Siri wa Imwaga
Member
- Jul 29, 2021
- 6
- 8
Lini wananchi wote wa tawala zote wakawa na imani na viongozi wao?Kaka kamwaga hapa kuna mambo mawili umeyaleta...
1.Nani kasema?
2.Kasema nini?
Umeandika vyema kaka na ndio maswali mengi yapo pia ?
Lini TEC ilitoa waraka kipindi cha awamu ya 3 ya taifa hili?Umeandika..
Lini TEC ilitoa waraka kipindi cha awamu ya 3 ya utawala wa nchi hii ?!!!Ila wa sasa si hakuna Askofu aliyejitokeza Kuupinga? Si unaona hata rais wa TEC anapigilia Msumari?
Hata wewe jiulize hivyo hivyo lakini ndivyo ilivyo kwani TISS halisi hujitangaza?wew umejuaje kuwa Pengo ni TISS? hlf kanisa halijui
Kamwaga kanunuliwa kama Kitenge.Maaskfu wote wa Kanisa katoliki wana PHD tena za kusotea darasani siyo za kwenu za kupeana, so wana uhakika na kilichomo na tafiti wamezifanya vilivyo - kwa hiyo ndugu usidanganyike, ule ndiyo msimamo wa wananchi wote wazalendo wa nchi hii.
Umesoma waraka, Kama hujasoma SEMA nikutumie. Ukishasoma nieleze wapo Kuna kasoro.Argumentum ad hominem....
Utetezi wako dhaifu kupindukia....
Hoja si maaskofu hawajui mambo....hoja ni wao kuamua kusimamia MASLAHI yao kwa kuitumia DINI na wananchi kwa ujumla....
Hebu angalia hili....
Ndani ya ule waraka wao wanadai kuwa kwa miaka 60 Tanzania kutowahi kupata mwekezaji wa bandari kutoka "NJE"...[emoji1787][emoji1787]
Hili ni kweli ?!!!!
Nijibu
Mnaacha kujadili waraka mnaanza kujadili watu.Kwenye tamko la bandari uliloliona umeoana saini zao au majina yao tu? Mie nimeona majina yao tu.
Kardinali sio kiongozi mkuu wa kanisa katoliki mahali popote pale au katika ngazi yoyote ile katika nchi husika.Huyu ndiye Kamarada Ezekiel Kamwaga nimjuaye [emoji120]
Huyu ndiye mjamaa mwenzangu wa kweli nimjuaye [emoji120]
Hakika amefunguka KISOMI....
"...mwaka 2018 baada ya waraka ule wa TEC ,Kardinal P.Pengo alisema kuwa "alichomekwa bila ya yeye kujua" [emoji1787][emoji1787]
Hebu jiulize watu wanaweza mpaka "kumchomeka" kiongozi wao mkuu ili tu sisi wanywa Wanzuki tuone kuwa ni msimamo mmoja wa kanisa....hatari sana hili....
Unao ushahidi au unajisemea tu? Kama una huo ushahidi ulete hapa na kisha ndiyo uanze kuuliza.[emoji1787][emoji1787]
Kwanini TEC haikuwahi kutoa waraka wowote kipindi cha awamu ya 3 ya utawala wa nchi hii....
Eager to know[emoji1787]
Ningeanza mimi ku'claim' burden of proof ingekuwa kwangu. Kwa vile wewe ndiye umeanza, lete huo ushahidi na nitakachofanya mimi ni falsify proof yako kwa kukuletea huo waraka halafu tuone utayeyuka au utageuka jiwe? Kujisemeasemea tu hakusaidii. Tunataka kila mtu aseme kile kilichopo na siyo kubunibuni tu mambo kwa sababu unataka kusema hivyo. Bring that proof that hapakuwa na waraka wowote kwa miaka 10 (yaani) kanisa lili'mute' wakati huo wakati awamu zingine limekua likitoa nyaraka. By the way, ni Benjamin Mkapa tu alikuwa Rais Mkatoliki? Na unadhani Kanisa Katoliki lilimwogopa Mkapa, lakini halikumwogopa Mwalimu Nyerere na Magufuli ambao pia walikuwa Wakatoliki? Argument hapa ni ipi? Na je Mkapa anahusikanaje na wakaka wa TEC kuhusu bandari?Likewise can you disprove it?
Mkuu huku kuna vilaza na wapuuzi a.k.a. mambumbu ambao hawawezi kabisa kukuelewa kabisa!Shida kubwa ya jamii yetu au watu-wapagani, ni kwamba hawawezi kutatua matatizo au changamoto zao; au kujenga hoja bila kuangalia shida, hoja, tatizo au changamoto yenyewe.
Kunapotokea tatizo au makosa au changamoto, tunakataa kukabiliana na hali hiyo na badala yake tunatafuta namna ya kuhalalisha udhaifu huo.
Ndio hapo wanawatafuta watu wengine, au vitu au mambo yasioonekana. Hapa utasikia sijui mizimu, sijui mababu, sijui majini, sijui matambiko-miungu, shetani, au Mungu kama sababu au chanzo cha hayo.
Namna hii ya kufikiri ni hatari sana kwa ukuaji na maendeleo ya akili na mwili. Kwa jinsi hii ya kufikiri na kuyaangalia mambo na vitu, mtu au jamii haiwezi kutatua matatizo yake, kusahihisha makosa yake, kugundua au kuboresha achilia mbali uvumbuzi wenyewe.
Kama mtu, au jamii inafanya makosa maana yake kuna shida sehemu fulani na kutatua tatizo hilo sio kushughulika na mtu mwenyewe au jamii yenyewe lakini kutafuta chanzo cha hilo tatizo au shida ni nini.
Tubadilike, tuache kuwaangalia watu, tuangalie jambo lilivyo. Tukubali kukabiliana na ukweli au tabia. Tunapoletewa jambo tuliangalie kwa mapana yote tufanye utafiti mwingi wa kutosha, twenda mbali zaidi ya jambo lenyewe, zaidi faida zake za kiuchumi na kijamii, zaida ya manufaa ya kimwili; lakini manufaa ya kiakili.