TAMKO la TEC: Upo uwezekano baadhi ya ma Baba Askofu hawajui kilichomo

wew umejuaje kuwa Pengo ni TISS? hlf kanisa halijui
 
Hivi wewe una maana gani? Issue ya mwaka 2018 unaileta leo ili ionekane ni kuwa ni hii ya kuhusu Bandari. Ukweli ni kuwa kuhusu tamko la juzi, Mwadhama Cardinal Pengo hakuwemo maana ni Askofu Mstaafu. Kwa rejea lipo hapo chini
 

Attachments

Habari za Pasaka[emoji57]

Ongelea tamko la TEC juu ya mkataba feki wa Bandari we vipi
Kwani la bandari ni tamko la kwanza kulitoa ?!!!

Hatuwezi kuwazuia wala kuwapinga kutoa matamko bali tunaangalia "contents" ya matamko tu [emoji1787][emoji1787]

Enheeee shem kwa hiyo maaskofu wakaighushi saini ya mhashamu P.P ?!!! [emoji1787][emoji1787]
 
Huwa sihami kwenye hoja hata siku moja. Nilichokujibu ndicho. Huyo mwandishi wenu ameumba story ambayo haikuwahi kuwepo ili apate pa kusimamia kuijenga hoja yake.
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Kwa hiyo amemzushia mhashamu Pengo ?!!

Duuh yaani unatulazimisha 2+2=7 ?!!![emoji1787]

Kamwaga kawabana "P M B U"....
 
Chezea bahasha toka DP world weye 🤣🤣 ni mwendo wa mapambio tu 😂😂
 
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Kwa hiyo amemzushia mhashamu Pengo ?!!

Duuh yaani unatulazimisha 2+2=7 ?!!![emoji1787]

Kamwaga kawabana "P M B U"....
Uwezo wako wa kuelewa umeulazimisha kufika hapo, sina namna ya kukusaidia
 
Alileta siasa ?!!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]

Unatufanya wanaJF kuwa watoto wa kubugizwa "ubuge"?!!

Hamtoki humu...

Humu Jandoni hamtoki na mazunga yenu....chaliii [emoji1787]

Baada ya kupitishwa jandoni karibu Wanzuki [emoji1787][emoji120][emoji120]
 
Kwani huyu Kamwaga alitakaje ? Wasitoe waraka ? Pili, Kamwaga anasemaje juu ya zile hoja 8 ndani ya waraka? Achilia mbali wawe wanaelewa wote au wachache ? Tuwe makini na akili za tumbo
....hoja ni KUGHUSHIWA kwa ile saini....
 

Kwa Nini Waandishi Mahiri wa Safu Wanapungua?​

By Ezekiel Kamwaga|Published On: November 9, 2018|Categories: Articles|1 Comment


Kwa Nini Waandishi wa Safu Wanapungua?
Na Ezekiel Kamwaga
MIAKA kumi ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete itakumbukwa kwa kuwa na kada maarufu ya waandishi wa safu mahiri ambao waliongeza sana mauzo ya magazeti na kulisha maarifa na taarifa mbalimbali kwa wasomaji wake.

Ingawa ni utawala wa Ali Hassan Mwinyi ndiyo uliofungua milango kwa vyombo vya habari binafsi kufanya kazi zake, kilele cha utendaji na kufahamika kwake kilikuwa wakati wa utawala wa Kikwete ambapo mitandao ya kijamii ilisaidia kupaisha umaarufu wa waandishi hao wa safu.

Katika miaka ya awali ya Rais Mwinyi, waandishi kama Stanley Kamana (RIP), Ndimara Tegambwage, na Kajubi Mukajanga walikuwa maarufu kwa sababu ya kazi zao murua kwa wasomaji.

Kwenye utawala wa Rais Benjamin Mkapa, gazeti maarufu zaidi lilikuwa RAI ambapo wanasafu kama Jenerali Ulimwengu, John Rutayisingwa (RIP), Johnson Mbwambo, na wengine wengi walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kiuandishi ipasavyo.

