Tamko la Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kumtaka Freeman Mbowe kuomba radhi

Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa Televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020
Halafu hao Chadema ndiyo wanaomba ridhaa ya kuchukua nchi Oct 28,moja ya Sera zao n Uhuru wa vyombo vya habari,hv mtu Kama huyo umpe nchi aiongoze itakuwaje,some time tuacheni mizaha jamani,hawafai hao hata kwa ubalozi wa nyumba kumi
 
Mbowe ni adui mkubwa wa vyombo vya habari.

Yaliyofanywa na TBC ni sawa?

Kwa nini TBC watupangie ya kusikia toka kwa WAPINZANI wa ccm?
Kejeli zinazotolewa na WAGOMBEA wa ccm ni sukari (tamu)?

Ubaya na madhaifu ya wanaccm yanayosemwa na WAPINZANI wa ccm kwa Nini yawe ni kukiuka maadili ya tasinia ya habari? KWA NINI TBC WALIKATA MATANGAZO NA JANA KULE LINDI WAMERUDIA KUKATA MATANGAZO?

TBC NDIYO WAWAOMBE RADHI WATANZANIA.
 
Zaidi ya miezi 6 Chadema wanalalamika TBC kurusha habari za upande mmoja,sasa walipoanza kurekebisha makosa na kuja kuanza kurusha habari za Chadema sasa mnawafanyia vurugu,mnataka kupora na camera,yani sijui msaidiweje.

Ustaarabu wa kuwatoa ulizingatiwa ndiyo maana waliondoka salama.
Ingewezekana kabisa kuwatoa kwa nguvu, lakini walitakiwa WAFUNGE VIRAGO VYAO NA WAONDOKE KWA USALAMA KABISA. KULIKO KUENDELEA KUFANYIA UHUNI TASINIA YA HABARI.

TBC WAWAOMBE RADHI WANACHADEMA NA WATANZANIA WALIOWANYIMA HABARI HALISI KUTOKA MBAGARA ZAKHEEM.
 
Wanachokifanya TBC miaka yote ni sahihi?
Mnataka Mbowe aombe radhi kwani amemkosea nani?
Dawa ya Mbowe mtumie video hii hapa ya Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Kigoma alipokamatwa akitapeli watu na hadi sasa yupo Lock up Kigoma
 
Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa Televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020
Kwani TBC ni chombo cha habari umma?
Afadhali Ungesema kipaza sauti cha ccm
 
Hana haja ya kuwaomba radhi. Wao waliipiga vita kampeni ya CHADEMA w siri yeye akajibu wazi. Vyombo vya habari acheni kufanya kazi kwa ubaguzi. Vyama vyote vina haki ya kusikiwa na watanzania wote. Ni kweli mlikuwa mnakata hotuba za wazungumzaji katika mkutano huo. Ile ni hujuma ya wazi. Vyama vya vyote vya siasa nchini Tanzania ni vyama vya watanzania. Wote wana haki sawa kikatiba na kisheria. Wote wanahitaji mazingira sawa katika kampeni hadi kwenye uchaguzi. Anaeshinda ashinde kwa haki na anaeshindwa ashindwe kwa haki. Msifanye hila katika Nazi.​
 
Lawama kwa TBC ziko kwa miaka mingi sana kwa upande mmoja ni kweli TBC ilikua vizuri sana chini ya Tido Mhando ikawa chombo chenye heshima sana.

Lakini baadae mambo yakabadilika walipomtoa TIDO.
Hivi sasa watu wanailaumu TBC na tasnia ya habari kwa kiasi kikubwa kwamba imekua inalalia upande mmoja kuna mikutano mingine wakionyesha hutaona hata kidogo kupepesuka kwa tangazo na mingine wakionyesha wanakata kila mara matangazo.Kwa hali hiyo TBC wanalaumiwa sana.
Ni vizuri wao wenyewe wajiangalie nyie wengine inaeleweka wandishi wa siku hizi kuna shida sana tasnia hiyo.
 
Je, vipi kule Lindi wakati 'Bwege' anaongea na alipotaja tu Lissu sauti ilipotelea wapi? Je, na kwenye mikutano ya CCM sauti upotea? Huyo Irene Mark si angesubiri mpaka game liishe ndio atoe hayo matamko yake. Hivi ana kiwango gani cha elimu? Na aliipatia wapi?
 
Watoto wa chekeachea ukiwapelekea hoja za aina hii, watakufa kwa kucheka. Polepole anazidi kuwafanya muonekane vituko.
Halafu hao Chadema ndiyo wanaomba ridhaa ya kuchukua nchi Oct 28,moja ya Sera zao n Uhuru wa vyombo vya habari,hv mtu Kama huyo umpe nchi aiongoze itakuwaje,some time tuacheni mizaha jamani,hawafai hao hata kwa ubalozi wa nyumba kumi
 
kwa sentensi hii ni na mashaka kama hawa watu hawatakuwa wamenunuliwa na kutumika , nanukuu,

''''' Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu''' .

kwenu haivumiliki , TBC aidha inavumilika , hamjui siasa ina makorokoro mengi ya hila . Mmoja wapo kaona hila na yeye kachukua hatua . ili wasikwazane . Tangu lini shetani akalipeleka kanisa la yesu mbinguni na hata kusema nililichunga vyema , haipo hiyo . shetani hubaki ni shetani tu .
 
Mbona kama Serikali ndio inawadhalilisha zaidi kwa kufikiri kwa niaba yso???.
 
Ni vyema kwanza TBC ieleze umma kwa nini ubora wa matangazo yao siku hiyo ulikuwa ni hafifu sana na kukatika mara kwa mara. Lakini mikutano ya watu wengine ubora unakuwa mzuri. Ni kwa nini kama siyo hujuma?
 
Back
Top Bottom