania wenyewe ndio waendeshe rasilimali zao, kama lilivyodai kanisa Katoliki na wadau wengine.

3.0 BASUTA tunatambua na kuheshimu haki ya makundi ya watu wakiwemo wanasiasa,

madhehebu ya dini, wasomi na wanahabari, kuwa na maoni, lakini haturidhishwi na

baadhi ya hoja za kibaguzi dhidi ya Uarabu, na hata Uislamu zinazotolewa na makundi

yanayotaka Mkataba huu wa bandari ufutwe. Badala ya kauli kama vile “Hatuwezi

kuwapa Waarabu bandari zetu”, tunadhani jambo bora na la busara ni kujikita kwenye

vipengele vya Mkataba kuainisha maeneo yenye udhaifu ili serikali iangalie namna ya kuboresha.

4.0 Vilevile, BASUTA inashangazwa na kusikitishwa na upotoshaji wa makusudi wa baadhi ya mambo katika mjadala wa Mkataba huu wa bandari, licha ya ufafanuzi uliotolewa na serikali, ikiwemo madai kuwa bandari inauzwa, DP World wanapewa waendeshe bandari zote na mengineyo.

Kipekee, tunasikitishwa sana na kauli isiyo na ushahidi wa kidodoso wa Kanisa Katoliki iliyodai eti wananchi wengi wanapinga Mkataba na wanataka ufutwe, ilihali hakuna utati kuhusu hilo uliofanyika.

BASUTA inashangazwa zaidi na makundi ya wapingaji kutotaka kusikiliza hoja zozote za ufafanuzi na kung’ang’ania misimamo.

Tunajiuliza, tatizo ni Mkataba tu au kuna waliyoyaficha vifuani mwao?

5.0 BASUTA tunasikitishwa na lugha za shinikizo na vitisho vya kuiangusha serikali kwa maandamano, fujo na vitendo vya jinai na uhaini. Iwapo kila kundi litataka matakwa yake yatimizwe kwa njia hizo, nchi inaweza kutumbukia katika machafuko makubwa.

Katiba inazungumzia haki ya kutoa maoni na kusikilizwa lakini haisemi lazima yafuatwe.

Utayari wa baadhi ya watu kuvuruga amani ili yao yatimie unazidi kutupa wasiwasi kuwa tatizo hasa sio Mkataba tu bali kuna chuki zilizojicha. Kwa kuliona hili, BASUTA tunatoa wito wa kuheshimiwa utawala wa sheria, hususan mfumo wa kukiwa maamuzi ya kiserikali katika uendeshaji wa nchi, kama yalivyoanishwa katika Katiba na Sheria za nchi kupitia vyombo rasmi kama Serikali, Bunge na Mahakama.

6.0 BASUTA imefurahishwa na kauli ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dr Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Agosti 21, 2023 wakati akihutubia katika

sherehe za miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya kuonesha

msimamo imara wa serikali na utayari wa kupambana na wanaotishia kuvuruga amani, pale aliposema: “Hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa taifa hili…. wa kuivunja
amani ya nchi yetu.”

7.0 Pamoja na kufurahishwa na msimamo wa Serikali, BASUTA tunaipa rai isikubali kuendeshwa kwa shinikizo la kundi lolote la kisiasa, kidini au kijamii na kufanya

maamuzi kwa kutii matakwa ya kundi hilo kwani kwa kufanya hivyo itaendeleza mbegu

mbaya iliyopandwa huko nyuma, ikamea na kuzaa tabaka la watu (wa aidha chama au dhehebu moja la dini) ambao ni raia zaidi kuliko wengine, na hivyo kuwa na kura ya

‘Veto’ katika maamuzi. Watu hao wasipolitaka jambo haliwi na wakilitaka huwa – tena

kwa sababu ya maslahi yao binafsi.

8.0 Kwa msingi wa tuliyoyataja katika 4.0, kuhusu kauli za ubaguzi, tunawahimiza Watanzania wenzetu hususan viongozi wa dini, ambao kauli zao ndiyo hatari zaidi kwa

sababu ya ushawishi mkubwa walionao, kujiepusha na matamko ambayo yanaweza

kuipelekea nchi yetu katika laana ya uvunjifu wa amani kama ilivyotokea Rwanda 1994

na nchi nyingine.

Tunakumbusha kuwa katika baadhi ya nchi hizo, mambo yalianza hivi hivi kwa nyaraka namatamko ya kichungaji. BASUTA tusingependa kuyaona hayo yakitokea katika nchi yetu na tunatoa rai kwa serikali na vyombo vyake vya usalama viwe makini sasa kuliko wakati wowote ule.