Kuna wakati watu walikuwa hawanunui RAI kwa sababu ya kilichoandikwa nje (habari) bali walinunua kwa sababu walitaka kuwasoma wanasafu mahiri waliomo ndani.

Sitasahau namna watu walivyokuwa wakinunua RAI mwaka 2005 wakati Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation wakati huo, Salva Rweyemamu, alipokuwa akifanya uchambuzi wa wasifu wa waliokuwa wamejitokeza kutaka kuwania urais wa Tanzania kupitia CCM.

Kwenye utawala wa Kikwete, magazeti yaliyokuwa na wasomaji wengi kwa sababu ya wanasafu yalikuwa ni MwanaHALISI, Raia Mwema, na Tanzania Daima ambapo waandishi kama Privatus Karugendo, Joseph Mihangwa, Ansbert Ngurumo, Ulimwengu, Msomaji Raia, M.M Mwanakijiji, Saed Kubenea, na wengine walijipambanua kwa uandishi wao wenye kalamu kali.

Katika utawala wa Rais John Magufuli – walau kwa miaka hii mitatu ya kwanza, hakuna gazeti jipya wala wanasafu wapya waliojitokeza katika magazeti wanaosisimua watu kama ilivyokuwa huko nyuma.

Kimsingi, kama kuna mtu anayesomwa na watu wengi hivi sasa basi atakuwa ni Mange Kimambi ambaye si mwandishi kitaaluma lakini anaandika taarifa zake kupitia mitandao ya kijamii.

Mimi ninaamini kwamba umaarufu wa Mange unatokana na hali halisi iliyopo nyumbani. Wakati wa utawala wa Kikwete kulikuwa na Bunge lililooneshwa mubashara, vyama vya siasa viliweza kuzunguka mikoani kufanya kampeni na vyombo vya habari vilikuwa na uhuru mkubwa zaidi wa kukosoa kuliko ilivyo sasa.

Kwa sababu hali hiyo ya uhuru imebadilika hapa nchini, mfumo umeamua kutafuta njia nyingine ya kupumua ambayo sasa ndiyo amekuwa Kimambi. Mange alikuwa anaandika tangu wakati Kikwete akiwa madarakani lakini hakuwa maarufu sana kwa sababu aliyokuwa akiyasema yalikuwa yakisemwa hapa pia.

Hata hivyo, hii ni mada nyingine tofauti na mada ya leo. Turejee kwenye hoja yangu mahususi kuhusu kupotea kwa wale wanasafu mashuhuri au kupungua kwa makali ya safu zao.

Hakuna sababu moja pekee ambayo ndiyo imesababisha wanasafu wapungue. Nimekuwa nikiulizwa maswali kuhusu kutoonekana kwa Mbwambo kwenye gazeti la Raia Mwema lakini huyu ni mwandishi ambaye aliaga kabisa wakati akiandika makala yake ya mwisho.

Mbwambo ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Raia Mwema, ameamua kwenda kuishi kijijini kwao wilayani Same mkoani Kilimanjaro tangu mwaka 2015. Huu ni uamuzi wa tofauti na wengine.

Wapo wanasafu ambao wameacha kuandika kwa sababu malipo wanayopewa na vyombo vya habari vya hapa nchini ni kiduchu na mbaya zaidi sasa hawalipwi kwa wakati au hawalipwi kabisa.

Vyombo vya habari vya Tanzania vinapita katika kipindi kigumu kimapato na hivyo vingi vinashindwa hata kulipa mishahara wafanyakazi wake.

Chukulia kampuni kama Sahara Communications ambayo ina tatizo la mishahara kwa wafanyakazi wake kwa takribani miaka miwili sasa.

Kampuni ambayo haiwezi kuwalipa wafanyakazi wake, inawezaje kuwalipa wanasafu ambao mara nyingi si waajiriwa wake? Kwa sababu ya kutolipwa, wapo wanasafu ambao wameamua kuacha kuandika ili kutumia muda wao kufanya mambo mengine.

