TAMKO LA MWENYEKITI Baba V Kuhusu Uenyekiti wa Tume ya Mahusiano na Ndoa Chit chat.

TAMKO LA MWENYEKITI Baba V Kuhusu Uenyekiti wa Tume ya Mahusiano na Ndoa Chit chat.

Baba V

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Posts
19,479
Reaction score
9,551
Ndugu wapendwa na wadau wa chit chat, Amani kwenu. Awali ya yote ningependa kumshukuru Mwenye enzi MUNGU kwa kuendelea kutujaalia uzima na afya bure kwa kila mmoja wetu.

Leo nimekuja ili kuweka kumbukumbu sawa baada ya kimya cha kadri tangu bwana mdogo Erickb52 atangaze uasi na kudai "eti amenipindua". Kimya changu hakikumaanisha kuwa nimekubaliana na "mapinduzi uchwara" La hasha, Nilikuwa kimya kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo kushughulikia Migogoro ya Kidplomasia katika mataifa ya Syria na Sudan, lakini pia nilitaka kujua hasa nini sababu ya hiki "kimuhemuhe" cha madaraka alichokuwa nacho huyu Erickb52 na baada ya kupata majibu nimeamua kuja kuweka kumbukumbu sahihi hapa jamvini. Najua baadhi yenu hamumjui Erickb52 kwa undani na nitachukua nafasi hii kuwajulisha.

Erickb52 ni nani..!??
Nimemfahamu huyu bwana mdogo wakati wa vita ya Iraq wakati huo mimi na yeye tukiwa katika jeshi la Marekani yeye kama SEAL na mimi nikiwa mshauri mkuu wa kiufundi katika medani za kivita tukiwa kama "mercenaries" (hapa watu8 atafafanua maana ya mercenary) na huku ndiko alikopata jina la B2 kutokana na uwezo wake wa kubinuka na ile midege ya kimarekani, tangu akiwa huko alikuwa ni mtu mkorofi, mpenda sifa na kupenda vyeo hata ambavyo havimudu.

Erickb52 na chit chat.
Hapa chit chat Erickb52 alikuwa kama members wengine tu hadi pale nilipounda Tume ya mahusiano na ndoa hapa chit chat na kumteua kwenye kamati ya SCREENING akishirikiana na Mamndenyi na Ruhazwe JR a.k.a Lundenga. Jukumu lao lilikuwa ni kupitia taarifa za wanaotaka kuingia kwenye ndoa kuona kama hawako katika mahusiano mengine yanayoweza kuleta migogoro, wakijiridhisha wanayapeleka kwenye kamati ya sheria ambayo inaundwa na Judgement ruttashoborwa na kipipi ambao baada ya kujiridhisha na vigezo vya kisheria wanatoa "go ahead" kwangu na wasaidizi wangu watu8 na gfsonwin kwa ajili ya kupitisha ndoa husika. Niliamua kuivunja "screening committee" baada ya kupata malalamiko mengi kuwa Erickb52 alikuwa akiwaomba rushwa ya penzi wadada walioenda kwake kwa ajili ya Screening na kwamba wakigoma alikuwa anawaundia zengwe. Sababu nyingine iliyopelekea kuvunjwa kwa screening committee ni maombi ya Mamndenyi kuwa asingeweza kufanya kazi kwa uhuru kwenye kamati moja na mwanae Ruhazwe JR. Kwa kuzingatia hayo nikaivunja screening committee.

Kufeli kwa Erickb52.

Kama ambavyo alifeli jeshini, kwenye screening committee na katika ndoa ndivyo ambavyo Erickb52 atafeli katika kila nafasi atakayoshika.

i. Amefeli ku maintain ndoa na ndo maana mbali ya kuwa na Chocs akikatiza binti mbele yake hamwachi, sikumbuki ni lini alitemana rasmi na kipipi na wengineo kabla ya kujitwisha Chocs. Itakuwa ni uwendawazimu kumpa dhamana ya kusimamia ndoa za watu mtu ambae ndoa yake tu imemshinda.

ii. Amekosa maono na si mbunifu, juzi amekuja ku verify ndoa ambazo tayari nilishazifungisha na nyingine zilikuwepo hata kabla ya uongozi wangu, na ameshindwa ku acknowledge "long standing couple" ya King'asti na Paw kutokana chuki na hasira zake kwa couple hii. HII SIO SIFA YA KIONGOZI, kama ameweza kuutenda hivi mti mbichi ( Paw ) itakuaje kwa miti mikavu!??

iii. Katika siku chache alizo "jisingizia" madraka ameingia katika migogoro na members Arushaone baada ya kuona mawasiliano yanayotia shaka kwenda kwa mkewe kipenzi Lady doctor na pia ameingia katika mzozo mkali na baunsa zubedayo_mchuzi baada ya kumlazimisha ndoa kitendo kilichopelekea baunsa atoe masaa 72 tu vinginevyo angemu westgate mall. Haifai kwa kiongozi kuwa hivyo.


HITIMISHO.
Napenda kuwatangazia wana chit chat wote kuwa mimi sijapinduliwa na sijawahi kufikiria kupinduliwa na mtu much less by Erickb52, Hivyo basi mimi ni mwenyekiti na nitaendelea kuwa mwenyekiti hadi pale nitakapoamua vinginevyo.

Napenda pia niwatangazie kuwaongezea Mzee na Kaizer kwenye jopo la washauri wa masuala ya ndoa, hawa wanaungana rasmi na wazee wenye busara zao Bishanga na Mtambuzi katika usuluhishi wa migogoro ya ndoa ambayo kama itashindikana ndipo itaenda kwenye kamati ya sheria.

