TAMKO la TEC: Upo uwezekano baadhi ya ma Baba Askofu hawajui kilichomo

TAMKO la TEC: Upo uwezekano baadhi ya ma Baba Askofu hawajui kilichomo

mtoa mada we ni stupid! Yan pengo umeona ndo wa kumtolea mfano humu! We hujui kama mtu akizeeka sana akili yake inachanganyikiwa? Hujiuliz why now kuna cardinal mpya? Yule now n kama mtoto wa miaka saba! Muachen apumzke
 
Ni vema Kamwaga ajikite kwenye hoja za maaskofu na mkataba baina ya Tanzania na Dubai. Suala la kuchambua uelewa wa askofu mmoja mmoja halimuhusu. Kamwaga akumbuke kuwa hata ndani ya serikali kuna uwajibikaji wa pamoja hivyo siyo kila hoja lazima wote wakubaliane lakini wanapokubali wengi hoja ni ya wote!
Ndugu Kamwaga haandamani dhidi ya "collective responsibility" ya taasisi....laa hashaa [emoji1787]

Ukisoma kwa utulivu UTAMAIZI kuwa amelenga kututanabahisha kuwa kuna wakati hizi NYARAKA za TAASISI zina malengo mengine kabisa....mbali na yale yanayoonekana na sisi "laymen" [emoji1787]

Na kufikia hayo malengo wako radhi wasigane vyovyote....rejea hilo la 2018....

Sasa kwa wao huwa wana "punda afe mzigo ufike" ila DOLA isiwe na "punda afe mzigo ufike"?!!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]

DOUBLE STANDARDS gani hii ?!! [emoji1787]
 
Hivi wewe una maana gani? Issue ya mwaka 2018 unaileta leo ili ionekane ni kuwa ni hii ya kuhusu Bandari. Ukweli ni kuwa kuhusu tamko la juzi, Mwadhama Cardinal Pengo hakuwemo maana ni Askofu Mstaafu. Kwa rejea lipo hapo chini
Kutokuwemo kunazuia mfanano kati ya 2018 na 2023?
 
mtoa mada we ni stupid! Yan pengo umeona ndo wa kumtolea mfano humu! We hujui kama mtu akizeeka sana akili yake inachanganyikiwa? Hujiuliz why now kuna cardinal mpya? Yule now n kama mtoto wa miaka saba! Muachen apumzke
Mkuu kumbuka ni mwaka 2018? alikuwa ameshezeeka tayari kama alivyo sasa?
 
Ni vema Kamwaga ajikite kwenye hoja za maaskofu na mkataba baina ya Tanzania na Dubai. Suala la kuchambua uelewa wa askofu mmoja mmoja halimuhusu. Kamwaga akumbuke kuwa hata ndani ya serikali kuna uwajibikaji wa pamoja hivyo siyo kila hoja lazima wote wakubaliane lakini wanapokubali wengi hoja ni ya wote!
Siku zote ili kuelewa walichoandika ni sahihi kuwajua walioandika
 
Unajua kilichomkuta Pengo kwa hatua ile, au unadhani alistaafu? Kuna usichokijua.
Wenzio wale hawakurupuki ,
Baraza la Maaskofu lina mfumo na misingi yake kwenye kufikia maamuzi ya pamoja.
Sawa....

Kwao "punda afe mzigo ufike" ni sawa?!!!

Ila kwa dola na serikali si sawa ?!!![emoji15][emoji1787][emoji1787]

Hivi kweli wazazi wetu wametupeleka shule kujifunza "ungeseee wa fikra"?!!! [emoji1787]
 
mtoa mada we ni stupid! Yan pengo umeona ndo wa kumtolea mfano humu! We hujui kama mtu akizeeka sana akili yake inachanganyikiwa? Hujiuliz why now kuna cardinal mpya? Yule now n kama mtoto wa miaka saba! Muachen apumzke
Ha ha ha ha ha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Argumentum ad hominem....