Wanasafu wengine hawaonekani kwenye magazeti kwa sababu magazeti ambayo yangeweza kukubaliana na uandishi wao yamefungiwa na serikali. Wiki moja iliyopita nilikutana na aliyekuwa Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa, ambaye alinieleza kwamba kwa mwaka mzima sasa amekosa nafasi kwenye magazeti kwa sababu makala zake ‘zinaogopwa’ kwa kuwa zinaweza kusababisha gazeti kufungiwa. Kwa hiyo, kama huoni makala za Jabir Idrissa, ujue sababu mojawapo ni hiyo.

Wapo pia wanasafu ambao wameamua kuacha kuandika kwa kuhofia kwamba wanaweza kuingia matatizoni na vyombo vya dola. Wameamua kutulia hadi pale watakapoona mazingira yamebadilika.

Kuna mwanasafu mmoja mashuhuri ambaye ameacha kuandika kwa madai kwamba siku hizi akiandika, makala zake huwa zinahaririwa kiasi cha kubadili kabisa alichotaka kukisema.

Badala ya kuandika na kushuhudia makala zake zikibomolewa na kuundwa upya, ameamua aache kuandika ili abaki na heshima yake ya nyuma.

Wapo wanasafu ambao sasa wamepata vyeo serikalini na kwa sababu hiyo hawawezi tena kuendelea na aina yao ya uandishi wa kukosoa iliyowapa umaarufu huko nyuma.

Kimsingi, kila anayepunguza makali au kuacha kabisa kuandika ana mojawapo ya sababu nilizozitaja hapo juu.
 
Hivi wewe una maana gani? Issue ya mwaka 2018 unaileta leo ili ionekane ni kuwa ni hii ya kuhusu Bandari. Ukweli ni kuwa kuhusu tamko la juzi, Mwadhama Cardinal Pengo hakuwemo maana ni Askofu Mstaafu. Kwa rejea lipo hapo chini
....msomi asifanye REJEA kuntu kisa ni mwaka 2018 ?!! [emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Kamarada Kamwaga ameeleweka na wenye kutaka kumuelewa.....endelea kuandamana...ameshapita kisu na "zunga" amebaki nalo [emoji1787][emoji1787]
 
Ni jukumu letu kuaminii kuwa watanzania wana uelewa au bado wapo gizani. Na je upande uliochagua upo sahiihi au kwa sababu flanni
 
Ni vema Kamwaga ajikite kwenye hoja za maaskofu na mkataba baina ya Tanzania na Dubai. Suala la kuchambua uelewa wa askofu mmoja mmoja halimuhusu. Kamwaga akumbuke kuwa hata ndani ya serikali kuna uwajibikaji wa pamoja hivyo siyo kila hoja lazima wote wakubaliane lakini wanapokubali wengi hoja ni ya wote!
 
Chezea bahasha toka DP world weye [emoji1787][emoji1787] ni mwendo wa mapambio tu [emoji23][emoji23]
Nina miezi 6 sijanywa bia....unadhani ninapenda kila siku kuwa na chupa hii ya shengena iliyo mbele yangu hapa ubandani?!!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]

Hakuna cha bahasha bali ni ujamaa wangu wa kiafrika na mapenzi yangu makubwa juu ya uadhimu kuntu wa taifa hili[emoji120]
 
Unajua kilichomkuta Pengo kwa hatua ile, au unadhani alistaafu? Kuna usichokijua.
Wenzio wale hawakurupuki ,
Baraza la Maaskofu lina mfumo na misingi yake kwenye kufikia maamuzi ya pamoja.
 
mtoa mada we ni stupid! Yan pengo umeona ndo wa kumtolea mfano humu! We hujui kama mtu akizeeka sana akili yake inachanganyikiwa? Hujiuliz why now kuna cardinal mpya? Yule now n kama mtoto wa miaka saba! Muachen apumzke
 
Unajua kilichomkuta Pengo kwa hatua ile, au unadhani alistaafu? Kuna usichokijua.
Wenzio wale hawakurupuki ,
Baraza la Maaskofu lina mfumo na misingi yake kwenye kufikia maamuzi ya pamoja.
Mkuu naomba uelewe kuwa Mungu hajawahi kuumba kiumbe kinaitwa Askofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…