TAMKO LA MWENYEKITI Baba V Kuhusu Uenyekiti wa Tume ya Mahusiano na Ndoa Chit chat.

TAMKO LA MWENYEKITI Baba V Kuhusu Uenyekiti wa Tume ya Mahusiano na Ndoa Chit chat.

sasa wewe umeshindwa kazi ya kuwa kiongozi bora unataka nini tena kama sio kumpendekeza kaka yangu ashike wadhifa huo ili taifa la cc llisonge mbele, hebu vua magamba hapa
Ndugu wapendwa na wadau wa chit chat, Amani kwenu. Awali ya yote ningependa kumshukuru Mwenye enzi MUNGU kwa kuendelea kutujaalia uzima na afya bure kwa kila mmoja wetu.

Leo nimekuja ili kuweka kumbukumbu sawa baada ya kimya cha kadri tangu bwana mdogo Erickb52 atangaze uasi na kudai "eti amenipindua". Kimya changu hakikumaanisha kuwa nimekubaliana na "mapinduzi uchwara" La hasha, Nilikuwa kimya kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo kushughulikia Migogoro ya Kidplomasia katika mataifa ya Syria na Sudan, lakini pia nilitaka kujua hasa nini sababu ya hiki "kimuhemuhe" cha madaraka alichokuwa nacho huyu Erickb52 na baada ya kupata majibu nimeamua kuja kuweka kumbukumbu sahihi hapa jamvini. Najua baadhi yenu hamumjui Erickb52 kwa undani na nitachukua nafasi hii kuwajulisha.

Erickb52 ni nani..!??
Nimemfahamu huyu bwana mdogo wakati wa vita ya Iraq wakati huo mimi na yeye tukiwa katika jeshi la Marekani yeye kama SEAL na mimi nikiwa mshauri mkuu wa kiufundi katika medani za kivita tukiwa kama "mercenaries" (hapa watu8 atafafanua maana ya mercenary) na huku ndiko alikopata jina la B2 kutokana na uwezo wake wa kubinuka na ile midege ya kimarekani, tangu akiwa huko alikuwa ni mtu mkorofi, mpenda sifa na kupenda vyeo hata ambavyo havimudu.

Erickb52 na chit chat.
Hapa chit chat Erickb52 alikuwa kama members wengine tu hadi pale nilipounda Tume ya mahusiano na ndoa hapa chit chat na kumteua kwenye kamati ya SCREENING akishirikiana na Mamndenyi na Ruhazwe JR a.k.a Lundenga. Jukumu lao lilikuwa ni kupitia taarifa za wanaotaka kuingia kwenye ndoa kuona kama hawako katika mahusiano mengine yanayoweza kuleta migogoro, wakijiridhisha wanayapeleka kwenye kamati ya sheria ambayo inaundwa na Judgement ruttashoborwa na kipipi ambao baada ya kujiridhisha na vigezo vya kisheria wanatoa "go ahead" kwangu na wasaidizi wangu watu8 na gfsonwin kwa ajili ya kupitisha ndoa husika. Niliamua kuivunja "screening committee" baada ya kupata malalamiko mengi kuwa Erickb52 alikuwa akiwaomba rushwa ya penzi wadada walioenda kwake kwa ajili ya Screening na kwamba wakigoma alikuwa anawaundia zengwe. Sababu nyingine iliyopelekea kuvunjwa kwa screening committee ni maombi ya Mamndenyi kuwa asingeweza kufanya kazi kwa uhuru kwenye kamati moja na mwanae Ruhazwe JR. Kwa kuzingatia hayo nikaivunja screening committee.

Kufeli kwa Erickb52.

Kama ambavyo alifeli jeshini, kwenye screening committee na katika ndoa ndivyo ambavyo Erickb52 atafeli katika kila nafasi atakayoshika.

i. Amefeli ku maintain ndoa na ndo maana mbali ya kuwa na Chocs akikatiza binti mbele yake hamwachi, sikumbuki ni lini alitemana rasmi na kipipi na wengineo kabla ya kujitwisha Chocs. Itakuwa ni uwendawazimu kumpa dhamana ya kusimamia ndoa za watu mtu ambae ndoa yake tu imemshinda.

ii. Amekosa maono na si mbunifu, juzi amekuja ku verify ndoa ambazo tayari nilishazifungisha na nyingine zilikuwepo hata kabla ya uongozi wangu, na ameshindwa ku acknowledge "long standing couple" ya King'asti na Paw kutokana chuki na hasira zake kwa couple hii. HII SIO SIFA YA KIONGOZI, kama ameweza kuutenda hivi mti mbichi ( Paw ) itakuaje kwa miti mikavu!??