Hata aje malaika hakuchomoi "hapa jandoni"....zunga lako kabaki nalo Ezekiel Kamwaga [emoji1787]
 
Bado unaleta habari zilizotungwa ambazo hazikuwahi kuwa na ukweli. Hiki ulicholeta hakijafikia viwango vya kuitwa habari. Hiki ni maoni kulingana na either uelewa au nia ya aliyeandika, lakini si habari hii.
Pengo alikua sehemu ya waliouandika Waraka ule na kamwe hakuwahi kuukataa isipokua alisema hakujua kama ungetoka. Wote tunajua jinsi Pengo alivyobaki pekee, hukubWakatoliki wakimpuuza kwa Unafiki wake. Alimuunga mkono Magufuli huku akiwakosoa wanaoipinga serikali wakati kipindi cha Kikwete yeye ndiye alikua Kinara kumpinga Kikwete.

Maneno ya Pengo haya hapa;
Mwadhama Kadinali Polycap Pengo amesema hakuwa anajua kama kuna waraka utatolewa kuhusu kwaresma na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania huku akisema waraka huo una mazuri mengi japo umechanganya dini na siasa.
Kadinali Pengo ameyasema hayo wakati akiadhimisha ibada ya Jumapili ya matawi huko Bagamoyo katika tamasha la vijana.


“Katika wiki chache zilizopita watu wamekuja kwangu wakaniuliza unaionaje ile barua ya Maaskofu kuhusu Kwaresma mwaka huu? Ninazungumzia hilo na wala mtu asiende aka-quote kitu kingine ndio maana nataka kusema wazi kabisa:-
“Barua ile ijapokuwa hata jina langu mnaliona limeandikwa pale kwamba na mimi ni mmoja wa waandishi au watamkaji…mimi nimeipokea, baadhi yenu mmeshaipokea.
” Kwahiyo sioni namna gani mimi naweza kuwa mwandishi au mhubiri kwenu wa ile barua ambayo imetungwa labda na maaskofu…naamini na baadhi ya maaskofu lakini mimi mwenyewe hata nilikuwa sijaiona, hata nilikuwa sijaambiwa kuna kitu cha namna hiyo kinakuja.
“Tuelewane vizuri, ninaposema hivi sitaki kusema ile barua ni mbaya. Moja tu ni kwamba barua nzima imechanganya vitu viwili; Mwalimu angekuwepo angepiga kelele Maaskofu msichanganye Dini na Siasa.
“Angepiga kelele sana kuhusu waraka huu katika nyakati zake. Na hilo nawambia sina hofu, muende mkamwambie mtu yeyote nimesema hivi. Ndio wala msione aibu, najua labda hata wengine mmekunja nyuso, kunjeni tu lakini huo ndio msimamo wangu.
“Zipo sehemu katika waraka huo zinazochanganya Dini na Siasa na si kazi ya maaskofu ni kazi yenu wanasiasa mkiwa ni wa CHADEMA, mkiwa ni wa CCM lakini haiwezi kuwa kazi yangu mimi.
“Siwezi kwanza nikaanza kuchambua na ku-criticize Serikali katika mambo yaliyo yake; sikupewa mamlaka hayo. Na kwanini niwe padri mpaka nikubali kuwa Askofu na huku kumbe wito wangu ni siasa?
Mkuu mimi nimeleta hoja ya kujadili, na ninaiongezea nyama kwa marejeo mbalimbali. Wewe umekuja na ufafanuzi, jambo jema kabisa. Acha mjadala uendelee
 
Umeandika
Na Ezekiel Kamwaga

KUELEKEA kipindi cha Kwaresma na Sikukuu ya Pasaka ya mwaka 2018, Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) lilitoa waraka ambao kimsingi ulikosoa vitendo vya uminyaji wa demokrasia na uhuru wa watu kujieleza uliokuwepo wakati wa utawala wa hayati Rais John Magufuli.

