TAMKO la TEC: Upo uwezekano baadhi ya ma Baba Askofu hawajui kilichomo

TAMKO la TEC: Upo uwezekano baadhi ya ma Baba Askofu hawajui kilichomo

Mosi, hadi sasa ni Askofu nani amelikana Hilo TAMKO?

Pili, kama Mkapa hakushauri ndio inaondoa uhalali wa SAMIA kushauriwa Leo? Je umelisoma TAMKO au na wewe umepita mbimbio tu? Hujasoma mahala wameandika kuhusu madhara ya uuzaji na WA rasilimali uliofanywa huko nyuma?

Je ni ulishawahi kuona siku Moja TEC Wametoa TAMKO la pamoja na viongozi wa dini nyingine? Na je kama hawakuafikiana? Na mwitiko wa hao viongozi wengine baada ya TAMKO haitoshi kukwambia kuwa hao viongozi wengine hawakukubaliana na TEC ?
 
Kaka kamwaga hapa kuna mambo mawili umeyaleta...
1.Nani kasema?
2.Kasema nini?

Umeandika vyema kaka na ndio maswali mengi yapo pia ?
Lini wananchi wote wa tawala zote wakawa na imani na viongozi wao?

Unatuletea hekaya za "illusions"?!! [emoji1787]
 
Lini TEC ilitoa waraka kipindi cha awamu ya 3 ya utawala wa nchi hii?!!

Lini ?!! [emoji1787][emoji1787]
 
Sababu ya muda na utunzwaji wa kumbukumbu lkn waraka wa KWARESMA ni Kila mwaka Sasa huko nyuma hata cm mm ckuwa nayo lakini ukienda maktaba ya TEC utaona Matamko yote ya wakati wa Mkapa
 
Shida kubwa ya jamii yetu au watu-wapagani, ni kwamba hawawezi kutatua matatizo au changamoto zao; au kujenga hoja bila kuangalia shida, hoja, tatizo au changamoto yenyewe.

Kunapotokea tatizo au makosa au changamoto, tunakataa kukabiliana na hali hiyo na badala yake tunatafuta namna ya kuhalalisha udhaifu huo.

Ndio hapo wanawatafuta watu wengine, au vitu au mambo yasioonekana. Hapa utasikia sijui mizimu, sijui mababu, sijui majini, sijui matambiko-miungu, shetani, au Mungu kama sababu au chanzo cha hayo.

Namna hii ya kufikiri ni hatari sana kwa ukuaji na maendeleo ya akili na mwili. Kwa jinsi hii ya kufikiri na kuyaangalia mambo na vitu, mtu au jamii haiwezi kutatua matatizo yake, kusahihisha makosa yake, kugundua au kuboresha achilia mbali uvumbuzi wenyewe.

Kama mtu, au jamii inafanya makosa maana yake kuna shida sehemu fulani na kutatua tatizo hilo sio kushughulika na mtu mwenyewe au jamii yenyewe lakini kutafuta chanzo cha hilo tatizo au shida ni nini.

Tubadilike, tuache kuwaangalia watu, tuangalie jambo lilivyo. Tukubali kukabiliana na ukweli au tabia. Tunapoletewa jambo tuliangalie kwa mapana yote tufanye utafiti mwingi wa kutosha, twenda mbali zaidi ya jambo lenyewe, zaidi faida zake za kiuchumi na kijamii, zaida ya manufaa ya kimwili; lakini manufaa ya kiakili.
 
Maaskfu wote wa Kanisa katoliki wana PHD tena za kusotea darasani siyo za kwenu za kupeana, so wana uhakika na kilichomo na tafiti wamezifanya vilivyo - kwa hiyo ndugu usidanganyike, ule ndiyo msimamo wa wananchi wote wazalendo wa nchi hii.
Kamwaga kanunuliwa kama Kitenge.
 
Inawezekana lakini sio Maaskofu wa Kikatoliki.
Wao, waamini wao na vitu vyao vyote huwa ni kitika umoja,
kuanzia salamu yao Mfano, Kristu-Tumaini Letu au Tumsifu Yesu Kristu-Milele Amina.
Kwahiyo kuhusu maaskofu katoliki nakataa ila maaskofu wengine ikiwa wanetoa waraka uwezekano wako unaweza kuwepo.
 
Argumentum ad hominem....

Utetezi wako dhaifu kupindukia....

Hoja si maaskofu hawajui mambo....hoja ni wao kuamua kusimamia MASLAHI yao kwa kuitumia DINI na wananchi kwa ujumla....

Hebu angalia hili....

Ndani ya ule waraka wao wanadai kuwa kwa miaka 60 Tanzania kutowahi kupata mwekezaji wa bandari kutoka "NJE"...[emoji1787][emoji1787]

Hili ni kweli ?!!!!