iii. Katika siku chache alizo "jisingizia" madraka ameingia katika migogoro na members Arushaone baada ya kuona mawasiliano yanayotia shaka kwenda kwa mkewe kipenzi Lady doctor na pia ameingia katika mzozo mkali na baunsa zubedayo_mchuzi baada ya kumlazimisha ndoa kitendo kilichopelekea baunsa atoe masaa 72 tu vinginevyo angemu westgate mall. Haifai kwa kiongozi kuwa hivyo.

HITIMISHO.
Napenda kuwatangazia wana chit chat wote kuwa mimi sijapinduliwa na sijawahi kufikiria kupinduliwa na mtu much less by Erickb52, Hivyo basi mimi ni mwenyekiti na nitaendelea kuwa mwenyekiti hadi pale nitakapoamua vinginevyo.

Napenda pia niwatangazie kuwaongezea Mzee na Kaizer kwenye jopo la washauri wa masuala ya ndoa, hawa wanaungana rasmi na wazee wenye busara zao Bishanga na Mtambuzi katika usuluhishi wa migogoro ya ndoa ambayo kama itashindikana ndipo itaenda kwenye kamati ya sheria.

Pia ninawatangazia rasmi kuundwa kwa chit chat Brigade ambayo hadi sasa ni operational with effect from tarehe 18 September 2013, ikiongozwa na kamanda Heaven on earth na Lt.Colonel Slave a.k.a Samaji samaki. hii brigade ina jukumu la kuwalinda viongozi na wanachama wa chit chat ndani na nje ya mipaka ya chit chat. Aluta continua.
CC Vin Diesel, Arabela, measkron, nitonye, The secretary, charminglady Madame B, BADILI TABIA, Himidini, Filipo, marejesho, Mr Rocky , KakaKiiza, DEMBA, sweetlady, Dark City , KOKUTONA, Mrembo by Nature, Asnam, ladyfurahia, Elli , Mentor , snowhite, cacico, Asprin, kyanaKyoMuhaya , Mamzalendo , Mwanyasi, C6 , kiwatengu , shansarie, Paloma, Mtambuzi, sosoliso , Dena Amsi , UNDENIABLE amu , wise lady , Mwita Maranya, Ben Saanane, Gwangambo, Gwamahala, Bujibuji , green city
 
sasa wewe umeshindwa kazi ya kuwa kiongozi bora unataka nini tena kama sio kumpendekeza kaka yangu ashike wadhifa huo ili taifa la cc llisonge mbele, hebu vua magamba hapa

Hivi unajitambua kuwa wewe bado ni katibu muhtasi wangu!? au hujielewi!?
 
Haya sasa mie yangu macho, nitaunga mkono upande utakaotangaza dau kubwa, hapa napokea rushwa kwa kila mtu. Ukubwa wa rushwa yako ndio kuungwa mkono na mie!!! Fulana na kanga sizitaki, nataka pesa! Tungepata na mtu wa mahesabu tungefahamu kiasi kilichotumika kwenye maandali ya kamati hizi na mapinduzi haya
 
@Baba v
wakati mwingine tujikumbushe mambo ya muhimu kama haya;
tuachane na hawa madogo wasitutie hasira.
IMANI YA CCM

  • Binadamu wote ni Sawa
  • Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
  • Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja

(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

(3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.

(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.

(7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.
aione pia chama
 
hivi hiyo inatumika eeee?
 
Unanikumbusha enzi zile CCM ni chama kweli cha wakulima na wafanyakazi, sio hii ccm masalia ya wafanyabiashara, hell no...!! huwa naumia sana nikiona wazee wenzangu wanaoifahamu CCM halisi kama akina Butiku wakishindwa kufanya lolote la maana kwa chama hiki kutokana na wafanyabiashara kukiteka chama. aaaaaaarghhhh..!!!!!!:heh::heh::heh:
 
Dhidi ya mapinduzi haya mengine....

Dogo mie sikuwahi kupinduliwa hata siku moja, nyie ndo mliodanganywa kuwa huyo dogo alinipindua mimi mkaingia mtegoni, kuwa makini kijana.., Nina nafasi kubwa sana ya kuamua maisha yako ya kimahusiano..
 
Back
Top Bottom