Waraka ule ulikuwa na sehemu nne lakini sehemu iliyozua mjadala zaidi ilikuwa ni sehemu ya tatu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho; “Dalili za Nyakati Zetu Tanzania” ambapo pamoja na mambo mengine, Maaskofu walieleza kutofurahishwa kwao na maandamano na mikutano ya kisiasa kuzuiwa na vyombo vya dola huku vyombo vya habari vikifungiwa.

Siku chache baadaye, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, alizungumza na vyombo vya habari na kutoa maelezo yaliyokuwa na sura ya kutokubaliana na waraka ule. Kwanza alisema kwamba hakuwa anajua chochote kilichoandikwa ndani ya waraka ule na kwamba jina lake alilikuta tu kwenye lile tamko. Na pili, Pengo ambaye pengine alikuwa ndiye Mkatoliki mashuhuri na anayeheshimika zaidi nchini, alieleza kutokubaliana na yaliyomo kwenye waraka ule – hasa masuala yasiyo ya kidini yaliyojumuishwa humo.

Kuna mambo makubwa mawili ambayo tunaweza kujifunza kutoka kwenye maelezo hayo ya Pengo wakati tukianza kudadavua waraka wa hivi karibuni uliotolewa na TEC kuhusu suala zima la mkataba wa uendeshaji wa bandari za hapa nchini baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai.

La kwanza ni kwamba waraka wa TEC si neno la Mungu. Kama ingekuwa waraka huo ni neno, mtu wa hadhi ya Kadinali Pengo asingeweza kutoka hadharani na kueleza mapungufu ya waraka wa mwaka 2018. Mwadhama Pengo ni mlinzi wa imani ya Kikatoliki na kwa vyovyote vile asingeweza kupingana na jambo lenye kulinda imani au la maelekezo ya Kimungu.

Jambo la pili linahusu wanaosaini waraka. Maelezo ya Pengo yalitufundisha kwamba unapoona waraka umesainiwa na Maaskofu 37 – kama ilivyokuwa kwa waraka uliosomwa kwa waumini Wakatoliki kwenye makanisa ya Tanzania Jumapili iliyopita, si lazima Maaskofu wote wawe wanajua kilichomo. Inawezekana kazi hiyo imefanywa na Maaskofu wachache tu – na wengine hawakujua chochote hadi waraka huo ulipojitokeza; kwanza kwenye vyombo vya habari na pili makanisani.

Na Mwadhama alikuwa na swali moja muhimu alilouliza TEC baada ya waraka ule wa mwaka 2018; kwamba Maaskofu wanajua nini kuhusu haki za kidemokrasia na kubana uhuru wa watu kujieleza? Pengo aliwaambia waandishi wa habari kwamba hayo si maeneo ambayo viongozi wa dini wanayajua zaidi kuliko wanasiasa na vyama vya siasa.

Ndilo swali ambalo pia nadhani Kadinali Pengo angeuliza kuhusu waraka huu wa TEC wa wiki iliyopita. Kwamba Maaskofu wanajua nini kuhusu masuala ya uendeshaji wa bandari? Wanajua nini kuhusu masuala ya haki za kibiashara za Tanzania na nchi nyingine kwenye uwekezaji?

Hili ni swali muhimu kwa sababu; kama Maaskofu wakianza kuhoji kuhusu uwekezaji bandarini, mpaka wa kuhoji utaishia wapi? Nini kitawafanya wasihoji kuhusu gharama za ujenzi wa Reli ya SGR au Bwawa la Mwalimu Nyerere? Kama wanaruhusiwa kuhoji uwekezaji bandarini, nini kitawazuia wasihoji kuhusu bei za korosho na kahawa kwa wakulima?

Hofu kubwa ya Pengo wakati ule – na naamini ndiyo hofu kubwa ya baadhi yetu kwenye waraka huu wa Maaskofu ni kwamba, Tanzania imebaki kuwa nchi ya mfano kwa Umoja na Amani yetu kwa sababu ya mgawanyo mzuri wa majukumu baina ya masuala ya kiserikali na yale ya kidini.