Nijibu
Umesoma waraka, Kama hujasoma SEMA nikutumie. Ukishasoma nieleze wapo Kuna kasoro.
 
Huyu ndiye Kamarada Ezekiel Kamwaga nimjuaye [emoji120]

Huyu ndiye mjamaa mwenzangu wa kweli nimjuaye [emoji120]

Hakika amefunguka KISOMI....

"...mwaka 2018 baada ya waraka ule wa TEC ,Kardinal P.Pengo alisema kuwa "alichomekwa bila ya yeye kujua" [emoji1787][emoji1787]

Hebu jiulize watu wanaweza mpaka "kumchomeka" kiongozi wao mkuu ili tu sisi wanywa Wanzuki tuone kuwa ni msimamo mmoja wa kanisa....hatari sana hili....
Kardinali sio kiongozi mkuu wa kanisa katoliki mahali popote pale au katika ngazi yoyote ile katika nchi husika.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa katika Kanisa Katoliki huwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki husika baada ya hapo Kiongozi mkuu ni Papa.

Tangu leo uelewe kwamba Kardinali sio kiongozi wa Kanisa katika nchi fulani. Kuna nchi hazina hata kardinali mmoja na kuna nchi zina Makardinali zaidi ya mmoja.
 
[emoji1787][emoji1787]

Kwanini TEC haikuwahi kutoa waraka wowote kipindi cha awamu ya 3 ya utawala wa nchi hii....

Eager to know[emoji1787]
Unao ushahidi au unajisemea tu? Kama una huo ushahidi ulete hapa na kisha ndiyo uanze kuuliza.
 
Likewise can you disprove it?
Ningeanza mimi ku'claim' burden of proof ingekuwa kwangu. Kwa vile wewe ndiye umeanza, lete huo ushahidi na nitakachofanya mimi ni falsify proof yako kwa kukuletea huo waraka halafu tuone utayeyuka au utageuka jiwe? Kujisemeasemea tu hakusaidii. Tunataka kila mtu aseme kile kilichopo na siyo kubunibuni tu mambo kwa sababu unataka kusema hivyo. Bring that proof that hapakuwa na waraka wowote kwa miaka 10 (yaani) kanisa lili'mute' wakati huo wakati awamu zingine limekua likitoa nyaraka. By the way, ni Benjamin Mkapa tu alikuwa Rais Mkatoliki? Na unadhani Kanisa Katoliki lilimwogopa Mkapa, lakini halikumwogopa Mwalimu Nyerere na Magufuli ambao pia walikuwa Wakatoliki? Argument hapa ni ipi? Na je Mkapa anahusikanaje na wakaka wa TEC kuhusu bandari?
 
Shida kubwa ya jamii yetu au watu-wapagani, ni kwamba hawawezi kutatua matatizo au changamoto zao; au kujenga hoja bila kuangalia shida, hoja, tatizo au changamoto yenyewe.

Kunapotokea tatizo au makosa au changamoto, tunakataa kukabiliana na hali hiyo na badala yake tunatafuta namna ya kuhalalisha udhaifu huo.

Ndio hapo wanawatafuta watu wengine, au vitu au mambo yasioonekana. Hapa utasikia sijui mizimu, sijui mababu, sijui majini, sijui matambiko-miungu, shetani, au Mungu kama sababu au chanzo cha hayo.

Namna hii ya kufikiri ni hatari sana kwa ukuaji na maendeleo ya akili na mwili. Kwa jinsi hii ya kufikiri na kuyaangalia mambo na vitu, mtu au jamii haiwezi kutatua matatizo yake, kusahihisha makosa yake, kugundua au kuboresha achilia mbali uvumbuzi wenyewe.

Kama mtu, au jamii inafanya makosa maana yake kuna shida sehemu fulani na kutatua tatizo hilo sio kushughulika na mtu mwenyewe au jamii yenyewe lakini kutafuta chanzo cha hilo tatizo au shida ni nini.

Tubadilike, tuache kuwaangalia watu, tuangalie jambo lilivyo. Tukubali kukabiliana na ukweli au tabia. Tunapoletewa jambo tuliangalie kwa mapana yote tufanye utafiti mwingi wa kutosha, twenda mbali zaidi ya jambo lenyewe, zaidi faida zake za kiuchumi na kijamii, zaida ya manufaa ya kimwili; lakini manufaa ya kiakili.
Mkuu huku kuna vilaza na wapuuzi a.k.a. mambumbu ambao hawawezi kabisa kukuelewa kabisa!
Na jamii hii ndio inatuchelewesha kutoka hapa tulipo!
 
Back
Top Bottom