TAMKO la TEC: Upo uwezekano baadhi ya ma Baba Askofu hawajui kilichomo

Kamwaga anaandika maneno mengi yakianzia na maneno mawili "upo uwezekano"

Huyu mjinga ametengeneza hisia kichwani mwake, akazijazia na matukio ya kufikirika bila ushahidi wa asilimia 100, then akaandika mada ndefu isiyo na kichwa wala miguu.
Awamu hii ameweka akili mfukoni. Akijisikia kukosoa anaamsha mzimu wa awamu ya tano. Yupo kwenye praise team ya awamu ya sita.
 
Wewe Kamwaga ni mwandishi Msomi Uchwara!
Size yako ni hao wajinga wajinga kina Maulid kitenge.
Umeitwa kuja kusaidia jahazi la mafisadi


Usomi wako hauna msaada kwa maendeleo ya nchi yetu.

Ndio maana una Paji la uso kuliko idadi ya cell za ubongo.

Nenda kamtafute kiyenge akupeleke na wewe ufanyiwe alichofanyiwa na kupewa gari.

Tanzania ya leo sio ile ya Enzi ya Radio Tanzania Dar es Salaam RTD.
 
Bado unaleta habari zilizotungwa ambazo hazikuwahi kuwa na ukweli. Hiki ulicholeta hakijafikia viwango vya kuitwa habari. Hiki ni maoni kulingana na either uelewa au nia ya aliyeandika, lakini si habari hii.
Pengo alikua sehemu ya waliouandika Waraka ule na kamwe hakuwahi kuukataa isipokua alisema hakujua kama ungetoka. Wote tunajua jinsi Pengo alivyobaki pekee, hukubWakatoliki wakimpuuza kwa Unafiki wake. Alimuunga mkono Magufuli huku akiwakosoa wanaoipinga serikali wakati kipindi cha Kikwete yeye ndiye alikua Kinara kumpinga Kikwete.

Maneno ya Pengo haya hapa;
Mwadhama Kadinali Polycap Pengo amesema hakuwa anajua kama kuna waraka utatolewa kuhusu kwaresma na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania huku akisema waraka huo una mazuri mengi japo umechanganya dini na siasa.
Kadinali Pengo ameyasema hayo wakati akiadhimisha ibada ya Jumapili ya matawi huko Bagamoyo katika tamasha la vijana.


“Katika wiki chache zilizopita watu wamekuja kwangu wakaniuliza unaionaje ile barua ya Maaskofu kuhusu Kwaresma mwaka huu? Ninazungumzia hilo na wala mtu asiende aka-quote kitu kingine ndio maana nataka kusema wazi kabisa:-
“Barua ile ijapokuwa hata jina langu mnaliona limeandikwa pale kwamba na mimi ni mmoja wa waandishi au watamkaji…mimi nimeipokea, baadhi yenu mmeshaipokea.
” Kwahiyo sioni namna gani mimi naweza kuwa mwandishi au mhubiri kwenu wa ile barua ambayo imetungwa labda na maaskofu…naamini na baadhi ya maaskofu lakini mimi mwenyewe hata nilikuwa sijaiona, hata nilikuwa sijaambiwa kuna kitu cha namna hiyo kinakuja.
“Tuelewane vizuri, ninaposema hivi sitaki kusema ile barua ni mbaya. Moja tu ni kwamba barua nzima imechanganya vitu viwili; Mwalimu angekuwepo angepiga kelele Maaskofu msichanganye Dini na Siasa.
“Angepiga kelele sana kuhusu waraka huu katika nyakati zake. Na hilo nawambia sina hofu, muende mkamwambie mtu yeyote nimesema hivi. Ndio wala msione aibu, najua labda hata wengine mmekunja nyuso, kunjeni tu lakini huo ndio msimamo wangu.
“Zipo sehemu katika waraka huo zinazochanganya Dini na Siasa na si kazi ya maaskofu ni kazi yenu wanasiasa mkiwa ni wa CHADEMA, mkiwa ni wa CCM lakini haiwezi kuwa kazi yangu mimi.
“Siwezi kwanza nikaanza kuchambua na ku-criticize Serikali katika mambo yaliyo yake; sikupewa mamlaka hayo. Na kwanini niwe padri mpaka nikubali kuwa Askofu na huku kumbe wito wangu ni siasa?
 
Uwaelimishe na njiwa wenzio hilo jambo waache kuja na vikashfa vyao uchwara wakidhani wanafanana nao

Mimi ni mchagga natumia mbege
[emoji1787][emoji1787]

Mtimilifu wa fikra huwa hafanyi "generalization" katika "mtawanyo wa mambo"....

Kuna mtu anasema kuwa TEC haina wasomi wabobevu ?!! [emoji1787][emoji1787]

Nitampinga asemaye hayo kwa kumrekebisha kuwa aseme "Kwa usomi mkubwa walionao TEC wanaweza pia kupotosha kimakusudi" [emoji1787][emoji1787]

Haya shemeji....nakandamiza "mma" hapa kwa shem wangu mama Lily wa Kiraracha
 
Unahamisha magoli ?!!