Kama Serikali ingekuwa imetangaza Jumapili kuwa siku ya kazi na watu hawataruhusiwa kwenda kanisani, waraka wa TEC kupinga hilo na kuusambaza na kusomwa makanisani lingekuwa jambo linaloingia kichwani. Kama Serikali ingelazimisha watu kufanya mambo ambayo ni kinyume cha misingi na imani ya kidini, waraka ungekuwa na maana kubwa.

Lakini suala la uwekezaji tayari lina mijadala yake kupitia itikadi za vyama. Ziko itikadi zinazoamini kwamba uchumi wa unatakiwa kumilikiwa na dola na watu wake na ziko itikadi za kisiasa zinazoamini uchumi unatakiwa kuamuliwa na nguvu ya soko. Rais wa Awamu ya Tatu, hayati Benjamin Mkapa, aliliweka hili vema kwa kutumia mfano wa paka.

Akimnukuu Kiongozi wa zamani wa China, Deng Xiaoping, Mkapa alisema yeye ni mfuasi wa kuamini kwamba cha msingi ni kuona paka anakamata panya na si paka ni wa rangi gani. Kuna wengine, wanaamini kwamba rangi ya paka ni muhimu kwenye kukamata panya. Ukisoma tamko la TEC, utaona kwamba wao wanaamini katika rangi ya paka. Lakini, hili ni jambo ambalo vyama vinatakiwa kushindana na wapiga kura kuamua. Si jambo ambalo Kanisa linatakiwa kutoa maelekezo – nikimnukuu Pengo; “wanajua nini” kuhusu paka au rangi yake?

Hekima ya Kidini

Wakati TEC ikitoa tamko lake, kulikuwa na dalili ya mgawanyiko wa kidini kuhusu jambo hili la uwekezaji kwenye bandari kupitia kampuni ya DP World kutoka Dubai. Busara ya kawaida kabisa, ilihitaji TEC kufanya tafakuri jadidi kuhusu ni wakati gani na namna gani wangeweza kutoa waraka wao.

Kwa mfano, wapo Waislamu wanaoamini kwamba Kanisa Katoliki limekuwa na utaratibu wa kuwa “wakali” zaidi wakati Rais anapokuwa Mwislamu kuliko Rais anapokuwa Mkristo. Kwamba Rais Samia Suluhu Hassan anakosolewa na kuandikiwa waraka kwa sababu za kidini zaidi kuliko suala lenyewe la uwekezaji.

Na wanatumia mifano kadhaa. Kwamba wakati wa utawala wa Mkapa – aliyekuwa Mkatoliki, Kanisa halikuwahi kutoa waraka wa kusomwa makanisani kuhusu kupinga ubinafsishaji wa viwanda, mabenki na mali nyingine za umma uliofanyika wakati wa utawala wake. Mkapa ndiye Rais aliyebinafsisha mali nyingi za umma kuliko mwingine yeyote.

Hata uwekezaji wa kwanza binafsi kufanywa kwenye Bandari ya Dar es Salaam kupitia kampuni ya TICTS ulifanyika wakati wa utawala wa Mkapa. Wanaoamini kuhusu ukali wa Maaskofu kwa marais Waislamu wanatoa pia mfano wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete ambapo matamko ya namna hii takribani matatu yalitolewa wakati wake. Enzi za Magufuli, waraka ulitoka mmoja – na bado Mkatoliki anayesheshimika na maarufu zaidi alikwenda hadharani kuukosoa.

Kwenye mazingira ya namna hii, kulikuwa na namna bora zaidi ya kuwasilisha waraka huu. Namna hiyo ilikuwa ni kushirikisha wadau wengine kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) . Na hili liliwezekana kwa sababu TEC wenyewe kwenye waraka wao wameonyesha kwamba wamewahi kukutana na Rais Samia kwa umoja wao kujadili kuhusu suala hili Juni mwaka huu.

