Usipende kujumuisha na wasiohusika, Wa - attack hao hao walioandika, na sio ujumuishe waislamu wote. Acha Chuki zako kwa dini nyingine. Nyie ndo huwa mnasema wachaga wote wabahili, wakati huenda kuna wachaga ambao hata wewe huwafikii kwa utoaji; Au wahaya wote wanapenda sifa , wakati huenda kuna wahaya ambao, wewe kwa mijisifa sifa yako hawakufikii; Au kabila fulani wana roho mbaya, wakati huenda katika kabila hilo kuna watu wana roho nzuri hata wewe huwafikii.
Hivyo usipende sana kuhukumu na wasiohusika, sababu hiko kilichoandikwa haimaanishi waislamu wote wa Tanzania nzima wamekipitia na kukiidhinisha kabla ya kuwa published. Na halikadhilika haimaanishi walichosema /walichoaandika TEC haimanishi wakatoliki wote wamekimepitia na kukiidhinisha kabla ya kuwa published.
Kaa ujitafakari. Usijione bora kuliko watu wengine. Huenda hao unaowadharau wakawa bora zaidi kuliko wewe Mbele ya Muumba wa Mbingu, ardhi na vilivyomo.