LGE2024 Tamko la kutangaza siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa siku ya mapumziko la mwaka 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
TAMKO LA KUTANGAZA SIKU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA SIKU YA MAPUMZIKO LA MWAKA 2024

KWA KUWA kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35, kinampa Rais mamlaka ya kutangaza siku yoyote kuwa siku ya mapumziko kama nyongeza ya siku zilizoainishwa kwenye Jedwali la Sheria hiyo au kubadili siku yoyote kati ya zilizoainishwa na siku nyingine na siku hiyo kuwa siku ya mapumziko kama vile imetajwa kwenye Jedwali la Sheria;

NA KWA KUWA tarehe 27 Novemba, 2024, Jumatano, ambayo ni siku ya kazi, imetangazwa na Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuwa Siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024;

NA KWA KUWA kwa madhumuni ya kuwezesha watu wote wenye sifa ya kupiga kura kutumia haki yao ya kupiga kura na KWA KUWA kuifanya siku hiyo ya uchaguzi kuwa siku ya mapumziko kutatoa fursa kwa wananchi wengi zaidi kushiriki kikamilifu katika kupiga kura, Rais anakusudia kutangaza Siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa siku ya mapumziko;

KWA HIYO BASI, kwa mamlaka aliyopewa Rais chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35, mimi, SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatoa Tamko kuwa tarehe 27 Novemba, 2024 itakuwa siku ya mapumziko.

Tamko hili limetolewa na kuwekewa Lakiri ya Umma leo tarehe 22 Novemba 2024.

IMG-20241124-WA0028.jpg
 
Wakuu,

Ni siku ya mapumziko kwaajili ya kupiga kura, sio kubaki mmelala tu majumbani au kwenda kula bata 🌚 🌚 🌚

TAMKO LA KUTANGAZA SIKU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA SIKU YA MAPUMZIKO LA MWAKA 2024 ...jpg

TAMKO LA KUTANGAZA SIKU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA SIKU YA MAPUMZIKO LA MWAKA 2024

KWA KUWA kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35, kinampa Rais mamlaka ya kutangaza siku yoyote kuwa siku ya mapumziko kama nyongeza ya siku zilizoainishwa kwenye Jedwali la Sheria hiyo au kubadili siku yoyote kati ya zilizoainishwa na siku nyingine na siku hiyo kuwa siku ya mapumziko kama vile imetajwa kwenye Jedwali la Sheria;

NA KWA KUWA tarehe 27 Novemba, 2024, Jumatano, ambayo ni siku ya kazi, imetangazwa na Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuwa Siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024;

NA KWA KUWA kwa madhumuni ya kuwezesha watu wote wenye sifa ya kupiga kura kutumia haki yao ya kupiga kura na KWA KUWA kuifanya siku hiyo ya uchaguzi kuwa siku ya mapumziko kutatoa fursa kwa wananchi wengi zaidi kushiriki kikamilifu katika kupiga kura, Rais anakusudia kutangaza Siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa siku ya mapumziko;

KWA HIYO BASI, kwa mamlaka aliyopewa Rais chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35, mimi, SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatoa Tamko kuwa tarehe 27 Novemba, 2024 itakuwa siku ya mapumziko.

Tamko hili limetolewa na kuwekewa Lakiri ya Umma leo tarehe 22 Novemba 2024.
 
Ni jambo jema sana na hata watumishi wa umma wamefurahi sana .na kusema kuwa wao na familia zao na marafiki zao na ndugu zao wanakwenda kumimina kura za ndio kwa wagombea wa CCM tu .ambao ndio wenye kujua shida na changamoto za watu na wenye uwezo wa kushirikiana na wananchi kuwaletea maendeleo na kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
 
Unaishi Dodoma maeneo gani? Mirembe?
 
kiulweli, hili halikuwa wazo zuri, watu wangeweza kupiga kura na kwenda makazini, kuna watu wako dodoma na dar kikazi, wamejikuta wanapata wrong weekend, kuna malipo ya kibenk abayo hufanyika work days, yamesogezwa mbele. na kimsingi watumishi wengi hawakuwa wamejiandikisha
 
Back
Top Bottom