Sasa, kama TEC, CCT na Bakwata walikutana na Rais kwa umoja wao na kuna mambo ya msingi walikubaliana naye – ilikuwaje waraka huo ukatoka wa dhehebu moja katika mazingira ambayo infahamika kuna kundi linaamini Wakatoliki huwa hawatendi haki kwa Rais Mwislamu? Siku chache baada ya waraka kusomwa kwenye makanisa ya Wakatoliki, Mkuu wa KKKT, Askofu Frederick Shoo, alizungumza hadharani kueleza kuwa bado wana imani kuwa Rais atatekeleza yale waliyokubaliana.

Inawezekana Askofu Shoo pia hakubaliani na spidi ya serikali kwenye utekelezaji wa masuala waliyokubaliana lakini pengine busara ilimfanya ajiepushe na kuweka msimamo mkali wa kanisa lake wakati huu – au akijua kwamba jambo hilo linaweza kuwagawa zaidi wananchi kuliko kupata kile wanachotarajia kukipata.

Bakwata – kwa upande wao, hawajasema chochote, kama ambavyo hakukuwa na taarifa iliyotolewa mara baada ya mkutano baina ya Rais Samia na wawakilishi wa TEC, KKKT na Bakwata. Labda kauli ya Bakwata kuunga mkono wakati huu ingeonekana kama kumuunga mkono Rais Mwislamu dhidi ya Kanisa, au pengine wakati sahihi wa kutoa matamko haujafika.

Kwa bahati nzuri, wenzetu Waislamu wana msemo mmoja maarufu kuhusu tabia ya kusubiri; Innallaha Ma Sabireen (Wamejaaliwa wale wenye Subra). Pengine subra, si jambo jepesi kwa kila mtu – na labda kwa kila dhehebu la dini.

Mwandishi ni Msomi wa Masuala ya Maridhiano ya Kisiasa mwenye Shahada ya Uzamili katika African Politics kutoka Chuo Kikuu cha London School of Oriental and African Studies (SOAS) nchini Uingereza. Anapatikana kupitia email: ekamwaga57@gmail.com
Moja ya vitu a,bavyo ni muhimu kwako Mleta mada linapokuja suala kam hili usiwe mrahisi kuweka nadharia zako kisha na kuaminisha wengine kisa tu huko nyuma ilikuwa imetokea hivyo.
Hata sisi tumeyasoma unayoelezea na kwa taarifa yako usipotoshe watu kuw Pengo alikiri kuwa wameamua ila hawakubaliana nanyo.
Sijui kama u mkatoliki au lah maan mambo mengine ni Mafundisho ya Kanisa. Kila jimbo katolili liko na ile mamlaka (AUTONOMY) ya kuamua tofauti na maamuzi ya maaskofu wenzake na hakuna Askofu mwenye mamlaka ya kumwajibisha askofu mwingine maana umemuweka pengo kama kiranja mkuu wa Kanisa katoliki Tanzania ili hali sio.Hata askofu akiandaa taarifa ya Jimbo lake inapelekwa Roma sio kwa maaskofu wenzie. Ukadrinali ni nafasi tu ya kuweza kupoga kira ya kumchagua baba mtakatfu kwa walio na sifa kiumri na kutoa hizi daraja za kiaskofu inapotokea na sio Mkuu wa kanisa ndo maana hata pale Dar anatakwa Ruwaich kama askofu mkuu na hata kwenye sala za kuliombea kaisa anatajwa Ruwaich na sio Pengo maana Umemshadadia kama msemaji wa kanisa katoliki Tanzania. Kama jambo hulielewi fanya jutafita au uliza usiongee ka mpagani tu.
Tunajua huyo pengo alivyokuwa mempenda mwenda zake na ni haki yake hatuchagulii mtu marafiki wa karibu au maadui.
Maaskofu wana vikao vyao wanavijua wao vya kamati na plennary na hasainiwi mtu kama ulivyoleta porojo humu.
Maaskofu kwa Hitimisho wanajua walichoandika na kusaini.
Hakuna Askofu angekubali kila jumapili parokia zote zisome kitu asichokielewa,
Umesoma mpaka Drarsasa la ngapi Kwanza////
 
Ila wa sasa si hakuna Askofu aliyejitokeza Kuupinga? Si unaona hata rais wa TEC anapigilia Msumari?
 
