Uchaguzi 2020 Tamko la chama cha Julius Malema wa EFF juu ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Tamko la chama cha Julius Malema wa EFF juu ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Wangewarudishia kwanza wazawa wa SA ardhi yao iliyoporwa kabla ya kuzungumzia masuala ya Tanzania. Katika uchaguzi huu, endapo wananchi wazalendo wasingeona mbali na kufanya uamuzi mzuri wa kuwakataa hawa vibaraka wa London & Washington, basi nchi yetu ingetumbukia na kuzama kwa mara nyingine tena katika minyororo ya utumwa na kwenye lindi la ukoloni ambamo Rais Magufuli amejitahidi kwa kiasi kikubwa kutunasua na kutunusuru.
 
T
Wizi wa dhahiri na ukiukaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi kama ulivyotokea safari hii kwenye uchaguzi wa 28 October, huhitaji kuleta mtazamaji kuweza kujua uharamia uliofanywa.

Awamu hii imeharibu karibia kila kitu. Imeharibu uwekezaji, umeharibu ajira, na sasa imeharibu taswira ya nchi kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeshawazoa kila mara mkishindwa lazima mlete stori kama hizo. Poleni sana malalamiko FC
 
Ni kweli kuwa CCM ni chama kikongwe Afrika. Kitendo cha vijana wadogo akina Malema na wenzake akina Mbuyiseni Ndlozi kwa kushirikiana na wenzao akina Mnyika na Zitto kutaka kupambana na vyama vikongwe ni utovu wa nidhamu.

Angalia tamko lao kuhusu uchaguzi wa Tanzania lilivyojaa kibri.
View attachment 1618635View attachment 1618636
Nimecheka kama mazuri mkuu yani dam changa kupambana na vyama kongwe ni utovu wa nidhamu? Nashukuru kwa andiko hili mkuu
 
Waangalizi wengi walizuiwa na ccm ndio iliyokuwa inachagua nani wa kuwaangalia na ni nani asije.
Sababu walijua wana mipango michafu ndio maana safari hii wakajidai uchaguzi tumefanya kwa fedha zetu za ndani kumbe ni ili waibe kura watakavyo, jaza sana kwenye mabegi.
 
Sababu walijua wana mipango michafu, ndio maana safari hii wakajidai uchaguzi tumefanya kwa fedha zetu za ndani kumbe ni ili waibe kura watakavyo, jaza sana kwenye mabegi.
Lakini Bwana Polepole kasema juzi kuwa hakuna kura iliyoibwa. NEC pia wametoa taarifa tena safari hii kwa kiingereza ili kuwajulisha mabeberu kuwa hakuna kura iliyokamatwa mtaani ama vinginevyo. Sasa hawa EFF wanapata taarifa kutoka chanzo gani?
 
Lak
Lakini Bwana Polepole kasema juzi kuwa hakuna kura iliyoibwa. NEC pia wametoa taarifa tena safari hii kwa kiingereza ili kuwajulisha mabeberu kuwa hakuna kura iliyokamatwa mtaani ama vinginevyo. Sasa hawa EFF wanapata taarifa kutoka chanzo gani?
Polepole ni nani katika kutenda Haki....aliyesema kura zilizokamatwa ni za Chama Cha Mbowe kama anavyoita CHADEMA..Pathetic
 
Hawa jamaa walileta mwangalizi ili awape ukweli? Au wanahukumu kwa kusikiliza upande mmoja?

Hakuna mtu ambaye hakuona ule upuuzi wa juzi. Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Hayo matamko hayasaidii kitu........kila kitu kinaishia huku mtandaoni...na mkiendelea kusumbua mtandao utazimwa

Zimeni, maana hata sasa mmezima, ila wenye hatari ya kukosa ni vibuyu wa CCM. Ila ule haukuwa uchaguzi bali utoto kama utoto mwingine fullstop.
 
Hivi kura feki nazo zilihitaji waletwe waangalizi ndio wajue kuwa zile ni feki?. Unadhani Tanzania tunaishi shimoni? Kiasi Cha kwamba waliopo duniani hawajui kinachoendelea Tanzania mpaka walete waangalizi?
Hawa jamaa walileta mwangalizi ili awape ukweli? Au wanahukumu kwa kusikiliza upande mmoja?
 
Hawa jamaa walileta mwangalizi ili awape ukweli? Au wanahukumu kwa kusikiliza upande mmoja?
Mwenyekiti wa Electoral Institute for sustainable democracy ni M-south ambaye alikuwa mwenyekiti wa tume yao huru ya uchaguzi, sasa unategemea waseme nini?
 
Wizi walifanya akina Mkapa na Kikwete lakini huu NI UJAMBAZI KABISA.
Lipumba anasema kuna mbunge wake alikwenda kupiga kura kwenye kituo akiwa na familia yake ya watu 7.
Cha ajabu huyo mbunge wake amepata kura 00000000.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Yaani mpaka kura yake watu wamepita nayo.
Mahesabu ya CCM yame kwenda wrong wizi ni jambo baya sana.
 
Hayo matamko hayasaidii kitu........kila kitu kinaishia huku mtandaoni...na mkiendelea kusumbua mtandao utazimwa
Bw. Ngongoti, matamko ni jambo jema hasa yanapotolewa kwa nia njema. Mimi nimegusia nidhamu ya hawa vijana kutoa matamko mazito namna hiyo.
Julishwa kuwa hata NEC wametoa tamko kujibu matamko hayo unayosema hayasaidii. CCM imetoa mfululizo wa matamko kujitenga na tuhuma zilizo kwenye matamko kinzani kwa kuandika ama kuongea.
 
Back
Top Bottom