Acha kupiga "dochi" mpira wa kuusukuma tu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Humu JF hakuna aliyezaliwa 2019...[emoji1787]
Huwa sihami kwenye hoja hata siku moja. Nilichokujibu ndicho. Huyo mwandishi wenu ameumba story ambayo haikuwahi kuwepo ili apate pa kusimamia kuijenga hoja yake.
 
Kamwaga amewaumbua mlisema TEC inampinga mama kisa dini, kumbe walimpinga hata Magufuli mwenzako kwenye ukatoliki.
Usifanye "generalization"...

Kila mtu na aaminicho....

Binafsi siamini kuwa TEC inampinga mh.Rais SSH kisa dini yake....bali inapigania maslahi yake kule bandarini...[emoji1787][emoji1787]

Ni sawa na masheikh wangu wa BAKWATA walivyopigia kelele "ile kodi" ya bandari....

Mjini hapa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wanatengenezo story wapate kusimika hoja zao. Pengo alitofautiana na wenzake lakini hakuwahi kukataa kushiriki kuuandika ule Waraka bali alileta siasa tu.

 
Bams unazunguuukaaaa [emoji1787][emoji1787]

Ni dhahiri Mwadhama P.Pengo hakukubaliana na waraka ule....kwani yeye hazijui taratibu za kanisa ?!!!

Hata aje malaika hawezi kuchomoa hili la KUGHUSHIWA kwa ile saini yake [emoji1787][emoji1787]
 

Kwani huyu Kamwaga alitakaje ? Wasitoe waraka ? Pili, Kamwaga anasemaje juu ya zile hoja 8 ndani ya waraka? Achilia mbali wawe wanaelewa wote au wachache ? Tuwe makini na akili za tumbo
 
Basi hapo mnatamani mpate habari kama hii kwa tamko la TEC juzi humu JF hatutapumia naona mtaandika nyuzi mwezi mzima

Hili la limkataba libovu maaskofu wote na makardinali wameridhia msitegemee kusikia tofauti poleni sana
Shem hofu yako tu [emoji1787]

Mbona kamarada Ezekiel Kamwaga kamaliza [emoji1787]
 

KUMBUKUMBU ZAKO ZINASEMAJE KUHUSU MAASKO WA KATOLIKI WASTAAFU KWENYE TEK.
Unapomzungumzia Pengo pia usimsahau Loibulu
 
Awamu hii ameweka akili mfukoni. Akijisikia kukosoa anaamsha mzimu wa awamu ya tano. Yupo kwenye praise team ya awamu ya sita.
[emoji1787][emoji1787]

Umebaki na "argumentum ad hominem" kulijibu bandiko lake?!!

Chaliii [emoji1787]
 
Msumari umekita haswa...

Nguvu alizotumia Kamwaga kuusukuma msumari katika ubao zimefanikiwa [emoji1787][emoji1787]

"Ubao" umebaki na ARGUMENTUM AD HOMINEM tu...chaliii chaliii chaliii [emoji1787]

Jandoni hapa...utake usitake tutabaki na ZUNGA lako [emoji1787]

Karibu Wanzuki [emoji120]

#SiempreJMT[emoji120]
 
Waraka wa TEC hata ungeandikwa na BAKWATA, mtu binafsi au taasisi yoyote iwe au isiwe ya kidini, unahitaji kujibiwa kwa hoja.

Watu wanahangaika sana kuhoji kwanini TEC, mbona hawastahili.

Nijuacho, TEC hawatamjibiu mtu. Washamaliza wajibu wao.

Nina amini utekelezaji kuhusu bandari na DPW utaendelea tu. Lakini muda ni hakimu mzuri daima ingawa kwa maumivu.

Hata kama tusingependa TEC kufanya walicho fanya, Je, kilichoandikwa sio Cha kweli?

Ingekuwa kilicho andikwa ni uongo au upuuzi tu bila shaka watu wange dharau na kupuuza.

Lakini kwa kuwa ni hoja za maana ndio maana wasiopendezwa wanaubatiza waraka na waliouandaa kuwa ni wachochezi.

Sasa si wapelekwe mahakamani, wasirudie tena siku nyingine?

Au wafutwe katika daftari la usajili?

Tuzoee kukosoana.
 
Kaka kamwaga hapa kuna mambo mawili umeyaleta...
1.Nani kasema?
2.Kasema nini?

Umeandika vyema kaka na ndio maswali mengi yapo pia ?

Ila Nafikiri mkataba wa bandari una shida mahali ndio maana kuna kelele nyingi,na hapo kwenye mkataba hata ukiwauliza vizuri waliosaini kunahatihati wasijue yote yaliyomo mule.

Wasilazimishe mambo na sioni haja ya viongozi kuwajibu tec bali warudi chini wajitafakari na waambie wapunguze ulafi na kuna dalili pia kundi kubwa halina imani na viongozi wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…