Umeandika

Moja ya vitu a,bavyo ni muhimu kwako Mleta mada linapokuja suala kam hili usiwe mrahisi kuweka nadharia zako kisha na kuaminisha wengine kisa tu huko nyuma ilikuwa imetokea hivyo.
Hata sisi tumeyasoma unayoelezea na kwa taarifa yako usipotoshe watu kuw Pengo alikiri kuwa wameamua ila hawakubaliana nanyo.
Sijui kama u mkatoliki au lah maan mambo mengine ni Mafundisho ya Kanisa. Kila jimbo katolili liko na ile mamlaka (AUTONOMY) ya kuamua tofauti na maamuzi ya maaskofu wenzake na hakuna Askofu mwenye mamlaka ya kumwajibisha askofu mwingine maana umemuweka pengo kama kiranja mkuu wa Kanisa katoliki Tanzania ili hali sio.Hata askofu akiandaa taarifa ya Jimbo lake inapelekwa Roma sio kwa maaskofu wenzie. Ukadrinali ni nafasi tu ya kuweza kupoga kira ya kumchagua baba mtakatfu kwa walio na sifa kiumri na kutoa hizi daraja za kiaskofu inapotokea na sio Mkuu wa kanisa ndo maana hata pale Dar anatakwa Ruwaich kama askofu mkuu na hata kwenye sala za kuliombea kaisa anatajwa Ruwaich na sio Pengo maana Umemshadadia kama msemaji wa kanisa katoliki Tanzania. Kama jambo hulielewi fanya jutafita au uliza usiongee ka mpagani tu.
Tunajua huyo pengo alivyokuwa mempenda mwenda zake na ni haki yake hatuchagulii mtu marafiki wa karibu au maadui.
Maaskofu wana vikao vyao wanavijua wao vya kamati na plennary na hasainiwi mtu kama ulivyoleta porojo humu.
Maaskofu kwa Hitimisho wanajua walichoandika na kusaini.
Hakuna Askofu angekubali kila jumapili parokia zote zisome kitu asichokielewa,
Umesoma mpaka Drarsasa la ngapi Kwanza////
Umemjibu vema sana, ungemuongezea na tusi.
 
Ila wa sasa si hakuna Askofu aliyejitokeza Kuupinga? Si unaona hata rais wa TEC anapigilia Msumari?
Mkuu tunawajua ma Baba Askofu na misimamo yao- kwa colective responsibility sawa, lakini wako wenye misimamo binafsi
 
Acha kumchafua Kardinali wetu...

Uongo mweupe huo.....

Mzushi wewe....mzushi haswaa....

Mkishindwa hoja mnakimbilia UONGO na "tarnishing image of other people" kwa visingio vya kitoto [emoji15][emoji15][emoji15]


Alichokieleza ni ukweli mtupu usio na chembe ya doa.

kumbuka Gwajima alipomvaa Pengo kuwa amekula maharage ya wapi vile, hajui. Pengo aliwaruka wenzie kwny waraka kama hivi ila ilikuwa ni kwa magufuli
 
