Tamko la Shura ya Maimamu kufuatia Jeshi la Polisi kuwashikilia Viongozi wa CHADEMA

Tamko la Shura ya Maimamu kufuatia Jeshi la Polisi kuwashikilia Viongozi wa CHADEMA

Joined
Sep 19, 2019
Posts
43
Reaction score
383
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

TAMKO LETU KUFUATIA JESHI LA POLISI NCHINI KUWASHIKILIA VIONGOZI WA CHADEMA

Shura ya Maimamu Tanzania tumefuatilia kwa kina tukio la Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendrleo CHADEMA. Tumejiridhisha tukio hilo ni ukandamizaji wa Demokrasia na haki za binadamu.

Tumepokea tukio hili kwa masikitiko makubwa.

Kushikiliwa kwa Viongozi hao wa CHADEMA na baadhi ya wanachama hao, kumetokea muda mchache kabla ya kufikia tarehe ya Kongamano la Kikatiba lilio andaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kufanyika Jijini Mwanza Ukumbi wa Tourist Hotel.

Kukamatwa kwa Viongozi hao ni kiashiria tosha kuwa Jeshi la Polisi nchini lina endeleza hujuma dhidi ya wananchi kwakuwa haki ya kukusanyika na kutoa maoni ni haki ya Kikatiba. Na kuendelea kuwazui Watanzania kutotumia haki yao ni kuvunja Katiba.

Shura ya Maimamu Tanzania inalitaka Jeshi la Polisi Tanzania kuwaachia viongozi wote wa CHADEMA na wanachama wake bila masharti yoyote.

Pia tunazidi kushauri vyombo vya dola ikiwemo Jeshi la Polisi Tanzania, kutoendeleza vitendo vya ukiukwaji haki za raia na kukandamiza uhuru wa watu kujieleza. Kwani vitendo hivi vina leta taswira mbaya kwa taifa letu.

KATIBU MKUU
Shura ya Maimamu Tanzania
Leo tar 23.07.2021
0656654546
 
brazaj, dictators never heed to words, they need actions of whatever type

I agree, but actions start with words. To my opinion, everything is going on essentially very well:

best of you

I see the portion in red amongst the people who matter:

IMG_20210724_124742_610.jpg

Notably, it is not for everybody.
 
Nyie Shura ya Maimamu tulieni fanyeni shughuli zenu kwa mujibu wa katiba yenu. Acheni serikali kupitia jeshi la polisi wafanye shughuli zao hakuna mtu anauawa ni sheria ndio itatumika. Rais aliapa kuilinda katiba na sheria zake zote. We unajuaje km kongamano la katiba ilikuwa geresha tu na kuna mambo yamejificha nyuma ya pazia?

Hawa watu wana mikono mirefu wanafanya kazi hata wakati we unakoroma au unam-do mwenza wako. Hatuchelewi kuja kuilaumu serikali yakitokea yakutokea na tena nyie na mnaofananao ndio mtakuwa wa kwanza kuinyoshea kidole serikali kuwa 'hamjawahi kuona serikali dhaifu km hii kwani hawana vyombo vya usalama'?

Tuna imani na serikali yetu. CHADEMA wameshakosa mwelekeo tangia 2015 wanataka kutumia njia haramu na huruma ya wananchi.
 
Wewe ni mpuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema onyeni vijana wenu kuhusisha kukamatwa kwa mbowe na udini wa mama samia.

Huko wanapokwenda waislamu wenye akili na wapenda haki watashindwa kuwaunga mkono.
 
Back
Top Bottom