9.0 BASUTA, kama tulivyotaja awali, tunaamini katika ukosoaji wenye afya wa kutaka maboresho ya baadhi ya vipengele vya Mkataba na sio upingaji wa jumlajumla wa kuukataa Mkataba wote.

Tunaamini aina ya pili ya upingaji unachangiwa zaidi na hisia kuliko hoja za msingi kwa ushahidi wa wazi wa kauli za chuki na ubaguzi dhidi ya Uarabu zinazotolewa na baadhi ya watu hususan mitandaoni na pia kwa ushahidi wa kampeni kubwa ya ‘kiimani’ ya Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kupinga Mkataba huu kupitia kanisani.

Kwa msingi huo, BASUTA tunatoa rai kwa TEC na makundi mengine kutafakari upya

misimamo yao kwa maslahi ya taifa na waweke pembeni hisia. Wakifanya hivyo,

watagundua kuwa huu siyo Mkataba wa kwanza wa aina hii duniani na hata hivyo ipo

nafasi ya maboresho. Pia, nchi nyingi duniani za Wakristo tena Wakatoliki zinafanya kazi

na DP World zikiwemo Angola kupitia bandari ya Lobito yenye urefu wa kilometa 7.2 wakati gati la Dar es Salaam linalokusudiwa lina urefu wa kilometa 2 tu.

Pia, zipo nchi kama Msumbiji kupitia bandari ya Beira, Brazil na Ufiilipino.

Hivyo, mikataba ya DP World na nchi hizi itoshe kuwahikikishia kuwa uwekezaji huu unahusu biashara yenye tija kwa taifa, na sio kitu kingine.

10.0 BASUTA, tunaungana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, kutahadharisha dhidi ya tabia ya kutumia majukwaa ya dini kwa maslahi ya siasa au kinyume chake, kwani kufanya hivyo kunaweza kuleta uvunjifu wa amani na kuharibu utulivu wa taifa.

Katika suala hili, tumesikitishwa kuona TEC inaendesha kampeni kubwa za kanisani kupinga Mkataba.

Iwapo mamlaka za dini nyingine zikianza kampeni kutetea Mkataba katika nyumba zao za ibada, tuna wasiwasi suala hili la kiuchumi halitaamuliwa kwa uzito wa hoja bali

ufuasi wa dini.

Mheshimiwa Kikwete alionya: “Siku ikika uanachama wa chama cha kisiasa au uumini

thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha kisiasa anachokifuata ndiyo mwisho wa nchi yetu…kutakuwa na chama cha siasa cha Wakristo, cha Waislamu vyama vya siasa vya Walokole.

Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, Serikali na utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari.”

11.0 Kwa kuwa imeibuliwa hoja ya ukomo wa Mkataba wa bandari, BASUTA inatoa wito wa kufanywa mapitio ya mikataba mingine isiyo na ukomo, ikiwemo ule ulioingiwa mwaka 1992 kati ya Serikali na makanisa (Memorandum of Understanding) ambapo sehemu ya mabilioni ya walipakodi, hata wasio Wakristo, hutolewa na serikali kwa ajili ya hospitali na vyuo vikuu vya makanisa hayo. Pia, tunataka makubaliano

yanayozungumzwa mara kwa mara kati ya serikali na kanisa ya kutojengwa hospitali za

umma mahali zilipo hospitali za makanisa yafutwe kwa sababu wananchi wana Mkataba na Serikali kuwakishia huduma za jamii kwa gharama wanayoweza kuzimudu na sio kanisa.

12.0 Hata hivyo, kwa ujumla, BASUTA inaungana na msimamo wa Serikali, Bunge na Mahakama Kuu kwamba Mkataba huu siyo tu ni sahihi bali pia ni muhimu kwa maslahi ya nchi.

Uwekezaji wa kampuni kubwa yenye uwezo wa mkubwa wa kimitaji na kiteknolojia, na yenye uzoefu na weledi kama DP World ya Dubai utaleta ufanisi katika biashara ya bandari hasa katika mazingira ya sasa ya ushindani mkubwa uliopo, na hivyo kuliwezesha taifa kuvutia nchi nyingi kutumia bandari zetu kupitisha mizigo yao na kuliingizia taifa mapato makubwa.

Angalizo:
Kuhusu vipengele vya mkataba wa bandari, majadiliano mengi yamefanyika huko nyuma na serikali Imeshatoa ufafanuzi dhidi y aupotoshaji unaofanywa hivyo BASUTA haikujikita katika mawanda hayo.

Hitimisho
Kwa maslahi ya umoja, mshikamano, utulivu na ustawi wa nchi yetu, tumetoa tamko letu hili

kwa nia njema kabisa kwa maslahi ya nchi yetu na Watanzania wote pasina kujali dini, rangi,

kabila, jinsia wala tofauti zao za kisiasa.