Ninachojua ni kwamba kila mwaka Kanisa Katoliki hutoa waraka wakati wa Kwaresimu na nyakati zingine "primarily" kulingana/kuendana na mahitaji ya "Kanisa mahalia" (local church). As far as I know, kabla ya Tanganyika kupata uhuru 1961 Kanisa Katoliki lilikuwa likitoa nyaraka kuhimiza mambo fulani mema au kukosoa mambo fulani yaliyokuwa yakifanyika enzi hizo. Records zangu zinaonyesha mwaka Julai 11, 1959 Kanisa Katoliki lilitoa wakara unaoitwa "Africans and the Christian Way of Life". Wakati wa Mwalimu Juliua Nyerere liliendelea kutoa nyaraka pia za kuhimiza/kukosoa mambo ambayo yalihitaji kuangaliwa kwa makini. Mfano, mwaka 1972 lilitoa waraka unaoitwa "Peace and Mutual Understanding" (Septemba 1972). Vivyo hivyo, katika awamu zingine had leo.

Kwamba wakati wa Benjamin Mkapa (1995-2005) TEC hawakuwahi kutoa waraka (which means kwa miaka 10 walikuwa TEC wali'mute' (hawakusema chochote) hapa ushahidi unahitajika kwa sababu kwenye any "claim" ni vizuri ku'justify'. Kanisa Katoliki enzi na enzi lina namna yake ya "kuinjilisha" which includes addressing socioeconomic, cultura, political and even moral dilemma issues (kama human cloning, genetic engineering, abortion, euthanasia, withdrawal of feeding to the terminally ill persons (whose are in "a vegetative state", homosexuality, extramarital intercourse, rape etc), ambayo siyo lazima iwe sawa au iendane na madhehebu mengine ya Kikristo au hata dini zingine. Hivyo, mtu hawezi kulichagulia Kanisa namna linavyoweza kuwasiliana au kufikisha ujumbe wake kwa waumini wake. It is impossible! Kanisa pia haliwezi kuwachagulia viongozi wa dini zingine namna wanavyoweza kuwasilisha ujumbe wao au kuwahubiria waumini wao. Kila kiongozi yuko huru kuhubiri au kutoa waraka kwa waumini wake kulingana na mahitaji ya waumini wake kama hiyo ni njia mojawapo ya kuhubiri kwa hao viongozi wa hizo dini. "Uniform preaching" (uniformity) naikuta tu hapa kwetu ambao viongozi wa dini wakiwa na jambo watumie njia fulani kufikisha ujumbe wao kwa waumini wao.

Wanasiasa wao wanakuwa huru kusema kile wanachoona kinafaa kwa wapiga kura wao. Kama mtu anakuwa na maoni yake kuhusu jambo fulani katika nchi yake, kwa nini viongozi wa dini nao wasiwe huru kutoa maoni yao kuhusu hilo jambo. Ubaya uko wapi au wanakuwa wamekiuka sheria au utaratibu gani? Hapa kutoa maoni, includes "constructive criticism". Ushauri wangu ni kwamba kujua namna Kanisa linavyoendesha mambo yake jifunze kutoka kwa Kanisa lenyewe (if you can and if you wish) na siyo kutoka kwa maoni ya watu wengine kwa sababu kila mtu ana maoni yake na unaweza ukali'judge' kanisa siyo kwa sababu liko wrong, bali kwa sababu kwa maoni ya mtu au watu wengine liko wrong, which is also wrong in itself. So, we shouldn't be prejudiced, but remain objective if at all we see ourselves objective or impartial critics. Ningekushauri uende kwenye archives za Kanisa Katoliki na ucheki nyaraka zake kuanzia miaka 1950s hadi sasa, halafu ndipo uje useme kwamba miaka ambayo walikuwa viongozi Wakatoliki TEC wali'mute' (hawakukosoa). Pili, kama Kanisa likitoa waraka leo it is useless kusema kwa nini miaka ya nyuma huko hawakutoa nyaraka (if at all it happened). Nikiamua kufanya jambo fulani leo ni uselss mtu kuniambia kwa nini sikufanya mwaka uliopita au mtu akiamua kuanza kuandika makala leo tuanze kusema kwa nini hukuandika mwaka jana au miaka iliyopita. It is illogical!
 
Back
Top Bottom