Pia ninawatangazia rasmi kuundwa kwa chit chat Brigade ambayo hadi sasa ni operational with effect from tarehe 18 September 2013, ikiongozwa na kamanda Heaven on earth na Lt.Colonel Slave a.k.a Samaji samaki. hii brigade ina jukumu la kuwalinda viongozi na wanachama wa chit chat ndani na nje ya mipaka ya chit chat. Aluta continua.
CC Vin Diesel, Arabela, measkron, nitonye, The secretary, charminglady Madame B, BADILI TABIA, Himidini, Filipo, marejesho, Mr Rocky , KakaKiiza, DEMBA, sweetlady, Dark City , KOKUTONA, Mrembo by Nature, Asnam, ladyfurahia, Elli , Mentor , snowhite, cacico, Asprin, kyanaKyoMuhaya , Mamzalendo , Mwanyasi, C6 , kiwatengu , shansarie, Paloma, Mtambuzi, sosoliso , Dena Amsi , UNDENIABLE amu , wise lady , Mwita Maranya, Ben Saanane, Gwangambo, Gwamahala, Bujibuji , green city
 
Last edited by a moderator:
Jamani Baba V mbona mwanakamati uliyenipa ( Mtambuzi) ni mkimbizi haramu na operesheni kimbunga imemtupa Goma?
Hizi tuhuma kuhusu Erickb52 kama ni za kweli basi ni bora Chocs achukue ukimbizi aje akae kwenye li apartment langu masaki.

Naskia UN wame mclear Mtambuzi na jana nimepishana nae maeneo ya Tabata, Kuhusu hilo ondoa shaka mkuu. Yeye sasa ni raia halali wa nchi hii.
 
Last edited by a moderator:
Mkubwa Baba V hao mared brigade ni masali??
Heaven on earth kila siku anaongoza mapambano ya kukupindua???
Mzee rekebisha wanaokupigania
 
Last edited by a moderator:
Naskia UN wame mclear Mtambuzi na jana nimepishana nae maeneo ya Tabata, Kuhusu hilo ondoa shaka mkuu. Yeye sasa ni raia halali wa nchi hii.

Ukisema wewe sitii neno,halafu nasikia jana Chocs kamfumania Erickb52 na nke ya jirani,jamaa kala kibondo mpaka kiuno kimeteguka,eti mwenyekiti pheeeeeewwww!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Duuh.. Ngoja nimuatendi kwanza shemeji yenu Paloma.. Anaumwa hapa akipata nafuu nitarudi na maswali na majibu yake lol..
 
Last edited by a moderator:
Naskia UN wame mclear Mtambuzi na jana nimepishana nae maeneo ya Tabata, Kuhusu hilo ondoa shaka mkuu. Yeye sasa ni raia halali wa nchi hii.
Ahsante kwa kuweka kumbukumbu hii vizuri maana mengi yamesemwa sana humu na watu wameendelea kunichafua, nawatumia salaam kwamba nimerudi na niko timamu na kwa sasa naongea na wanasheria wangu Rutashobolwa na Kaizer namna ya kuwafikisha wahusika katika mikono ya sheria hasa huyu Bishanga kanichafua sana.

Mimi nilikwenda Goma kwa special mission sasa iweje aje hapa na kunitangazia ukimbizi..?

It will it on their side.....
 
Last edited by a moderator:
mimi sipendi tabia yako ya kunitaja taja kwenye sector zako za ajabu ajabu,ungenipanga kwenye kitengo nyeti cha uhasibu ningekuona wa maana.Hujambo Baba V

Mie sijambo wangu, afu nimekumiss sana ujue, nimerudi toka Singida juzi nikiwa na mihela ya vitunguu... nakutafuta sana aisee...
 
Mkubwa Baba V hao mared brigade ni masali??
Heaven on earth kila siku anaongoza mapambano ya kukupindua???
Mzee rekebisha wanaokupigania
amu nasubiri kuapishwa tu kazi nianze, nitawapenda sana iwapo mtakuwa na nidhamu ya woga kwa vigogo. kwa sasa namalizia kuokoa mateka hapa westgate muda mchache nitakuwa hapo chit-chat
 
Last edited by a moderator:
Mkubwa Baba V hao mared brigade ni masali??
Heaven on earth kila siku anaongoza mapambano ya kukupindua???
Mzee rekebisha wanaokupigania

Hahaha hawa Red Brigade ni kundi maalum kwa ajili ya Ulinzi, Heaven on earth amekuwa secret service aki operate kwenye covert operations nyingi akinipigania, na kwa sasa nimemkabidhi kitengo rasmi.
 
Last edited by a moderator:
Ukisema wewe sitii neno,halafu nasikia jana Chocs kamfumania Erickb52 na nke ya jirani,jamaa kala kibondo mpaka kiuno kimeteguka,eti mwenyekiti pheeeeeewwww!!!!!

Yule mbona majanga... Kesho utamuona na picha zake kwenye JF udaku..
 
Ha haha haha .....!@baba V nadhani hapo kwa Bishanga hapo paangalie upya.Ana historia ya kung'ang'ania ma-ex wake hata kama wame-move on!

CC: Madame B

Ukiona Nyani mzee ujue kakwepa mishale mingi, najua atautumia vizuri uzoefu wake katika mapenzi kutoa ushauri.:nod::nod::nod:
 
Back
Top Bottom