Tanzania ni kubwa kuliko sisi sote na wala baadhi yetu wasijitwishe ukiranja wa kuwasemea wengine ilhali wako hai na wanazo haki za kiraia kama walizo nazo wao.



Mungu Ibariki Tanzania.


My Take
TEC wamechokonoa vingi.
Sijaambulia hata moja hapa inamaana hawa basuta wamekuja kuishambulia tec badala ya kutoa maoni yao😂😂😂😂😂
 
sawa mkuu ila ukipata muda soma vizuri apo kwa makini ata kwa baadae inaweza saidia maana wengine sisi ni waandishi wabovu,

Swali la kufungia umeona watu wa imani ambao ni wasomi wakisapoti tamko hili??
Apo,ata...ulisoma wapi!?..we usomi unauchukulia vipi!?..vyuo vitu vinatoa watu wanaovaa suti na tai jua Kali na nyuzi joto 30-35,huyo ana akili timamu!?..
 
Apo,ata...ulisoma wapi!?..we usomi unauchukulia vipi!?..vyuo vitu vinatoa watu wanaovaa suti na tai jua Kali na nyuzi joto 30-35,huyo ana akili timamu!?..
ata,,,, hata

mkuu, waislamu wa arabuni na sisi huku tanzania kuna utofauti mkubwa. Mm naweka nukta mkuu
 
Badala ya kuja na hoja juu ya vipengele vya mkataba wao wanasema tayari vimeshajadilwa, sasa hii inakuwa vipi??? Tena katika hili hupaswi kumu attack mtu/taasisi directly wee jibu vifungu alivyodai vina utata njoo na argument yako kuelezea umakini wake

Sasa ukija na ushubwada kama huu ambao ni mipasho badala ya uchambuzi wa kina mnaonesha ni kwa namna gani mlivyo weupe kichwani

As a matter of fact, govt works on paper, je kuna document yoyote ambayo imetoka serikalini inafafanua kifungu kimoja baada ya kingine? Ningependa kuipata kama ipo niisome kwa makini
Asante sana comrade.
 
BASUTA haturidhishwi na 'undumilakuwili' na ukosefu wa uadilifu wa wapingaji wa mkataba ambao walifumbia macho mikataba mingi ya hovyo huko nyuma katika sekta mbalimbali ikiwemo madini na hawakutaka ifutwe lakini wako tayari kwa gharama yoyote kuhakikisha mkataba huu unafutwa na unakufa".
Kabla ya kusoma hayo mengine yote yaliyoandikwa huko chini, kipande hiki hapa pekee kinaonyesha udhaifu mkubwa wa tamko lenyewe.

1. Kama paliwahi kuwepo mikataba mibovu huko nyuma, na bila shaka ilikuwepo, hili Baraza kama waliiona nani aliwazuia wasiitolee tamko?

2. Hili tamko, ni la Mikataba Mibovu, au ni kuhusu shutuma kwa hao wanaoitwa "ndumila Kuwili"?

3. Hawa ni maadui wa nchi, hawana tofauti yoyote na hao wanaotafuta kutuuza huko nje.

4. Hawana chochote kinachotuunganisha kama waTanzania, mbali kabisa na madai wanayofanya hapa.

Ngoja nikasome walichoandika humo.
 
Wewe una elimu gani? Pumbavu mnaficha udini wenu kwenye elimu na elimu yenyewe ni ya kuunga uga
Afu wewe kichwa box kweli unatukana tu watu badala ya kujikita kwenye hoja au ndo umewaandikia huo upumbavu
 
Sijaambulia hata moja hapa inamaana hawa basuta wamekuja kuishambulia tec badala ya kutoa maoni yao[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
It's true niliona live TV Iman kwenye hili waislam wenzangu wa Ansari Sunna wamepuyanga it's a pathetic opinions and shows how they are incompetent [emoji134][emoji134][emoji34][emoji34]
 
Kwani BASUTA ni lini mikataba hiyo ya madini na mingine imewahi kuwekwa hadharani? Kwa kumbukumbu zangu mkataba huu wa bandari ndio wa kwanza kuwekwa hadharani.
 
Helo Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) Wameshutumu Vikali kile wamepita Undumilakuwili na Ukosefu wa Uadilifu Kwa Wanaopinga mkataba wa Bandari kwa kile wameita kugumbia macho Mikataba ya hovyo iliyowahi ingiwa hapo kabla.
---

Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) likielezea kuhusu makubaliano ya uendeshaji na uendelezaji wa bandari."
Lilotafutwa limepatikana sasa kila mtu adai chake tuheshimiane.
 
Back
Top Bottom